BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi Mbezi Mwisho hali ni mbaya, abiria tupo wengi lakini mabasi hakuna, kuna watu wako hapa tangu Saa 12:10 Asubuhi (leo Novemba 15, 2023) lakini hakuna msaada wowote.
Hivi viongozi wetu wanaishi wapi mpaka hawaoni hii kero? Kila siku ni kilio cha Mwendokasi tu.
Hapa watu wameshakata tiketi, wengine wana hela za ngama, basi linakuja moja kisha lingine linakuja baada ya dakika 40 au zaidi.
Hakuna mvua kama ilivyosemwa na watabiri, labda ingetumika kama kisingizio, mamlaka zinatakiwa kuwajibika na ikiwezekana viongozi wanaosimamia usafiri huu wawajibishwe au wawajibike wao wenyewe, hii ni zaidi ya kero na shughuli nyingi za uchumi zimesimama.