Tum-judge Rais Samia kwa mawazo, maneno, na matendo yake ya sasa akiwa ni Rais wa JMT na siyo kwa alivyokuwa VP!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,556
Wanabodi,

Mimi ni mtu wa mastori mastori hivyo kama wewe sio mtu unaependa mastori mastori just jump this.

Self Proclaimed Psychoanalysis Teacher wa Jf
Humu duniani kuna daraja mbalimbali ambazo watu tunazipata ama kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo.
Daraja la kwanza ni "mtoto," hili kila binadamu hulipata baada ya kuzaliwa, akikua anakuwa kijana au binti, akioa au kuolewa anakuwa mke au mume na akipata mtoto anakuwa baba au mama.

Kuna daraja mbalimbali kwenye kila kitu, darasani kuna monitor, prefect, kuna daraja mtu unaipata kwa kosomea, ukisoma ualimu unakuwa mwalimu, ukisoma udakitari unakuwa dakitari etc. Kuna daraja mtu unapewa kutokana na uwezo, kipaji, kipawa mfano mganga wa kienyeji, mchawi, mwanga, au "fundi" huku kwetu Uswazi.

Ziko daraja zina heshima sana na nyingine kawaida tuu. Moja ya daraja zenye heshima sana ni daraja za viongozi, wawe wa siasa au wa dini, hivyo rais, waziri, mbunge, padri, askofu mchungaji etc.

Ziko daraja za kupewa na daraja za kujipa. Enzi zile naendesha kile kipindi cha kiti moto, kabla ya mahojiano huwa nina kaa ya mgeni wangu na ku brainstorm baadhi ya maswali. Kabla ya kumkaribisha Askofu Zakaria Kakobe kwenye kiti moto nika brainstorm nae maswali, miongoni mwa maswali hayo ni tuhuma kuwa waumini wake wenye dhahabu wanatakiwa kuzileta kanisani zinateketezwa kwa moto.

Nikaomba kwenda kuona hapo zinapoteketezewa ili nishuhudie mabaki, kisha nikamuuliza viongozi wa dini hupewa hizi daraja na mamlaka mfano sisi Catholic daraja zetu huitwa sacrament nazo ni ubatizo, kumunio ya kwanza, kipaimara, ndoa, mpako wa mwisho na kwa viongozi wa kanisa ni utawa, ushemasi, upadirisho, uparoko, uaskofu, ukadinali na upapa. Hivi vyeo hutolewa na wakuu wa kanisa.

Basi nikamuuliza Askofu kakobe hilo daraja la yeye kuwa Askofu Mkuu wa kanisa la FGBF amepewa na nani?
Naomba nisikutajie majibu yake, ila na mimi naomba kujiita humu Jf ni mwalimu wa somo liitwalo Psychoanalysis na nawaomba mnikubalie na msiniulize nimepewa na nani?!

Psychoanalysis ni Nini?

Kwa wale tunao endelea tuanze na Psychoanalysis ni nini na ya kazi gani au inasaidia nini?.
Psychoanalysis ni Nini, na ya Kazi Gani?
Kuna msemo usemao, information is power, yaani ukiwa na taarifa sahihi, unakuwa na nguvu, hivyo hii psychoanalysis ni somo la kujifunza kwa nini watu wana behave kwa namna fulani kwenye situations fulani. Hivyo ukijua tabia za watu, kwa nini they behave the way they behave, wewe unakuwa na power ya kuwafahamu na sometimes bila wenyewe kujifamu, hivyo kwa kuandika humu kuhusu human behaviors, hii inaweza kuwasaidia kubadilika, and changing for the better kwa kupunguza maneno na kuongeza vitendo. Waalimu wakuu wa hili somo la psychoanalysis, ni wawili, Carl Jung na Sigmund Freud.
Carl Jung na Sigmund Freud ni Nani na Walifundisha Nini kwenye Psychoanalysis?
Hawa ni mabingwa wa somo la saikojia ya watu na walijikita katika kufanya analysis za kubaini chanzo, the motive behind, tabia, maneno na matendo ya baadhi ya watu, huku Freud akijikita zaidi katika mahusiano ya kifamilia na Jung akijikita katika mahusiano ya kijamii, hivyo Freud kuheshimika kama mwanzilishi wa psychoanalysis na Jung akawa ni muasisi wa analytical psychology au Jung psychology, tena ingekuwa ni amri yangu, ningeamrisha viongozi wetu wote wapatiwe semina ya Jung Pschology inafundishwa katika kituo cha TAGLA pale IFM, kwa njia ya distance learning, kutawasaidia sana, maana kuna wengine wanadhani kuongea sana, kuhutubia sana, au kuongea kwa ukali na vitisho, ndiko kutalisaidia taifa hili kupata maendeleo!. No way, maendeleo ya kweli hayaletwa na maneno, na ukali au vitisho, bali yataletwa na matendo na mipango mkakati!, Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno
Psychoanalysis ya macho huwa yanasema kila kitu!
Jicho la binadamu linafanya kazi kama kamera na kutunza kumbukumbu kwenye retina yake. Nchi za wenzetu walioendelea wana mpaka uwezo wa ku print kumbukumbu za mwisho kwenye jicho la marehemu aliona nini mara ya mwisho hivyo kupata clue ya kilichosababisha mauaji yake!

