Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Rafiki wa kweli ni ndugu zako wa damu, familia na watoto the rest do not care about you aisee.
Siku ukitoka kwenu Dar..

Ukaenda kutafuta maisha Kigoma au Ruvuma huko.

Ndo utajua Maisha ni Watu na watu sio ndugu zako na wazazi wako. ( utakavyomuishi mtu, ndivo atakuishi ikiwa umechangamana na watu ambao kiakili mko ktk mstari mmoja)

Watu wengi tunapenda kupendwa na kutendewa mambo makubwa mazuri, ili hali sisi wenyewe hatupendi kuwatendea wengine ivo .

Alafu baadae tunakuja unasikia....Watu wabaya sanaa, wana roho mbayaaa mnoo.

Sikatai kwamba kuna watu hata uwatendee mema gan, wao watatafuta kukutenda ubaya, Hao dawa yao ni kuwafanyia ubaya pia .
 
si uliitoa kwa roho moja?!mimi hapa nimekopeshwa na wanangu tofauti tofauti kama 6m hivi,nataka kufanya deal ya 50m wiki ijayo. Hivi ikitokea mtu anataka kunikopa itakuwaje? Lakini haimaanishi wale walionikopesha wajinga,Hapana kuna timing ya matumizi ya hela
👍
 
Inategemea mkuu huwa Kuna ndugu vichomi kuliko kichomi chenyewe na hawapendani hata kidogo, na hyo chuki huwa ni asili tu ya baadhi ya Koo familia kwa familia so inakuwa kama ni utamaduni wa kuendekeza kuchukiana.
All in all nyakati hizi upendo na utu umepungua sana kupata mtu mwenye utu wako wachache sana aisee. Mungu atusaidie tulee familia zenye utu na upendo
Ukija huku chuga baadhi ya wanandugu toka nitoke,wamekuwa maadui juu ya vipande vya ardhi tu.
 
Siku ukitoka kwenu Dar..

Ukaenda kutafuta maisha Kigoma au Ruvuma huko.

Ndo utajua Maisha ni Watu na watu sio ndugu zako na wazazi wako. ( utakavyomuishi mtu, ndivo atakuishi ikiwa umechangamana na watu ambao kiakili mko ktk mstari mmoja)

Watu wengi tunapenda kupendwa na kutendewa mambo makubwa mazuri, ili hali sisi wenyewe hatupendi kuwatendea wengine ivo .

Alafu baadae tunakuja unasikia....Watu wabaya sanaa, wana roho mbayaaa mnoo.

Sikatai kwamba kuna watu hata uwatendee mema gan, wao watatafuta kukutenda ubaya, Hao dawa yao ni kuwafanyia ubaya pia .
Nimeshakaa sehemu tofauti tofauti na nyingine far away from ndugu na nilijifunza mengi sana hasa kwa kuishi na watu tofauti hasa kwa kuepuka kuvuka mipaka ila pendo lao bado mkuu kufikia bandugu ingawa lilikuwa la kiasi always napendaga win win situation na sio win loose situation nashikamana na watu wenye interest za kufanana
 
Waheshimiwa Sana Wana JF, Hbr za jioni? Kama kichwa kinavyosema katika mapito niliyopitia nimegundua kuwa hakuna Binadamu "ANAYEKUPENDA KWA DHATI',. Mwenye upendo wa dhati nawe ni Mwenyezi MUNGU aliyekuumba na kukupa Pumzi na riziki na Wazazi wako tu waliokuzaa na kukulea vema.

Fuatilia visa hivi.
Mimi Nilikuwa na rafiki yangu mkubwa ambaye tulikuwa tunasaidiana ktk shida na raha, Lakini kuna wakati nilikuja kuyumba Sana kimaisha jamaa alikuwa vizuri, Siku moja nikaomba anikopeshe 50,000/= (Elfu hamsini tu),jamaa alikataa kunikopesha kuwa hana Hela wakati huo Mimi najua jamaa ana pesa kwasababu yeye mwenyewe alikuwa anasema kuhusu mipango yake na baada ya hapo akaanza kupunguza mawasiliano na ukaribu.

Rafiki zangu wengine waliacha kabisa kuwasiliana na Mimi, wakati nilipokuwa na hali nzuri kiuchumi walikuwa ni watu safi sana wakionyesha kuwa Wana upendo wa dhati kwangu, Kumbe sivyo.

