Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Kwa hiyo baada ya kujua hukutaka kuwa na rafiki hapo ulipokuwa kijana mdogo?
Rafiki ninaye wawiili mmoja ni bro wangu. Ambao Sina Shaka kuwa naweza beba family yangu tukaishi kwake kula kulala juu Yao. Rafiki manaye you've to polish them ila Ile real friend it happen in rare case Sana.

Nimesoma primary tatu,olevo moja, advance shule tatu,chuo kikuu viwili kimoja hapa nchini kingine kwa Putin Ila Nina only one real friend,ambaye akiwa na njaa naumia na vice versa is the true
 
Umuhimu wa ndgu unapatikana pale kwenye msiba kuoa au kuuguza, ila ndg wengi hawapendi maendeleo ya ndg wegine, watakupenda sanaa ukiwa masikini wa kipato mwenye kujishusha mbele yao, ila usijifanye mujuaji watt wako kuenda English medium, nk hapo watakupenda kiunafiku tu.
Umasikini uliokithiri naona huongeza chuki kwa aliyepata hata hicho kidogo aisee
 
Rafiki ninaye wawiili mmoja ni bro wangu. Ambao Sina Shaka kuwa naweza beba family yangu tukaishi kwake kula kulala juu Yao. Rafiki manaye you've to polish them ila Ile real friend it happen in rare case Sana.
Nimesoma primary tatu,olevo moja, advance shule tatu,chuo kikuu viwili kimoja hapa nchini kingine kwa Putin Ila Nina only one real friend,ambaye akiwa na njaa naumia na vice versa is the true
Aisee, washike Sana hao Mkuu.
 
Waheshimiwa Sana Wana JF, Hbr za jioni? Kama kichwa kinavyosema katika mapito niliyopitia nimegundua kuwa hakuna Binadamu "ANAYEKUPENDA KWA DHATI',. Mwenye upendo wa dhati nawe ni Mwenyezi MUNGU aliyekuumba na kukupa Pumzi na riziki na Wazazi wako tu waliokuzaa na kukulea vema.

Fuatilia visa hivi.
Nikisema nieleze jinsi nilivyotendwa na mtu alieitwa rafiki kwangu, inahitaji uzi kabisa😫
 
Mkuu,

Ni kweli ni mtizamo wangu na uzoefu wangu, si kwamba sijawahi kukutana na marafiki wabaya, nimekutana nao.
Wengine wamenifanya mabaya kuliko ulivyoandika lakini hainifanyi niwahukumu wote.

Nina marafiki wema pia ingawa ni wachache (wako wawili) lakini ni wema kweli kweli tunaelewana na tunabebeana mizigo ya kimaisha.Kuna ndugu tunaweza tusiwasiliane hata miaka 5 lakini si hawa jamaa tuna muunganiko imara
Tunashauriana, tunakosoana na tunaelimishana.

Nb: kuna raha ya kuwa na rafiki asiye ndugu yako, UNAKUWA HURU.
 
Unamuomba mtu 50000 anakuambia hana unasema ana roho mbaya ... unajuaje labda na yeye alikua na shida zake?
 
Rafiki wa kweli ni ndugu zako wa damu, familia na watoto the rest do not care about you aisee.
Mbona mimi ninamjua mzee aliyekuwa anahitaji figo mwanae pekee wa kiume akakataa kujitolea? Akamwambia baba yake ampe 80m na akamwambia hela najua unazo na kweli mzee alikuwa na hela.
 
Mkuu,
Ni kweli ni mtizamo wangu na uzoefu wangu, si kwamba sijawahi kukutana na marafiki wabaya, nimekutana nao.
Wengine wamenifanya mabaya kuliko ulivyoandika lakini hainifanyi niwahukumu wote.
Nina marafiki wema pia ingawa ni wachache (wako wawili) lakini ni wema kweli kweli tunaelewana na tunabebeana mizigo ya kimaisha.Kuna ndugu tunaweza tusiwasiliane hata miaka 5 lakini si hawa jamaa tuna muunganiko imara
Tunashauriana, tunakosoana na tunaelimishana.

