HALI YA MZEE MALECELA: Ninawashukuru Sana JF

Status
Not open for further replies.
Tunashukuru kwa kupona kwake, sisi huku bado tunasotea appointment za ma Doctor Muhimbili bila ya mafanikio.
 
Mungu amtangulie na kuimarisha afya yake tunamuombea awe salama bulldozer wetu
 
Namkumbuka sana mzee wangu alikuja kufunga mafunzo ya JKT makutupora - OP vyama vingi wakati huo akiwa Prime Minister: nafikiri Willie @ NYC.USA akuwa bado o'level. Kwata la nguvu lilipigwa kwa niamba ya JKT zote Tanzania, ilikuwa hatari sana - chief wetu wakati huo alikuwa Major General Makame Rashid.

Ugua Pole mzee wetu, nakuomba upone fasta uje uweke mambo sawa CCM inayumba mno mnaweza kupoteza utawala 2015: ingawa nakumbuka msemo wako uliowahi kusema kwamba " Kufikiria kuiangusha CCM ni sawa na kufanya zoezi la kukausha maji bahari ya hindi kwa kutumia ndoo" kweli mzee malecela misemo yako ni kiboko.
 
Sasa mnafanya nini huko Marekani? Rudini nyumbani tuonje wote ugumu wa maisha.
Ole wenu nisikie Someone Malecela anagombea uongozi huko tuendako wakati mnaishi Marekani.
Mtulie huko huko, mtuachie liinchi letu.
 
ha ha ha, wilie @nyu yoki arudi bongo? anaogopa mgawo wa maji, umeme na foleni. pia mishahara huku midogo sana na POSHO ndiyo hizo mmeanza kuziwangia wangia.
 
Hizo kazi unazowaambia wazifanye kwa bidii zikwapi?.

Acha uvivu wa kufikili, hizo kazi akina Mzee mbowe walizipata wapi? Babu yangu aliipata wapi na hao akina Mengi leo wanazipata wapi? Tokeni vijiweni UHURU wa kweli ni kujikomboa kutoka kwenye umasikini, mkiendelea kupigania uhuru wa kuongea na kucheza bao nakuambia mtaendelea kubeba maiti zenu kwa baiskeli wakati tunakula maisha na uhuru wa kipato. Sio Slaa wala mama yake atakaye mpeleka baba yako hospitali, jitahidi wewe binafsi msaidie mzee wako la sivyo ataishia kunyweshwa mizizi na waganga wa kijijini kwenu mwisho wake atakufa kama kuku tu.
 
- Wananchi JF, ninaomba kuwashukuru kwa sala na salam zenu za kheri kwa mzee wetu Malecela, hatimaye juzi ametua hapa US, akifuatana na mama, ni mzima wa afya sana na tunamshukuru sana Mungu kwa miujiza yake!

- Ninawashukuru JF wote mliotufariji na hata wale wengine pia, ndio Demokrasia wote nimewasikia sana, lakini ninawashukuru sana kwamba sometimes tunaweza kuweka siasa na tofauti zetu pembeni, tukawa bina-adam na kurudi tena kwenye tofauti zetu za kawaida tukijali Taifa kwanza!

Love you all people! Thaanks JF, ndio maana hatupo kidogo, lakini tutarudi soon 100% tena!

Willie @ NYC, USA

W.J, bila kukwepa maneno ya kutumia nasema lazima uamini kwamba una tatizo la kimsingi. Pamoja na kwamba taarifa yako inahitaji salamu za pole, wengine lazima tukutolee uvivu. Yabidi ujifunze jinsi ya kuzungumza na makundi mbali mbali ya watu na hata jinsi ya kutoa taarifa za namna hii na hasa ktk JF.

Lakini kama wengine walivyouliza, unajisikiaje mzee Malecela kuokolewa maisha yake ktk nchi nyingine wakati alikuwa na uwezo wa kuweka mazingira ya aina hiyo hiyo hapo Dodoma? Hakuona umuhimu huo? Kwa kupima tu maamuzi yako, unawaonaje wananchi wa Mtera ambao kawaacha bila hata uwezo wa kununua aspirini?