Kisa kingine ni Cha mdogo wangu,huyu alipatwa na matatizo makubwa hadi kufungwa jera,aisee marafiki zake aliokuwa akijidai nao kuwa oh!, Mimi Nina rafiki wengi tulioshibana, aisee walijiweka mbali sana na shida hiyo hata kwenda gerezani hawakwenda,hata kuulizia tu maendeleo yake hawakuthubutu kabisa.Alipotoka ndio wakawa wanakuja kwa aibu wanasema eti "Tuliogopa kuja gerezani", Wengine wakasema "Tulikuwa na mpango wa kuja baadaye", wakati mtu amekaa jera miezi minne.

Hitimisho
Ndugu yangu/zangu ukiwa vizuri kimaisha,kwa maana ya kazi nzuri, biashara nzuri,cheo kizuri,n.k.Usije ukalewa sifa kutoka kwa rafiki zako hao wanakupendea nafasi uliyonayo na si wewe, ukitaka kuthibitisha hilo hebu pata msukosuko kidogo uone jinsi jamaa zako watakavyotoka nduki.

Hivyo ushauri wangu ukiwa na nafasi nzuri jari kwanza Wazazi wako,Famili Yako,Bila kumsahau Mwenyezi MUNGU;Km unataka kumsaidia mtu msaidie tu km Ibada tu na si kutegemea kurudishiwa fadhila. Kuwa na Marafiki ni kitu kizuri lakini uwe mwangalifu,ishi nao huku ukijua wazi kuwa siku mambo yakikuendea mrama lazima hao marafiki zako wakukimbie au wakusaliti.Tujifunze pia kupitia kwa Yesu namna Wanafunzi wake walivyomkwepa wakati wa Mateso yake.
Ndugu, haya mambo uliyoandika hapa jukwaani mbona yanajulikana sana hapa duniani?
Kwani ulikuwa huyajui? Kama ulikuwa huyajui na umeanza kuyajua sasa, basi umeanza kukomaa.
Hakuna jipya chini ya mbingu.
 
Nimeshakaa sehemu tofauti tofauti na nyingine far away from ndugu na nilijifunza mengi sana hasa kwa kuishi na watu tofauti hasa kwa kuepuka kuvuka mipaka ila pendo lao bado mkuu kufikia bandugu ingawa lilikuwa la kiasi always napendaga win win situation na sio win loose situation nashikamana na watu wenye interest za kufanana
Umuhimu wa ndgu unapatikana pale kwenye msiba kuoa au kuuguza, ila ndg wengi hawapendi maendeleo ya ndg wegine, watakupenda sanaa ukiwa masikini wa kipato mwenye kujishusha mbele yao, ila usijifanye mujuaji watt wako kuenda English medium, nk hapo watakupenda kiunafiku tu.
 
si uliitoa kwa roho moja?!mimi hapa nimekopeshwa na wanangu tofauti tofauti kama 6m hivi,nataka kufanya deal ya 50m wiki ijayo. Hivi ikitokea mtu anataka kunikopa itakuwaje? Lakini haimaanishi wale walionikopesha wajinga,Hapana kuna timing ya matumizi ya hela
Sawa,Sasa Kwanini ukate na mawasiliano??.
 
Mifano ipo mingi sana...

Ila huu nimeshuhudia kwa macho.. ..ndugu

Wa kuzaliwa baba na mama mmoja ..wanazungukana na kuharibiana

Maisha si kazini..kwenye ndoa..biadhara mpaka kupelekana jela ...yaani mtu anamtengenezea kesi ndugu yake na kusimamia show ili akaozee jela. ..

Shukuru Mungu kupata ndugu na mkawa ndugu kweli..sio kwa vile ni damu moja tu

.... Naa huyo mtu alitolewa jela kwa msaada wa rafiki zake tu ..walijichanga changa..

Sasa hivi imani inatoweka... .. tunakoelekea ndugu /rafiki atakuwa ni pesa yako na akili yako tu...

Maana hata wazazi na watoto wanasalitiana..
Dah!!!, Inasikitisha Sana.Umenikumbusha Mama mmoja alikuwa Mwalimu akastaafu,Sasa binti yake wa kwanza kuzaliwa ktk tumbo lake alitaka kumuua kwa kumuwekea sumu, MUNGU ni mkuu akamuokoa.
 
Inategemea mkuu huwa Kuna ndugu vichomi kuliko kichomi chenyewe na hawapendani hata kidogo, na hyo chuki huwa ni asili tu ya baadhi ya Koo familia kwa familia so inakuwa kama ni utamaduni wa kuendekeza kuchukiana.
All in all nyakati hizi upendo na utu umepungua sana kupata mtu mwenye utu wako wachache sana aisee. Mungu atusaidie tulee familia zenye utu na upendo
Tuombe MUNGU atusaidie ili tuweze kurejesha upendo ule wa zamani uliopotea.
 
Back
Top Bottom