Macho huwa yanasema kila kitu. Mimi na dada yangu mkubwa Maria (RIP) baada ya baba yetu Mzee Andrew Mayalla (RIP) kuhusishwa kwenye ile kesi ya mauaji Mwanza ya 1976, tulichukuliwa na baba yetu mdogo Mzee Mathew Kasanga na kulelewa nyumbani kwake, hivyo mimi nimepata malezi ya mama wa kiganda, Norah Katusabe Kasanga, mke wa Mzee Kasanga. Hivyo ni miongoni mwa watanzania wachache wanao wajua vizuri waganda, kitu ambacho ni plus katika lile jambo langu lile! Ukijumlisha ujana kuwa mchumba wa kikenya na baadae wa kinyarwanda ndio usiseme!

Mastory ya Kubaini Mhalifu kwa Kutumia Macho!
Familia ya Kasanga ilikuwa na watoto 6, ukitujumlisha na sisi 2 tunakuwa watoto 8, hivyo its a big family. Hapa ndipo nilipo develop skills za kusoma macho. Ukitokea udokozi au mtoto kaharibu kitu bila kujilikana ni nani, tutachapwa wote mpaka tumtaje kama hatumjui wote tunaishia kuandhibiwa.

Nikaanza kunotice, kwa tulio adhibiwa bila kosa, tunaendelea kuumia kwa muda mrefu lakini kwa mhusika baada ya muda mfupi anakuwa poa as if nothing happened!

Ikafika kipindi likifanyika tukio la kuadhibiwa wote, mimi nagoma kwa hoja kuwa kwanini nichapwe bila kosa kwa kosa la mwingine? Nikajitolea kumbaini mkosaji kwa kumtazama machoni.
Jinsi ya kumbaini mhalifu kwa kumwangalia machoni tuu.
Macho yameumbwa na aibu, hivyo likitokea tukio namtazama mmoja mmoja kwa kumkazia macho, mtu ambaye hakusiki macho yake yatakuwa steady, nikifika kwa mhusika, lazima macho yatacheza cheza na hapo hapo namdakua na kumkazimisha kukiri, hii ikapelekea mimi kuitwa inspector.

Uwezo huu wa kumtazama tuu mtu machoni na kumbaini mkweli na muongo ni tool muhimu kwenye kubaini haki, niliwahi kushauri hata majaji wetu na mahakimu wetu wafunzwe technic hii ya kuwa na jicho la kuibaini haki, kuna circumstances mtu unakutwa kwenye tukio la mauaji with all circumstantial evidence pointing to you, kama Jaji hana jicho la kubaini haki, mtu huyu atahukumiwa kunyongwa na anaweza kunyongwa bila hatia

Naangalia possibility ya kupata course materials nim-convince Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel, ili tuwapige msasa majaji na mahakimu wetu semina ya Jung Psychology. Itawasaidia sana kutenda haki kwenye mhimili wa mahakama kama nilivyo shauri hapa Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Mambo maovu mabaya ya awamu ya 5.
Hakuna ubishi kuhusu kutokea kwa matukio maovu wakati wa awamu ya 5, yakiwemo ya miili yenye majeraha kuokutwa ikielea kwenye viroba, kupotea kwa baadhi ya watu, kwa mtindo wa vanishing into thin air kama alivyopotea mwenzetu humu Ben Saanane na mwanahabari Azory Gwanda na tukio kubwa kabisa ni kuibuka kwa kundi linaloitwa "wasiojulikana" na kushambuliwa kwa Tundu Lissu mchana kweupe kwenye eneo la makazi ya viongozi lenye ulinzi mkubwa.

