Hakuna mantiki kutoa ajira kwa usawa baina ya wanawake na wanaume ilihali mzigo wa kutunza familia unabaki kwa mwanaume

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,066
40,725
Haina mantiki, na hakuna logic yeyote kwa kutoa nafasi za ajira kwa usawa baina ya wanawake na wanaume ilihali mzigo wa kutunza familia pamoja na huyo mwanamke mwenye ni la mwanaume kwa 100%. USHETANI!

Haina mantiki, na hakuna logic yeyote ya kumuongezea mwanaume mzigo wa kulipa house girl wakati mama wa watoto anaepaswa kuwalea yupo, kana kwamba haitoshi, mwanaume inabidi aanze kugombania ajira chache zilizopo na mwanamke, mwanamke ambae tayari anatunzwa na mumewe, hivyo yuko tayari kufanya kwzi ile ile kwa mshahara mdogo zaidi, sababu tayari mume wake analea familia na kumtunza na yeye, hivyo hata akilipwa laki 2 kwa mwezi ni sawa tu, sasa mwanaume hawezi kushindana na mwanamke kwenye soko la ajira! Kumbukeni mwanamke anatafuta pesa ya kubadilisha mawigi na kucha tu, ila a man really needs the money kutunza familia yake! USHETANI!

Kana kwamba haitoshi, tunatoa nafasi za upendeleo kwa wanawake ambao tayari wanatunzwa na waume zao, vipi kuhusu wanaume wanaolipa kodi za nyumba, ada, matubabu, chakula , mavazi nk? Yeye kwanini hapendelewi?

Familia zinavurugika, watoto wanarudi nyumbani kutoka shule hawamkuti mama yao, wanakutana na dada wa kazi, cha maana hakuna, maana mshahara wenyewe unaishia kwenye nauli tu za kwenda na kurudi, jamani, wanawake acheni viherehere, kaeni majumbani mlee watoto wenu.., kuwaacha na wadada ndio mwishowe wanakuwa wahuni. Baba yupo kazini, na wewe upo kazini? Stupid!

Mwisho wa siku na housegirl anakusaidia na kubeba mimba sasa, ndio mkome! Ushetani tu
 
Kwa mabadiliko ya dunia na mtindo wa maisha minafikiri....Mwanaume anapaswa asikose iwezo ufuatao:-
1. Akili ya kumuona na kisha kumpata mke.
2. Akili ya kuishi na mke.
3. Akili ya kulea familia.
Mimi naamini kwamba, Mungu akikupa hayo mambo matatu basi hizi lawama zote hazito kuwepo zaidi ya tofauti za kawaida.
Na siamini kama mke akiajiriwa/akijiajiri ama kujishughulisha inabadili tabia yake ama kufanya mwanaume asifulfil majukumu yake kama mume na baba wa familia.
 
Lemme tell you something FRANCIS DA DON na naandika haya nikiwa hapa kwenye kiti changu ofisini tangu saa 12 asubuhi.

Hakuna mwanamke mwenye akili timamu anapenda struggle; hakuna mwanamke anapenda kuacha watoto wake wa-cuteee akaenda kupewa stress na kiongozi wake kazini, wafanyakazi wake au wateja.

Haiba ya kike ni kung'aa, kupendeza and nurturing everything kwenye mazingira yako.

Haya mambo yamesababishwa partly na wanaume ambao somewhere walikengeuka na aidha kutelekeza familia au kutotoa huduma kikamilifu. Hii imeipa nguvu wave ya women empowerment na feminism.

Wamepelekea sasa kuharibu hata wale wanawake ambao wanatunzwa tu poa na waume zao kujiona hawako salama na wanahitaji kujilinda kwa kuhangaika ila hatupendi haya mahangaiko!

Sababu ya sisi kutotumia hayo mapato yetu kwenye ustawi wa familia ni kwa sababu kwanza tunaamini sisi tunachuma for the best interest of our children as opposed to men ambao wanachuma for the best interest of whatever means the most to them (inaweza kuwa mamaake, mchepuko n.k) so tunatunza pesa ili siku ikitokea interest yako imeshift, wanetu waendelee kuishi poa.

Pili hatuchangii kwa sababu tunaona it is unfair that mimi licha ya kwenda kazini lazima nihakikishe kila kitu kimeenda sawa nyumbani (hii mental load haizungumziwagi) na kuhakikisha mume na watoto wako comfortable hata ikimaanisha kuamka saa 9 usiku. So pesa yangu natumia mwenyewe nijuavyo kwa sababu nina mchango mwingine natoa hata kama sipo nyumbani physically.
 