Nb: kuna raha ya kuwa na rafiki asiye ndugu yako, UNAKUWA HURU.
Offcourse na Mimi ni mtizamo wangu,sio lazima uwe mtazamo wa wote.Ni namna ambavyo Mimi nilimchukulia na matokeo yake yakawa hasi,Na huyu ni mmoja tu niliyemzungumzia hapa,wapo wengi tu, wengine walikula njama hata kutaka kunifukuzisha kazi lkn MUNGU ni mwema akaninusuru, yaani unamsaidia mtu then baadaye anakugeuka, Aisee niache na mtizamo wangu.Ni vile tu sijataka kuelezea matukio yote kiunagaubaga.
 
Unamuomba mtu 50000 anakuambia hana unasema ana roho mbaya ... unajuaje labda na yeye alikua na shida zake?
Ndugu yangu wewe hujasoma vizuri huo uzi.Mimi ni mtu mzima naelewa ndio maana nililaumu Sana.Kwasababu yeye alikuwa akinikopa at any time.
 
Waheshimiwa Sana Wana JF, Hbr za jioni? Kama kichwa kinavyosema katika mapito niliyopitia nimegundua kuwa hakuna Binadamu "ANAYEKUPENDA KWA DHATI',. Mwenye upendo wa dhati nawe ni Mwenyezi MUNGU aliyekuumba na kukupa Pumzi na riziki na Wazazi wako tu waliokuzaa na kukulea vema.

Fuatilia visa hivi.
Mimi Nilikuwa na rafiki yangu mkubwa ambaye tulikuwa tunasaidiana ktk shida na raha, Lakini kuna wakati nilikuja kuyumba Sana kimaisha jamaa alikuwa vizuri, Siku moja nikaomba anikopeshe 50,000/= (Elfu hamsini tu),jamaa alikataa kunikopesha kuwa hana Hela wakati huo Mimi najua jamaa ana pesa kwasababu yeye mwenyewe alikuwa anasema kuhusu mipango yake na baada ya hapo akaanza kupunguza mawasiliano na ukaribu.

Rafiki zangu wengine waliacha kabisa kuwasiliana na Mimi, wakati nilipokuwa na hali nzuri kiuchumi walikuwa ni watu safi sana wakionyesha kuwa Wana upendo wa dhati kwangu, Kumbe sivyo.

Kisa kingine ni Cha mdogo wangu,huyu alipatwa na matatizo makubwa hadi kufungwa jera,aisee marafiki zake aliokuwa akijidai nao kuwa oh!, Mimi Nina rafiki wengi tulioshibana, aisee walijiweka mbali sana na shida hiyo hata kwenda gerezani hawakwenda,hata kuulizia tu maendeleo yake hawakuthubutu kabisa.Alipotoka ndio wakawa wanakuja kwa aibu wanasema eti "Tuliogopa kuja gerezani", Wengine wakasema "Tulikuwa na mpango wa kuja baadaye", wakati mtu amekaa jera miezi minne.

Hitimisho
Ndugu yangu/zangu ukiwa vizuri kimaisha,kwa maana ya kazi nzuri, biashara nzuri,cheo kizuri,n.k.Usije ukalewa sifa kutoka kwa rafiki zako hao wanakupendea nafasi uliyonayo na si wewe, ukitaka kuthibitisha hilo hebu pata msukosuko kidogo uone jinsi jamaa zako watakavyotoka nduki.

