Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,371
- 14,481
- Thread starter
- #101
Moyo wa mtu kichaka.Kule Musoma kuna jamaa alikuwa Mwalimu akamkopesha jamaa yake ambaye alikuwa ni mwananchi wa eneo lile, pesa hiyo wakadaiana muda mrefu,siku moja mdeni wake akamwambia yule Mwalimu kuwa aende nyumbani kwake ili amlipe deni lake, Mwalimu alienda kufika kule Kumbe Mwamba ameandaa vijana wenye silaha, Aisee walimchakaza yule Mwalimu hadi Umauti.Kisa Tshs.400,000/=, Ambazo ni zake mwenyewe, kwa hiyo akikosa pesa na uhai pia.Nyie Acheni tu, binadamu Wabaya sana.Siku ukitoka kwenu Dar..
Ukaenda kutafuta maisha Kigoma au Ruvuma huko.
Ndo utajua Maisha ni Watu na watu sio ndugu zako na wazazi wako. ( utakavyomuishi mtu, ndivo atakuishi ikiwa umechangamana na watu ambao kiakili mko ktk mstari mmoja)
Watu wengi tunapenda kupendwa na kutendewa mambo makubwa mazuri, ili hali sisi wenyewe hatupendi kuwatendea wengine ivo .
Alafu baadae tunakuja unasikia....Watu wabaya sanaa, wana roho mbayaaa mnoo.
Sikatai kwamba kuna watu hata uwatendee mema gan, wao watatafuta kukutenda ubaya, Hao dawa yao ni kuwafanyia ubaya pia .