Matukio yote haya yanahusishwa na serikali ya awamu ya 5. Siwezi kusema kama ni kweli serikali ilihusika au la, ila Tanzania tunao watu wenye uwezo wa kuwabaini wasiojulikana hawa, na wakajitolea kuisaidia serikali yao, kama hapa Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija na hapa WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? lakini serikali haikuonyesha any positive response ya kuuhitaji msaada huu, hivyo kuhesabiwa...

Wakati yote hayo yakitokea, Rais wa sasa Samia Suhuhu Hassan ndio alikuwa VP, hivyo kuna watu wanamlaumu na kumshutumu kuwa na yeye ni mhusika wa matukio hayo, na ndio maana sasa nawafundisha watanzania wenzangu hili somo la kuyatumia macho ya mtu, na kubaini uhusika wake katika tukio fulani la uhalifu, hivyo mtuhumiwa wetu huyu jee alihusika na uhalifu huu?

Sasa kuna hoja hii imeletwa humu Rais Samia amejaa hofu ya Mungu, ndiyo maana unaona akihubiri haki

Japo sisi wana Jf as wana Jf we all equal, ila hatulingani! Kuna wana Jf wa kila aina na hadhi tofauti tofauti na tuna command Jf respect ki tofauti tofauti, hivyo hoja ikiletwa au kuchangiwa na wana Jf wanao command much respect na high respect sio ya kupuuzwa, hivyo miongoni mwa walio changia uzi huu ni mwana Jf huyu anaye command much respect
Umetoka sayari gani ndugu yangu, mbona usahaulifu umekuganda kama shati lililonyeshewa?
Mbona ndiye alikuwa msaidizi mkuu mwaminifu wa Rais aliyepita kwa muda wa miaka mitano?
Je iwapo bosi wake angekuwa hai hadi leo, si angeendelea kuwa msaidizi wake kama zamani?

Hebu nikumbushe ndugu yangu...
  • Je ni wapi aliwahi kuwakemea polisi walipofanya hivyo vitendo anavyovikemea sasa hivi?
  • Ni wapi aliwahi kuhoji utekaji, utesaji, upotezaji wa Watanzania katika hiyo miaka mitano?
  • Ni wapi aliwahi kulalamika au hata kukemea uovu kama ni mcha Mungu kama unavyodai?
  • Ni wapi katika hiyo miaka mitano ya mateso aliwahi kuhoji vitendo vya vikosi kama cha wasiojulikana?
Sasa ndugu yangu, hebu pia naomba unijibu swali lamgu hili...unatafsirije uwepo wake na ushiriki wake katika hiyo serikali na ukimya wake yote hayo yakitendeka?
Ukinijibu nitakuwa na swali la nyongeza.
Hivyo hapa ni kumhusisha Samia na yaĺiyotokea awamu ya 5, hivyo mimi nami ni miongoni mwa tulio changia

Mkuu Mag3, japo aliyeulizwa si mimi ila kwa vile baadhi ya majibu ninayajua, naomba kuchangia

She was not the big boss, naamini unaijua kanuni ya the collective responsibility kwenye utawala husika, hata kama hukubaliani unakaa kimya.

Naamini uliwahi kuisikia ile tetesi ya yule dada wa taifa kumhusu huyu mama, naomba mimi nisiseme it was true kwasababu its not for me to say, natumia kanuni ya uadilifu wa mke wa Kaizari, just tetesi is enough!