Hivyo ushauri wangu ukiwa na nafasi nzuri jari kwanza Wazazi wako,Famili Yako,Bila kumsahau Mwenyezi MUNGU;Km unataka kumsaidia mtu msaidie tu km Ibada tu na si kutegemea kurudishiwa fadhila. Kuwa na Marafiki ni kitu kizuri lakini uwe mwangalifu,ishi nao huku ukijua wazi kuwa siku mambo yakikuendea mrama lazima hao marafiki zako wakukimbie au wakusaliti.Tujifunze pia kupitia kwa Yesu namna Wanafunzi wake walivyomkwepa wakati wa Mateso yake.
Ukiacha Mungu,wakukupenda kwa dhati anaweza kuwa mzazi wako tu,watoto wanaweza kukutosa pia
 
Mimi hili lilinikuta nikiwa mdogo sana wakati wazazi wangu walipoyumba kiuchumi,marafiki,ndugu na hata wanafunzi niliosoma nao waliingia mitini,ilinibidi nitafute marafiki wenye uwezo wangu ndio ikawa faraja yangu,ilikuwa ni funzo kwangu kwani tokea kipindi hicho sijawahi kuamini kuwa kuna mtu anayeweza kunipenda kwa dhati zaidi ya wazazi wangu,ndugu zangu wa tumbo moja,watoto wangu na Mungu wangu ambaye upendo wake yeye haulinganishwi na chochote....
 
Waheshimiwa Sana Wana JF, Hbr za jioni? Kama kichwa kinavyosema katika mapito niliyopitia nimegundua kuwa hakuna Binadamu "ANAYEKUPENDA KWA DHATI',. Mwenye upendo wa dhati nawe ni Mwenyezi MUNGU aliyekuumba na kukupa Pumzi na riziki na Wazazi wako tu waliokuzaa na kukulea vema.

Fuatilia visa hivi.
Mimi Nilikuwa na rafiki yangu mkubwa ambaye tulikuwa tunasaidiana ktk shida na raha, Lakini kuna wakati nilikuja kuyumba Sana kimaisha jamaa alikuwa vizuri, Siku moja nikaomba anikopeshe 50,000/= (Elfu hamsini tu),jamaa alikataa kunikopesha kuwa hana Hela wakati huo Mimi najua jamaa ana pesa kwasababu yeye mwenyewe alikuwa anasema kuhusu mipango yake na baada ya hapo akaanza kupunguza mawasiliano na ukaribu.

Rafiki zangu wengine waliacha kabisa kuwasiliana na Mimi, wakati nilipokuwa na hali nzuri kiuchumi walikuwa ni watu safi sana wakionyesha kuwa Wana upendo wa dhati kwangu, Kumbe sivyo.

Kisa kingine ni Cha mdogo wangu,huyu alipatwa na matatizo makubwa hadi kufungwa jera,aisee marafiki zake aliokuwa akijidai nao kuwa oh!, Mimi Nina rafiki wengi tulioshibana, aisee walijiweka mbali sana na shida hiyo hata kwenda gerezani hawakwenda,hata kuulizia tu maendeleo yake hawakuthubutu kabisa.Alipotoka ndio wakawa wanakuja kwa aibu wanasema eti "Tuliogopa kuja gerezani", Wengine wakasema "Tulikuwa na mpango wa kuja baadaye", wakati mtu amekaa jera miezi minne.

Hitimisho
Ndugu yangu/zangu ukiwa vizuri kimaisha,kwa maana ya kazi nzuri, biashara nzuri,cheo kizuri,n.k.Usije ukalewa sifa kutoka kwa rafiki zako hao wanakupendea nafasi uliyonayo na si wewe, ukitaka kuthibitisha hilo hebu pata msukosuko kidogo uone jinsi jamaa zako watakavyotoka nduki.

Hivyo ushauri wangu ukiwa na nafasi nzuri jari kwanza Wazazi wako,Famili Yako,Bila kumsahau Mwenyezi MUNGU;Km unataka kumsaidia mtu msaidie tu km Ibada tu na si kutegemea kurudishiwa fadhila. Kuwa na Marafiki ni kitu kizuri lakini uwe mwangalifu,ishi nao huku ukijua wazi kuwa siku mambo yakikuendea mrama lazima hao marafiki zako wakukimbie au wakusaliti.Tujifunze pia kupitia kwa Yesu namna Wanafunzi wake walivyomkwepa wakati wa Mateso yake.
Hujakosea lakini maandiko yanasema amtegemea mwanadamu atalaaniwa, Mungu ameshaijua mioyo yetu
 
Back
Top Bottom