Barua ya wazi kwa Rais Samia: Viongozi mna tija gani kwenye maeneo yenu ya uongozi kuboresha maisha ya wanaowaweka madarakani?

Godfrey Bishanga

New Member
Aug 5, 2017
2
4
VIONGOZI MNATIJA GANI KWENYE MAENEO YENU YA UONGOZI, KUBORESHA MAISHA YA WANAOWAWEKA MADARAKANI.

Barua ya wazi Kwa Mhe. Rais wa JMT Dr. S.S.Hassan.

Imeandikwa Na:
Eng.Bishanga, Godfrey Charles (Educator & MP aspirant)
Former MP-DARUSO (USRC)- UDSM
Vibrant & active member of UVCCM (CCM)
Kyerwa-Kagera
Contact: 0755372659
Email: gbishanga90@gmail.com

Barua hii ya wazi imeandikwa Kwa Mhe. Rais Kwa sababu mbili ambazo ni:

1. Mhe. Rais Kama taasisi, hivyo hii barua itagusa viongozi na madaraka yote yanayoundwa na chombo cha Urais.

2. Kuwakumbusha wenye madaraka, kuwajibika na kuwa hizo nafasi walizonazo ni mali ya wananchi, wawatumikie

Ni wazi Tija ya Mhe. Rais Kwa Taifa letu inaweza kuonekana vizuri bila kupigiwa chapuo Kama viongozi (wasaidizi) na madaraka yote ndani yake na chini yake itafanya wajibu wake ipasavyo. Na pia tija yaweza isionekane Kama viongozi kwenye maeneo yao ya uwajibikaji wakafanya ovyo.

Nisipige maneno matupu, nianze kwa mfano hai, mkoa wa Dar es salaam Kwa jinsi ulivyo asili yake, ukuaji wake na kuongezeka Kwa watu Kwa kasi kubwa, mimi naamini pia ni mkoa anzilishi (Pilot) wa mambo mengi ya kimfumo kiasi kwamba serikali uanzisha mifumo mbali mbali Dar wakiwa na lengo la kujifunzia (case study) na kwamba ikifanikiwa waipeleke mikoa mingine ya Tanzania.

Kwa mfano, Niongelee tena Kwa Mara nyingine USAFIRI WA MWENDOKASI (UDART) mwaka 2019 baada ya kuhitimu shahada ya kwanza chuo kikuu cha Dar es salaam , niliwashawishi wenzangu wanne tuungane tutafuta suluhu ya changamoto ya Usafiri wa mwendokasi, Kwa sababu Kwa kipindi hicho mwaka 2020 kulikuwa na changamoto nyingi sana za usafiri Kama ilivyo leo, yaani hazijaisha! Hivyo basi mimi na wenzangu tukaja na mradi (Project) ya namna ya kuboresha uendeshaji na kutatua changamoto zinazoikumba huduma hii ya usafirishaji rejea andiko letu Kwa uchache kwenye link hii hapa chini

Barua ya Wazi kwa Waziri Mkuu, Kassim Majiliwa (mb)

Tulifanikiwa na kupokelewa vizuri Ofisi za UDART makao makuu. Na tukafanya wasilisho (presentation) nzuri sana na kimsingi tuliweza kujibu maswali yao na solutions (majawabu) ya changamoto Kwa kiasi kikubwa tuliyatoa. Na tukapewa ahadi hewa mpaka leo, hakuna mrejesho. (tuyaache Hayo)

Tuzungumze ya leo; Mwendokasi (UDART) kunashida, Wananchi wengi wanaotumia usafiri huo, ukiwasikiliza wanasema hizi shida wanazozipata ni bora warejeshewe njia zao (routines) na magari yao ya kawaida au huduma zote za mwendokasi binafsishwe na apewe shirika binafsi (private sector) kuendesha.

Sasa hiko hivi Kampuni ya UDA Rapid Transit Public Limited (UDART) inamilikiwa na Shirika la Usafiri Dar es Salaam Limited (UDA) taasisi ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo yenye Hisa nyingi na mwaka 2019, serikali iliongeza hisa zake katika umiliki wa UDART kutoka asilimia 51 hadi asilimia 85.

Kampuni ilianzishwa nchini Tanzania chini ya sheria ya kampuni tarehe 19 Disemba 2014 ikiwa na usajiri wa nambari 113954. Mfumo huo unasimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), huku huduma za mabasi zikiendeshwa na Usafiri Dar es Salaam Rapit Transit (UDART). UDART ilianzishwa na kampuni ya mabasi ya Usafiri Dar es Salaam (UDA), ikishirikisha sekta ya umma na binafsi, pamoja na waliokuwa waendesha daladala.

Je, unajua UDART inamagari mangapi hadi Sasa? Na yeye ukubwa gani?

Je, unajua Kwa siku moja , UDART wanaingiza kiasi gani?

Jibu ni; mwanzoni mwa shughuli za UDART mwaka 2016, kulikuwa na Kundi la mabasi 140 yenye uwezo wa kuhudumia takribani watu 200,000 Kwa siku. Hapo awali mfumo ulingiza mapato ya hadi TZS 130 MILLION Kwa siku. Mwaka 2019 ,UDART iliongeza mabasi 70 na kufanya jumla ya mabasi Hayo kufikia 210. Na katika robo ya Kwanza ya mwaka 2022 serikali ilitoa zabuni Kwa mwendeshaji wa pili , Kuleta mabasi 95. Hivyo kufanya jumla ya mabasi 305 Kwa Sasa. Malengo Yao ni kuhakikisha wanabeba abiria 635,000 Kwa siku, ambavyo itaongeza mapato Kwa asilimia 317% Sawa na Mara tatu ya mapato ya awali hivyo kufanya Kwa siku wakusanye takribani TZS.400 MILION.