Yes angeendelea

She was not the boss then, she is the boss now anakemea

Atakuwa alihoji ila vitu vya ndani havitoki nje. One thing for sure is though alikuwa sehemu ya utawala ule but she was not a part to it, macho aliyomtazama Lissu pale Nairobi hospital speaks everything.

Amini nakuambia kuna vitu vinafanyika behind your back na wewe huvijui kwasababu you were kept in the dark.
Je, unajua ile kabla ya March 17, she was on the dark on what was going on.

She was not the boss then, alikuwa anakemea ndani kwa ndani na Mungu anasikia, kwani kuna mtu yoyote anayejua ni kwanini Mungu alifanya vile?.Vitu vingine acheni.

Mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote kama wasiojulikana wale ni wasiojulikana kweli au ni 'wasiojulikana' tuu, as long as sasa hawapo, ni jambo la kushumuru Mungu.

Hili nimeisha kujibu tangu mwanzo ila kwa sababu hapa nachangia tuu na aliyeulizwa atakujibu pia.
Maadam sasa ni yeye, tunamuona tunamshuhudia akisema na akitenda tofauti, naomba tuwe watu wa shukrani kwa haya, badala ya kuendelea kulalamika na kulaumu yaliyopita, tuwe appreciative kwa haya tunamshukuru sana Mungu kwa mtu huyu.

Sasa ndio naomba niwapeleke kwenye somo la kujifunza kusoma body language na kubaini uhusika wa mtu katika tukio kwa kuangalia macho

Kwanza angalia hizi picha na video, concentration yako ikiwa ni macho.

sami1sd-Copy-950x565.jpg
samia1-Copy-950x531.jpg
sammmif-950x538.jpg
12-7-768x754.jpg
images.jpeg
7-10-768x536.jpg

Google Image Result for https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2017/11/lissu.jpg
Sasa twende Ubelgiji

Hatua ya pili ni uyatazame macho ya Samia anavyo mwangalia Lissu, halafu ujiulize ndani ya moyo wako je, mtu huyu anayeongea na Lissu kwa upendo hivi, anaweza kweli akawa ni mhusika wa tukio hili? Sauti ndani ya moyo wako itakueleza. Hicho unachoelezwa ndio ukweli wenyewe.

Huu uwezo wa kutumia macho na kusikiliza sauti ya ndani yako, ndio uwezo nilio shauri majaji wetu wawe nao ili kuwatendea haki Watanzania.

Hitimisho
Nasisitiza Rais Samia sio malaika ni binadamu, na kwa sisi binadamu, no one is perfect, anaweza kutenda makosa, hivyo akitenda makosa ahukumiwe kwa mawazo yake, maneno yake na matendo yake ya sasa akiwa ni Rais wa JMT na sio kuendelea kumlaumu na kumshutumu na kumkosoa kwa kile ambacho kilitokea awamu iliyopita ambayo japo she was also a part and parcel, kwasababu mtindo wetu wa uongozi ni wa a collective responsibility.

Serikali ikifanya mazuri ni wote, na kukitokea maovu pia lawama ni kwa wote, ila kwa kauli zake za sasa, maneno na matendo, ya sasa, ameonyesha kwa kauli na matendo yenye uthibitisho tosha na ushahidi usiotia shaka kuwa japo she was part and parcel ya awamu iliyopita, she was just silent kutimiza takwa la a collective responsibility but she was not supporting maovu yale na kulithibitisha hili, now on the drivers seat, in full control amebadili mwelekeo kwa kuwaza, kusema na kutenda tofauti.

Paskali
Rejea za Psychoanalysis za mwandishi huyu
  1. Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”
  2. Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila...
  3. Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.
  4. Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity
  5. Psychoanalysis: Je, wajua dress code ya mtu ina represent the soundness of his mind?
  6. This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea?
  7. Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani!
 
Attachments

  • images (1).jpeg
    images (1).jpeg
    6.9 KB · Views: 11
  • samniiii-950x533.jpg
    samniiii-950x533.jpg
    35.9 KB · Views: 12
  • samiwe-950x539.jpg
    samiwe-950x539.jpg
    35.1 KB · Views: 11
  • 18-2-768x957.jpg
    18-2-768x957.jpg
    50.3 KB · Views: 13
  • samiiass-950x550.jpg
    samiiass-950x550.jpg
    36.4 KB · Views: 11
  • samia1-950x531.jpg
    samia1-950x531.jpg
    38.4 KB · Views: 11
  • images (3).jpeg
    images (3).jpeg
    8.8 KB · Views: 10
So far Mama yupo on the right track..