Hahah na wasioingia kwenye ndoa wasipewe ajira kisa majukumu ya wanaume?kwani kwenye kuomba kazi Kuna kigezo Cha ndoa?wengi wanaingia ndoani wana kazi zao tayari🙏so man up,tafuta hela wewe🤔na wanaume walioajiajiri kama deeppond nao wapate wateja wengi kuliko wanawake waliojiajiri kwakua Wana mzigo wa kutunza familia?🤣🤣🤣hoja yako imekaa kulialia, wanaume hamlii🤣🤣🤣nyinyi ndo ninyi,miamba,vichwa vya familia,waamuzi,watafutaji pesa,🤣🤣🤣so man up🏌️🏌️🤺
 
vyo kwa sababu nina mchango mwingine natoa hata kama sipo nyumbani physically.
Sasa mwanaume anapolazimishwa kugombea ajira na mwanamke unategemea nini? Mwanaume kiuhalisia anahitaji kiasi flani minimum cha pesa ili kutumiza majukumu yake, anaenda kwenye soko la ajira anakuta kazi ya kulipwa laki 5 mwanamke anaifanya kwa laki 2 sababu yeye na familia yake inatunzwa na mwanaume tayari. hapo tayari mwanaume anawekewa mazingira ya kuikimbia au kutelekeza baadhi ya majukumu yake katika familia, kwahiyo tunarudi pale pale, kwamba hapatakiwi kuwa na usawa katika ugawaji ajira ilihali mizigo yetu inatofautiana katika jamii.
 
Lemme tell you something FRANCIS DA DON na naandika haya nikiwa hapa kwenye kiti changu ofisini tangu saa 12 asubuhi.

Umeelezea vizuri Sana. Hata mwenye Akili kisoda ataelewa.

Kuna sehemu wanaume tulipuyanga, na wengi walioanzisha hiyo movement ya women empowerment ni Watoto wakiume waliolelewa na Mama zao na kutelekezwa na Baba zao.

Wanawake Hawana huo uwezo wa kujipa nguvu bila ya Wanaume. Hata hivi Leo wanaume wakiamua Wanawake wakae nyumbani Hilo linawezekana.
Lakini tatizo linakuja wapo wanaume ambao hawajui wajibu na Majukumu Yao kama Wanaume.

Wengine wanajiona miungu watu(na hawa wengi ndio watesaji wakubwa) hivyo wanaume wenye Akili hawatakubali Dadazao, wake zao, Mama zao na Binti zao wateseke kisa wanaume Fulani wapumbavu
 
Hahah na wasioingia kwenye ndoa wasipewe ajira kisa majukumu ya wanaume?kwani kwenye kuomba kazi Kuna kigezo Cha ndoa?wengi wanaingia ndoani wana kazi zao tayari🙏so man up,tafuta hela wewe🤔na wanaume walioajiajiri kama deeppond nao wapate wateja wengi kuliko wanawake waliojiajiri kwakua Wana mzigo wa kutunza familia?🤣🤣🤣hoja yako imekaa kulialia, wanaume hamlii🤣🤣🤣nyinyi ndo ninyi,miamba,vichwa vya familia,waamuzi,watafutaji pesa,🤣🤣🤣so man up🏌️🏌️🤺
Hapa nazungumzia social impact ya ujumla katika jamii ya kulazimisha usawa wa ajira baina ya makundi mawili yasiyo na mizigo sawa katika jamii.
 
Umeelezea vizuri Sana. Hata mwenye Akili kisoda ataelewa.

Kuna sehemu wanaume tulipuyanga, na wengi walioanzisha hiyo movement ya women empowerment ni Watoto wakiume waliolelewa na Mama zao na kutelekezwa na Baba zao.

Wanawake Hawana huo uwezo wa kujipa nguvu bila ya Wanaume. Hata hivi Leo wanaume wakiamua Wanawake wakae nyumbani Hilo linawezekana.
Lakini tatizo linakuja wapo wanaume ambao hawajui wajibu na Majukumu Yao kama Wanaume.

Wengine wanajiona miungu watu(na hawa wengi ndio watesaji wakubwa) hivyo wanaume wenye Akili hawatakubali Dadazao, wake zao, Mama zao na Binti zao wateseke kisa wanaume Fulani wapumbavu
Tuache hayo ya juu ambayo nilishamjibu. Kwahiyo hapo mwishoni unasema mimi ni mpumbavu kwa kuona mzani umeyumba, sivyo?
 
Mleta mada Hayo hayahusu serikali hakuna anayejua kuwa mkipokea mshahara wote wawili huko ndani ni mwanaume tu ndiye anaumia
Hayo ni yenu huko vyumbani kwenu serikali haiwezi kuja kuchungulia huko.nfani na kusimamia matumizi ya.pesa iliyowapa mishahara
 
Tuache hayo ya juu ambayo nilishamjibu. Kwahiyo hapo mwishoni unasema mimi ni mpumbavu kwa kuona mzani umeyumba, sivyo?

Sijataja mtu Fulani ni mpumbavu Ila nimeeleza wale wanaume wenye tabia za unyanyasaji, umungumtu, kutaka kutetemekewa Kwa vitu vya kijinga, wanaopiga Wake zao(Kwa sababu Hawana Akili ya kuwaongoza), wanaowadhalilisha na kupendwa kuombwaombwa kila kitu, wanaopenda kuingilia mambo binafsi ya Wake zao, hao ndio ninaowazungumzia kuwa ni wapumbavu.