Naomba nisiendelee.
 
Poleni sana William, kwa mashaka na kazi ya kuuguza Mzee wetu John Malecela.Najua akiugua mwana familia ,familia yote inaugua.
Lakini Mungu ni mwema, na ashukuriwe
 
- Wananchi JF, ninaomba kuwashukuru kwa sala na salam zenu za kheri kwa mzee wetu Malecela, hatimaye juzi ametua hapa US, akifuatana na mama, ni mzima wa afya sana na tunamshukuru sana Mungu kwa miujiza yake!

- Ninawashukuru JF wote mliotufariji na hata wale wengine pia, ndio Demokrasia wote nimewasikia sana, lakini ninawashukuru sana kwamba sometimes tunaweza kuweka siasa na tofauti zetu pembeni, tukawa bina-adam na kurudi tena kwenye tofauti zetu za kawaida tukijali Taifa kwanza!

Love you all people! Thaanks JF, ndio maana hatupo kidogo, lakini tutarudi soon 100% tena!

Willie @ NYC, USA

.....Tupo Pamoja Sana Kamanda wetu ..huyu Mungu mwacheni aitwe Mungu!!!......Mbarikiwe sana!!
 
Lakini kama wengine walivyouliza, unajisikiaje mzee Malecela kuokolewa maisha yake ktk nchi nyingine wakati alikuwa na uwezo wa kuweka mazingira ya aina hiyo hiyo hapo Dodoma?

Hivi Nyerere alifia hospitali gani hapa nchini?
 
Twamshukuru Mungu Mkuu, ila nifikishie ujumbe kwa mzee kwamba yeye aweze kuthubutu kukemea maovu ndani ya ccm, yeye sasa ni mzee mwenye busara na hekima, ajaribu kutuhurumia watanzania kwa kuwaambia ukweli ccm.

Kweli Baba.
 
Mungu ni mwema!, mzee wa @ Newyork, Mungu akutie nguvu, tunamuombea mzee wetu, Mungu ampe nguvu na afya njema.
 
William mpe pole Mzee wetu John Cygwiyemisi Malecela, Tingatinga,Dume la zizi.Poleni sana na Mungu awe nanyi wakati huu wa ugonjwa.
Huyo ni mzee wetu mweye track record ambayo ni watu wachache sana hapa Tanzania wanayo.
Wengi humu wanambeza lakini hawajui kuwa kwa huyu mzee ukipata nafasi ya kumona kwa tatizo lolote lile, atalifuatilia mpaka mwisho na kukupa usuluhisho-quality ambayo viongozi wachache wanayo.
 
Mbona hii mnai-neglect? hawa ni wazee kama alivyo Mzee Malecela, pengine hawahitaji kwenda USA lakini je wanapata huduma nyeti angalau kukidhi mahitaji yao. Huu ni wajibu wa viongozi wa nchi na sisi sote kwani kufikia umri wa uzee ni neema ya upendeleo toka kwa Mola.

attachment.php
 
.....Tupo Pamoja Sana Kamanda wetu ..huyu Mungu mwacheni aitwe Mungu!!!......Mbarikiwe sana!!
Huyo sio kamanda, ni kada wa chama magamba! Kada willie tupo pamoja, endelee kumuuguza mzee apate afya njema zaidi.. Mpe pole zetu then twamtakia afya njema!
 
- Wananchi JF, ninaomba kuwashukuru kwa sala na salam zenu za kheri kwa mzee wetu Malecela, hatimaye juzi ametua hapa US, akifuatana na mama, ni mzima wa afya sana na tunamshukuru sana Mungu kwa miujiza yake!

- Ninawashukuru JF wote mliotufariji na hata wale wengine pia, ndio Demokrasia wote nimewasikia sana, lakini ninawashukuru sana kwamba sometimes tunaweza kuweka siasa na tofauti zetu pembeni, tukawa bina-adam na kurudi tena kwenye tofauti zetu za kawaida tukijali Taifa kwanza!

Love you all people! Thaanks JF, ndio maana hatupo kidogo, lakini tutarudi soon 100% tena!

Willie @ NYC, USA

My Prayers. Allah atamuaf
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom