Hakuna kazi ngumu kama kusoma shule

Hakuna kazi ngumu kama kusoma shule

Haina umuhimu mkuu maana nimeona unataka kunipima na ufaulu wako!!!
 
Alie elewa atueleze kijana anataka kufikisha ujumbe gani kwa wananzengo.

Naona majigambo tu ya balehe hapa
 
Kuanzia 2016 kwa muongozo wa waziri wa Elimu Prof Ndalichako, kuchaguliwa special school ni km hivi.

A, level science mwsho div 1 ya 13, na comb grade AAA - ABB. Kwa arts mwsho div 1 ya 17, comb grade AAA - BBB

O, level mtu aliyepata wastan wa A, huku akiwa na A 4 - 5, std 7.
yap! najua wamechange 2016 ila niliingia pale 2014, 2013 ndo nilimaliza elimu ya sekondari .
 
Mkuu hakuna kazi ngumu kama kutafta pesa , we njoo mtaani ndo utakuja kujua ukweli.Hayo madarasa nimeyamaliza yote sikuona kazi ila kuamisha pesa kutoka mfuko wa mtu mwingne kuzileta mfukoni kwangu haitakaa itokee kazi ngumu kama hii
 
Mkuu sina hakika Kama hadi 2013 zilikuwa bado ni shule za watoto wenye vipaji maalumu kwa uhalisia wake,maana shule hizi zilipewa hiyo hadhi mwaka 1991 na mwaka 1992 zikaanza kuchagua hao vipanga,zikaleta walimu Bora kabisa,kupewa vitabu vingi na budget kubwa. Ni shule pekee za boarding za serikali ambazo wanafunzi wake tulikuwa tunakula wali kuku hata wiki zima,Sasa wewe hiyo uliyosoma nadhani ilikuwa imebaki jina tu ndo maana ukaweza kujiunga na one ya 15
kikubwa nilichojifunza ni kuwa mtu yeyote anaweza kufanya makubwa, kinachohitajika dedication pekee, so hapa tunafuta dhana ya wanafunzi vipanga. kwa maana wale majamaa zangu ambao hawakupangiwa vipaji maalum nilikutana nao chuo na mkopo walipata sawa na mimi.
kikubwa bongo hakuna maajabu yoyote kwa shule za vipaji ,zaidi ya kutengeneza cheti tu cha 1 ya 5. mbaya zaidi mwaka wetu 2016 hadi na div 3 30 pamoja na div 2 72 zilikuwepo 😂😂😂
 
Tatizo mnakalili kuna watu 2007-2009 wana 1 point 3,4,5 na hawakusoma Telecom wala Computer Engineering.

Nina mwanangu alipata 1 point 5 kapiga zake Electromechanical lkn pamoja na one yake kali kapigwa gap la GPA na na mtu aliyepata 2 ya 12.

Kuna mwengine alisoma Ilboru alipiga 1 point 4 kapiga Civil,mwengine nae 1 point 4 kapiga Bsc with Computer Science.

Wapo kibao ambao walikuwa na point kali lakini wakaenda kosoma vitu vingine na kuna wengine wana one kali tu wapo mtaani wanakata mapindi sio kwamba vilaza bali wameamua kufanya na kusoma vitu wanavyo vipenda so acha kukalili.
Upo sahihi sana
 
Inategemea na unachosoma, kama unasoma history, English, Kiswahili, Biology, Economics, Accounting sawa, lakini sio Physics, chemistry and Mathematics.
Inategemea na mtu husika mkuu, wengine tumesoma hizo comb ila hakuna ugumu, sema tyuuh kupambana n lazima.
 
Yote tisa mzee mwenzangu,cha muhimu ni kupata pesa hapo ndio mwisho wa mchezo.

Wenzako wamesoma mpaka PHD walikuwa wanalipwa laki tano lumumba pale,alafu kuna wana wamekimbia umande wana mijengo yao kila siku weekend.
 
Back
Top Bottom