Kuna mambo mengi ameyaweka sawa hususani soko la ajira sasahiv lipo vizuri sana both kwenye private sector na public sector. Labor market is vibrant now than ever.

Ila kuna mambo yanahatarisha mustakabali wa uongozi wake

- Tozo - kipato cha chini wanalalamika so atafute namna bora ya kuongeza mapato ya serikali bila kuwakera wananchi kwenye tozo kila kona

- Kuna watu wanamsnich kwenye uongozi wake inatakiwa awaondoe mara moja.
 
Kwanini umeme umekuwa tatizo nchini kuliko wakati uliopita, kwanini kuna utitiri wa kodi zinazoenda moja kwa moja kwa mwananchi wa chini bila kuangalia uwiano wa kipato chake?

Hiyo dhamira nzuri na yadhati unayozungumza,ni kumnyonga zaidi wa hali ya chini tu, mbona hatuoni serikali ukiwa na mpango wa kupunguza matumizi katika uendeshaji wake?

Bado ni gizaaa,mwanga ukitoka hatutahitaji karabai.
 
So far Mama yupo on the right track..

Kuna mambo mengi ameyaweka sawa hususani soko la ajira sasahiv lipo vizuri sana both kwenye private sector na public sector. Labor market is vibrant now than eve...
Dah, nyie jamaa mna mambo, unamsifu yupo kwenye right track halafu unalalamikia tozo!

Upo kama wale wabunge wa CCM, kwenyr speech zao wanalalamikia mapungufu kibao, mwishoni utawaskia; "naunga mkono hoja"!.
 
Kiukweli unyenyekevu wake anapotoa hotuba, kauli zake na matamanio yake yananifanya niamini ana dhamira njema ya dhati toka moyoni mwake. Huyu mhe rais hataki sifa kama yule aliyepita.

Ana mapungufu yake lkn yanavumilika Sana. Bado Nampa muda
 
Jiwe alikuwa ashauriki na yoyote, na ukithubutu kumkosoa anakutimua au vinginevyo,

Kuna kipindi Makamu wa Rais inasemekana alitaka kuachia ngazi sababu ya kero za jiwe,baada ya kumshauri Jambo, jiwe akapanic nakutema mbovu.

Ni chizi tu atasema kwanini Rais wa sasa akukemea maovu katika awamu ya Tano....mzee alikuwa kiburi haswaa
 
Nchi imemshinda unajua hilo.
Jiwe ndio Nchi ilimshinda akabakia kuteka watu na kuwapa kesi, Rais wa Sasa Ni mchamungu na muwazi kwa kila kitu kwenye serikali yake,

Ni matahila tu na misukule ya bwana yule ndio inampinga na kumtukana Rais
 
Don't be a phony Pascal Mayalla.
Wanabodi,

Mimi ni mtu wa mastori mastori hivyo kama wewe sio mtu unaependa mastori mastori just jump this.

Self Proclaimed Psychoanalysis Teacher wa Jf

Naomba nisikutajie majibu yake, ila na mimi naomba kujiita humu Jf ni mwalimu wa somo liitwalo Psychoanalysis na nawaomba mnikubalie na msiniulize nimepewa na nani?!

Psychoanalysis ni Nini?

Kwa wale tunao endelea tuanze na Psychoanalysis ni nini na ya kazi gani au inasaidia nini?.

Psychoanalysis ya macho huwa yanasema kila kitu!

Jicho la binadamu linafanya kazi kama kamera na kutunza kumbukumbu kwenye retina yake. Nchi za wenzetu walioendelea wana mpaka uwezo wa ku print kumbukumbu za mwisho kwenye jicho la marehemu aliona nini mara ya mwisho hivyo kupata clue ya kilichosababisha mauaji yake!

