Hakuna kazi ngumu kama kusoma shule

Hakuna kazi ngumu kama kusoma shule

This could either be physical or mental
work is the product of force and displacement. A force is said to do positive work if the force has a component in the direction of the displacement of the point of application
 
Habari za leo wakuu,

Leo nilikua nawaza jinsi kazi ya kusoma ilivyo ngumu.

Nikikumbuka vijana wenzangu ambao nilisha waacha nyuma mara baada ya wao kushindwa kuelewa kinacho endelea darasani, ndipo nagundua jinsi kazi ya kusoma ilivyo ngumu.

Just imagine mkuu unaanza chekechea unasoma mpaka unafika chuo kikuu sio kazi ndogo kabisa hii.

Hii kazi ya kusoma hata wanajeshi iliwashinda, wakaona ni bora watumie miguvu yao tu.

Watu wengine wamo humu Jamiiforums, kazi ya kusoma iliwashinda. Utakuta mtu anarudiaga mitahani tu mara kumi bado haperform tu.

Nakumbuka kuna rafiki yangu mmoja shule ya msingi ni alikaririshwa madarasa mara 10, la kumi na moja ndio akaperform. Hii kazi sio mchezo bwana.

Yaani kuna jamaa yangu mmoja naye, elimu ya O-level kasoma mara nane ndipo akaperform. Daa ni hatari.

Wewe unayesema kusoma sio kazi ngumu ya nini kukesha kama bundi.

Utakuta mwingine anasinzia darasani au mezani akiwa anasoma.

Vimitihani vya utumishi tu vinakufanya kuwa bundi.

Karibuni kwa maoni sasa.
Ni kweli kusoma sio mchezo na nimeona hili tangu nikiwa shule ya msingi, siku ikitangazwa likizo tulikuwa tunafurahi sana. Mimi tangu kuanza chekechea imenichukua miaka 31 mpaka napata kazi kutokana na kisomo changu. Siku nilipohitimu nilifurahi kiasi ambacho sijwahi kufurahi maisha yangu yote.
 
Kusoma sio kazi sema wakati tuko shuleni tunakuwa na mambo mengi yasiyohusiana na shule kitu ambacho humrundikia mwanafunzi vitu vya kusoma kabla ya mitihani hali inayowafanya watu kuwa mabundi
 
Back
Top Bottom