Sasa tujiulize, mradi Kama huu wenye miundombinu binafsi na kipekee Kama hii, yenye uhakika wa mapato Kama hivi, VIONGOZI mnafanya nini maofisini kwenu? Mbona Huduma hii inawafia mikononi mwenu? Mabus yote ya abiria 305 yanafanya Kazi? Yako wapi? Mapato Hayo yote yaani Milion 130 hadi milion 400 Kwa siku yanaenda wapi wapi? Kufanya nini?

Tarehe 29/11/2023 magari mapya ya size ya Kati yameonekana barabarani bila ya kuandikwa Vituo vyao vya usafiri. Sasa napenda kuuliza huo Ndio ule mpango wa mwekezaji wa pili wa magari 95 ? Ambaye UDART (serikali) imempatia tenda ya kuleta magari mapya? Na Kama jibu ni Ndiyo, mmeshajiuliza shida hasa ni ipi ,ya kushindwa kuuendesha mradi huu kama inavyotakiwa (effectively)?

My take:
UDART imefeli kuendesha huu mradi, na mtu mwenye akili sawasawa atashindwa kuwaelewa yaani mmeshindwa kivipi? Kwa pesa zote hizo mnazokusanya? Kwa miundombinu yote hiyo iliyopo? Swali litakuwa tu WHY??……..Basi yafuatayo naamini Ndio yanawafelisha kwenye utaratibu wenu.

1. Poor Planning; hii inasababishwa na kufanya Kazi Kwa Mazoea wakati, huduma ya usafiri wa mabasi ya mwendokasi (BRT) ni jambo la kimifumo kote duniani, haiwezekani unataka ufanikiwe wakati mifumo yote ya kisasa (Digital) umeiuwa, mfano. Ni BRT gani duniani mtu anacheleweshwa kwenda atakako yaani anakaa kituoni zaidi ya Lisaa au dk. 30? Yaani ni vituko, ukiuliza wanasema “ Operation costs “ kivipi ? Yaani magari mengine yamepaki tu kituoni, abiria wamejaa vituoni. Ukiuliza kuhusu magari yaliopaki wanasema mengine mabovu. Yote hii ni kuonesha jinsi gani hamna plan ya kuhakikisha kuwa abiria hawasongamani vituoni na magari yote yanafanyiwa service Kwa wakati .

Suluhisho
Mfumo wa kadi za kidijitali urudi yaani mfano kituo kiwe na uwezo wa kutambua abiria wangapi wamekata tickets za kwenda mahali fulani Kwa mfano mbezi, kivukoni,kimara au moroco Alafu mfumo wenyewe uweze kusaidia bus husika kuitwa kuchukua abiria wa kwenda watakako. Pia jambo wanalosema la “Operation costs” Linatatulika Kwa kuwa na good “financial analysis” hivi Hayo makusanyo yote ya siku zaidi ya milion Mia 2 hadi milion Mia 4, mnatumia vipi kwenye mapato ya “Cash inflow & cash outflow”. Mnafanya biashara kimazoea, au la kuna WIZI sana.

2. Poor monitoring & Evaluation; yaani sijui kwanini tu mambo mengi yanayoendeshwa na serikali, hakuna(ga) kabisa uwajibikaji (accountability) hasa kwenye hizi sekta zinazojiendesha zenyewe ( parastatals) . Zinafanya mambo Yao kimazoea yaani Hakuna muda wa kujitafakari tulipotoka, tulipo na tunapotaka kwenda( Evaluation). Wao ni kuamka tu kwenda kazini , hawajui kwamba ili kitu kidumu na kikuwa lazima ufanye uhakiki na usimamizi wa Mara Kwa Mara (Monitoring) Kwa kuzingatia malengo na madhumuni ya mradi.

Suluhisho
Hii sekta ikabidhiwe Kwa mtu binafsi (Private sector) yaani amiliki hisa zote (100%) serikali itulie kupokea Mulabaha tu, na pengine serikali inaweza kutumia vyombo vyake kama CAG kufanya Kazi yake kawaida kama anavyofanya kwenye mashirika na vyombo vya serikali mbalimbali. Kwasababu naamini private sector (mtu binafsi) atakuwa na uchungu wa pesa kupoteza, na pia atakuwa na nia ya kutaka kukuwa haraka.

MWISHO
Tija ya viongozi mahali penu pa utawala inaonekana Kwa kuwezesha na kurahisisha maisha ya wananchi kutokana na shughuri mbalimbali za kila siku za wananchi, kwasababu usafiri wa mwendokasi ni muhimu sana kwa wananchi wa Dar es salaam lakini kwasasa umekuwa Kero kubwa,umeleta usumbufu kwa wananchi hasa kuwafanya watu kuchelewa makazini na majumbani kwao. Ewe mkoa wa mkoa wa Dar es salaam Ndugu Albert chalamila unamsaidia ndugu Rais wa nchi na wananchi wake, vipi kwenye hili jambo.
 
Back
Top Bottom