Kwa upande wangu, ninaona ni Sahihi Wanawake kufanya Kazi, Kwa sababu wamenyanyaswa na kuteseka vya kutosha.

Sisemi kuwatetea au kumaanisha hawana madudu Yao, Ila nazungumzia uhalisia WA Yale yanayotokea kwenye jamii yetu.

Kimsingi Mimi MKE wangu, mabinti zangu NI lazima wafanye kazi ili wawe huru na wasiwe na unafiki nafiki wa kijinga, wasionewe na wajitegemee. Kama ni kusaidiana na mumewe wasaidiane Kwa mapenzi.
 
Mke wako na mabinti zako? Au watarajiwa unamaanisha, maana i doubt kwa haya maelezo uliyoyatoa.

Anyway, hapawezi kuwa na usawa wa aina yoyote ile katika utoaji wa ajira kwa makundi mawili yasiyo na mizigo sawa katika kuhudumia familia na katika jamii kiujumla, haiwezekani, ni kuzidi kumoa mwanume ugumu wa maisha ambao haupo.
 
Sasa mwanaume anapolazimishwa kugombea ajira na mwanamke unategemea nini? Mwanaume kiuhalisia anahitaji kiasi flani minimum cha pesa ili kutumiza majukumu yake, anaenda kwenye soko la ajira anakuta kazi ya kulipwa laki 5 mwanamke anaifanya kwa laki 2 sababu yeye na familia yake inatunzwa na mwanaume tayari. hapo tayari mwanaume anawekewa mazingira ya kuikimbia au kutelekeza baadhi ya majukumu yake katika familia, kwahiyo tunarudi pale pale, kwamba hapatakiwi kuwa na usawa katika ugawaji ajira ilihali mizigo yetu inatofautiana katika jamii.
Kwa dunia ilipo at the moment, usawa unatakiwa uwepo kwa sababu kuna familia nyingi za single parents, kuna wanaume walio ndoani na hawatoi senti tano, lakini pia hata katika kulea wazazi kaka zetu wanatutegea kwa kujua tuna ajira hivyo huu usawa labda usingekuwepo a long time ago but sasa hivi uwepo tu dunia ishavurugika na waliovuruga ni wanaume wenyewe.
 
Au basi tuseme hivi, maisha hayana formula, tuishie hapo.
 
Lemme tell you something FRANCIS DA DON na naandika haya nikiwa hapa kwenye kiti changu ofisini tangu saa 12 asubuhi.

Hakuna mwanamke mwenye akili timamu anapenda struggle; hakuna mwanamke anapenda kuacha watoto wake wa-cuteee akaenda kupewa stress na kiongozi wake kazini, wafanyakazi wake au wateja.

Haiba ya kike ni kung'aa, kupendeza and nurturing everything kwenye mazingira yako.

Haya mambo yamesababishwa partly na wanaume ambao somewhere walikengeuka na aidha kutelekeza familia au kutotoa huduma kikamilifu. Hii imeipa nguvu wave ya women empowerment na feminism.

Wamepelekea sasa kuharibu hata wale wanawake ambao wanatunzwa tu poa na waume zao kujiona hawako salama na wanahitaji kujilinda kwa kuhangaika ila hatupendi haya mahangaiko!

Sababu ya sisi kutotumia hayo mapato yetu kwenye ustawi wa familia ni kwa sababu kwanza tunaamini sisi tunachuma for the best interest of our children as opposed to men ambao wanachuma for the best interest of whatever means the most to them (inaweza kuwa mamaake, mchepuko n.k) so tunatunza pesa ili siku ikitokea interest yako imeshift, wanetu waendelee kuishi poa.

Pili hatuchangii kwa sababu tunaona it is unfair that mimi licha ya kwenda kazini lazima nihakikishe kila kitu kimeenda sawa nyumbani (hii mental load haizungumziwagi) na kuhakikisha mume na watoto wako comfortable hata ikimaanisha kuamka saa 9 usiku. So pesa yangu natumia mwenyewe nijuavyo kwa sababu nina mchango mwingine natoa hata kama sipo nyumbani physically.
Saa 12 asubuhi upo ofisini wkt server ime log post yako 9:22 AM? Kila mwanamke yupo tofauti. Lkn kitu kimoja kinachowafanya wafanane ni kwamba hawapendi ku share income yao na waume zao. Ni wabahili sana hata kwa watoto waliyowazaa hawataki kutumia sentano if they can get away with it. Hii hoja yangu ya mwisho siwezi kusisitiza vya kutosha maana it’s a fact of life kwa wanandoa wengi sana. Wanawake wanapenda wapewe na wachukue tu. Ni one-way street . Ukimwacha mke utaona quality of life yake itaporomoka ghafla. Na ukimwachia watoto ukasepa zako hapo ndiyo utakuwa umemmaliza kabisa hadi kifo.
 
Back
Top Bottom