Kuna usawa kati ya Mwanaume na Mwanamke lakini Mume na Mke hakuna usawa

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,102
22,539
Salaam shalom!!!

Mtu na asikudanganye, Kuna usawa kati ya Mwanaume na Mwanamke,

Lakini hakuna usawa kati ya Mke na Mume.

Kabla ya NDOA, mtoto wa kike atakuwa chini ya uangalizi wa familia, Baba akiwa kiongozi mkuu Hadi pale atakapokuwa tayari kuingia katika NDOA na kuwa mke wa mtu Mume.

Mungu aliwaumba mwanamke na Mwanaume Kwa Mfano wake ( Mwanzo 1:27),

Mtu Mwanaume na mtu mwanamke katika mwanzo 1:27 ni ROHO, Si katika mwili.

Mwnzo chapter 2, Baada ya Mungu kumwuumba Adam Kutoka mavumbi ya ardhi na kuishi miaka lukuki bila msaidizi,

Ndipo Mungu akaona amletee msaidizi.

Baada ya kuamka Toka usingizini, Adam akakutantayari ameletewa msaidizi, ndipo akasema, Utaitwa Mke, sababu umetoka katika mifupa yangu.

Ewe mwanamke, unazo HAKI zote kama Mwanaume katika nyanja mbalimbali Kijamii ,kiuchumi, kisiasa, nk nk,

Ukipiga hatua na kuingia katika NDOA, jua hapo hakuna usawa ,chumbani ni ofisi ingine kabisa yenye Utaratibu wake.

Chumbani hakuna usawa, mahusiano ya mke na mume ni mahusiano kati ya mtu na msaidizi wake, lazima ukubali kuongozwa, kutekeleza na kubaki na nafasi Yako ya usaidizi, ushauri,ukitii maagizo ya mumeo kiongozi wako Ili familia yenu Ipate KUSTAWI sana.

Ukikaa katika nafasi Yako, ndipo utaona Upendo Kutoka Kwa mumeo.

Angalizo: Mume anayeongelewa hapa, Si Hawa wenye kushinda betting, Si Hawa wachagua KAZI, walevi nk nk ,

NDOA na iheshimiwe na watu wote.

Amen
 
Usawa haupo. Hata wanaotaka huo usawa wakiachiwa majukumu wanashangaa kwanini? Matokeo wanadai wamesusiwa
 
Back
Top Bottom