Macho huwa yanasema kila kitu. Mimi na dada yangu mkubwa Maria (RIP) baada ya baba yetu Mzee Andrew Mayalla (RIP) kuhusishwa kwenye ile kesi ya mauaji Mwanza ya 1976, tulichukuliwa na baba yetu mdogo Mzee Mathew Kasanga na kulelewa nyumbani kwake, hivyo mimi nimepata malezi ya mama wa kiganda, Norah Katusabe Kasanga, mke wa Mzee Kasanga. Hivyo ni miongoni mwa watanzania wachache wanao wajua vizuri waganda, kitu ambacho ni plus katika lile jambo langu lile! Ukijumlisha ujana kuwa mchumba wa kikenya na baadae wa kinyarwanda ndio usiseme!

Mastory ya Kubaini Mhalifu kwa Kutumia Macho!

Jinsi ya kumbaini mhalifu kwa kumwangalia machoni tuu.
Macho yameumbwa na aibu, hivyo likitokea tukio namtazama mmoja mmoja kwa kumkazia macho, mtu ambaye hakusiki macho yake yatakuwa steady, nikifika kwa mhusika, lazima macho yatacheza cheza na hapo hapo namdakua na kumkazimisha kukiri, hii ikapelekea mimi kuitwa inspector.

Uwezo huu wa kumtazama tuu mtu machoni na kumbaini mkweli na muongo ni tool muhimu kwenye kubaini haki, niliwahi kushauri hata majaji wetu na mahakimu wetu wafunzwe technic hii ya kuwa na jicho la kuibaini haki, kuna circumstances mtu unakutwa kwenye tukio la mauaji with all circumstantial evidence pointing to you, kama Jaji hana jicho la kubaini haki, mtu huyu atahukumiwa kunyongwa na anaweza kunyongwa bila hatia

Naangalia possibility ya kupata course materials nim-convince Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel, ili tuwapige msasa majaji na mahakimu wetu semina ya Jung Psychology. Itawasaidia sana kutenda haki kwenye mhimili wa mahakama kama nilivyo shauri hapa Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Mambo maovu mabaya ya awamu ya 5.
Hakuna ubishi kuhusu kutokea kwa matukio maovu wakati wa awamu ya 5, yakiwemo ya miili yenye majeraha kuokutwa ikielea kwenye viroba, kupotea kwa baadhi ya watu, kwa mtindo wa vanishing into thin air kama alivyopotea mwenzetu humu Ben Saanane na mwanahabari Azory Gwanda na tukio kubwa kabisa ni kuibuka kwa kundi linaloitwa "wasiojulikana" na kushambuliwa kwa Tundu Lissu mchana kweupe kwenye eneo la makazi ya viongozi lenye ulinzi mkubwa.

Matukio yote haya yanahusishwa na serikali ya awamu ya 5. Siwezi kusema kama ni kweli serikali ilihusika au la, ila Tanzania tunao watu wenye uwezo wa kuwabaini wasiojulikana hawa, na wakajitolea kuisaidia serikali yao, kama hapa Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija na hapa WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? lakini serikali haikuonyesha any positive response ya kuuhitaji msaada huu, hivyo kuhesabiwa...

Wakati yote hayo yakitokea, Rais wa sasa Samia Suhuhu Hassan ndio alikuwa VP, hivyo kuna watu wanamlaumu na kumshutumu kuwa na yeye ni mhusika wa matukio hayo, na ndio maana sasa nawafundisha watanzania wenzangu hili somo la kuyatumia macho ya mtu, na kubaini uhusika wake katika tukio fulani la uhalifu, hivyo mtuhumiwa wetu huyu jee alihusika na uhalifu huu?

Sasa kuna hoja hii imeletwa humu Rais Samia amejaa hofu ya Mungu, ndiyo maana unaona akihubiri haki

Japo sisi wana Jf as wana Jf we all equal, ila hatulingani! Kuna wana Jf wa kila aina na hadhi tofauti tofauti na tuna command Jf respect ki tofauti tofauti, hivyo hoja ikiletwa au kuchangiwa na wana Jf wanao command much respect na high respect sio ya kupuuzwa, hivyo miongoni mwa walio changia uzi huu ni mwana Jf huyu anaye command much respect

Hivyo hapa ni kumhusisha Samia na yaĺiyotokea awamu ya 5, hivyo mimi nami ni miongoni mwa tulio changia

Mkuu Mag3, japo aliyeulizwa si mimi ila kwa vile baadhi ya majibu ninayajua, naomba kuchangia

She was not the big boss, naamini unaijua kanuni ya the collective responsibility kwenye utawala husika, hata kama hukubaliani unakaa kimya.

