Hakuna kazi ngumu kama kusoma shule

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,318
8,228
Habari za leo wakuu,

Leo nilikua nawaza jinsi kazi ya kusoma ilivyo ngumu.

Nikikumbuka vijana wenzangu ambao nilisha waacha nyuma mara baada ya wao kushindwa kuelewa kinacho endelea darasani, ndipo nagundua jinsi kazi ya kusoma ilivyo ngumu.

Just imagine mkuu unaanza chekechea unasoma mpaka unafika chuo kikuu sio kazi ndogo kabisa hii.

Hii kazi ya kusoma hata wanajeshi iliwashinda, wakaona ni bora watumie miguvu yao tu.

Watu wengine wamo humu Jamiiforums, kazi ya kusoma iliwashinda. Utakuta mtu anarudiaga mitahani tu mara kumi bado haperform tu.

Nakumbuka kuna rafiki yangu mmoja shule ya msingi ni alikaririshwa madarasa mara 10, la kumi na moja ndio akaperform. Hii kazi sio mchezo bwana.

Yaani kuna jamaa yangu mmoja naye, elimu ya O-level kasoma mara nane ndipo akaperform. Daa ni hatari.

Wewe unayesema kusoma sio kazi ngumu ya nini kukesha kama bundi.

Utakuta mwingine anasinzia darasani au mezani akiwa anasoma.

Vimitihani vya utumishi tu vinakufanya kuwa bundi.

Karibuni kwa maoni sasa.
 
Nimesoma PCM Ila Leo ndo nasikia Kuna lugha inaitwa physics,chemestry na Mathematics kweli awamu ya tano Ina Mambo mengi mno
The language of mathematics is the system used by mathematicians to communicate mathematical ideas among themselves.

Mathematics language use symbols instead of words.

Mfano mtu aliyesoma Degree ya mathematics na aliyesoma degree ya kiswahili ni yupi atajieleza vizuri mbele za watu?
 
work is the product of force and displacement. A force is said to do positive work if the force has a component in the direction of the displacement of the point of application
another definition

Work is an activity in which one exerts strength or faculties to do or perform something:
 
The language of mathematics is the system used by mathematicians to communicate mathematical ideas among themselves.

Mathematics language use symbols instead of words.

Mfano mtu aliyesoma Degree ya mathematics na aliyesoma degree ya kiswahili ni yupi atajieleza vizuri mbele za watu?
Huwezi ukasema PCM then any Engineering degree then ukashindwa kujieleza mbele ya watu either kwa kuswahili au English unless wewe uwe kilaza,na may be hiyo ndo sababu unasema kusoma ni kazi ngumu while wengine tulikuwa tukienjoy to calculate like a machine
 
Back
Top Bottom