Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

maisha nikuishi na kujifunza ,tunaishi ili kujifunza ,na Tunajifunza ili tuishi,

maisha haya kumejaa watu wengi masnitch ,kunzia ndgu jamaa hata marafiki ,wote sio wakuwaamini ,

wapo ambao wanapenda wakusikie una shida ili wakusaidie ,hawatapenda kukuona ukipata wanachotaka wao siku zote uwe chini yao ,

.wapo ambao kila siku wao ndo wenye shida na kupenda kusaidiwa wao ,hata kama watapata ,basi hawatoweza kukusaidia ,kama ntapata elfu 50 wote basi itatumika ya kwako yake itabaki ,

kuna mengi nimepitia ,toka kwa ndugu jamaa na marafiki ,yamenifunza nikusimama na Nafsi yangu familia yangu na watoto wangu ,yaan wamenifanya niwe m'binafsi kuangalia maslahi yangu kwanza kabla ya mtu yeyote ,maana hata wao hawajali ya kwako
nyoka mzee
 
Mkuu haijalishi marafiki wangapi watakuangisha,marafiki ni kama vitabu kupata kitabu kizuri ndio kazi lakini kwa vyoyote na kwa chochote huwezi fanikiwa pasipo misaada ya ndugu,jamaa na marafiki.
 
Mkuu kuna wakati hata uwe na kila kitu au uwe na uwezo vipi,lkn utahitaji tu msaada kutoka kwa mtu mwingine.Fikiri mfano upo gerezani utawezaje kutoka bila kumtegemea ndugu yako wa Karibu au mzazi wako au mkeo?.
Yeye anamaanisha hahitaji msaada wa marafiki, ila wa mke na wazazi ni LAZIMA.
 
Ila upande fulani upo sahihi. Sijui ni ushamba wa kujifanya kujua jua watu, au kuzoeana zoeana na watu hivyo au nini??? Yaani tumekutana kwenye kazi, vilabuni n.k, halafu unalalamika hujasaidiwa? Tatizo watu wana ushamba mwingi wa mikoa na shobo nyingi.

Watu wanafanya wrong selection ya company ya kusaidiana nayo kwenye shida na raha, kabla hawajalaumu ni vema wajifunze kuchagua watu husika wa kuahirikiana nao. Wakiweza hivyo, hakutakuwa na malalamiko yao, ushamba ushamba tu!
Sawa Mkuu, Wewe usiye mshamba mshamba.Usilolijua ni usiku wa giza.
 
Mkuu haijalishi marafiki wangapi watakuangisha,marafiki ni kama vitabu kupata kitabu kizuri ndio kazi lakini kwa vyoyote na kwa chochote huwezi fanikiwa pasipo misaada ya ndugu,jamaa na marafiki.
Kweli,Inatupasa kuomba MUNGU ili tuweze kupata marafiki wa kweli wasio vigeu geu.
 
Back
Top Bottom