Naamini uliwahi kuisikia ile tetesi ya yule dada wa taifa kumhusu huyu mama, naomba mimi nisiseme it was true kwasababu its not for me to say, natumia kanuni ya uadilifu wa mke wa Kaizari, just tetesi is enough!

Yes angeendelea

She was not the boss then, she is the boss now anakemea

Atakuwa alihoji ila vitu vya ndani havitoki nje. One thing for sure is though alikuwa sehemu ya utawala ule but she was not a part to it, macho aliyomtazama Lissu pale Nairobi hospital speaks everything.

Amini nakuambia kuna vitu vinafanyika behind your back na wewe huvijui kwasababu you were kept in the dark.
Je, unajua ile kabla ya March 17, she was on the dark on what was going on.

She was not the boss then, alikuwa anakemea ndani kwa ndani na Mungu anasikia, kwani kuna mtu yoyote anayejua ni kwanini Mungu alifanya vile?.Vitu vingine acheni.

Mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote kama wasiojulikana wale ni wasiojulikana kweli au ni 'wasiojulikana' tuu, as long as sasa hawapo, ni jambo la kushumuru Mungu.

Hili nimeisha kujibu tangu mwanzo ila kwa sababu hapa nachangia tuu na aliyeulizwa atakujibu pia.
Maadam sasa ni yeye, tunamuona tunamshuhudia akisema na akitenda tofauti, naomba tuwe watu wa shukrani kwa haya, badala ya kuendelea kulalamika na kulaumu yaliyopita, tuwe appreciative kwa haya tunamshukuru sana Mungu kwa mtu huyu.

Sasa ndio naomba niwapeleke kwenye somo la kujifunza kusoma body language na kubaini uhusika wa mtu katika tukio kwa kuangalia macho

Kwanza angalia hizi picha na video, concentration yako ikiwa ni macho.

View attachment 2341546View attachment 2341547View attachment 2341549View attachment 2341553View attachment 2341545View attachment 2341556
Google Image Result for https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2017/11/lissu.jpg
Sasa twende Ubelgiji

Hatua ya pili ni uyatazame macho ya Samia anavyo mwangalia Lissu, halafu ujiulize ndani ya moyo wako je, mtu huyu anayeongea na Lissu kwa upendo hivi, anaweza kweli akawa ni mhusika wa tukio hili? Sauti ndani ya moyo wako itakueleza. Hicho unachoelezwa ndio ukweli wenyewe.

Huu uwezo wa kutumia macho na kusikiliza sauti ya ndani yako, ndio uwezo nilio shauri majaji wetu wawe nao ili kuwatendea haki Watanzania.

Hitimisho
Nasisitiza Rais Samia sio malaika ni binadamu, na kwa sisi binadamu, no one is perfect, anaweza kutenda makosa, hivyo akitenda makosa ahukumiwe kwa mawazo yake, maneno yake na matendo yake ya sasa akiwa ni Rais wa JMT na sio kuendelea kumlaumu na kumshutumu na kumkosoa kwa kile ambacho kilitokea awamu iliyopita ambayo japo she was also a part and parcel, kwasababu mtindo wetu wa uongozi ni wa a collective responsibility.

Serikali ikifanya mazuri ni wote, na kukitokea maovu pia lawama ni kwa wote, ila kwa kauli zake za sasa, maneno na matendo, ya sasa, ameonyesha kwa kauli na matendo yenye uthibitisho tosha na ushahidi usiotia shaka kuwa japo she was part and parcel ya awamu iliyopita, she was just silent kutimiza takwa la a collective responsibility but she was not supporting maovu yale na kulithibitisha hili, now on the drivers seat, in full control amebadili mwelekeo kwa kuwaza, kusema na kutenda tofauti.

Paskali
Be REAL.
 
Back
Top Bottom