Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Aisee hii imenigusa sana, nilijua ndugu tu ndo wanatabia hii kumbe hata mama wazazi, tuliache kuwaombea wazazi wetu kama ulivyosema hata kama wana tuchukia wakati mwingine
Mama yangu mzazi alinipenda sana na akawa anaongea na mimi muda mwingi na kuniombea sana. Leo pesa zimeisha hata nikipiga simu wanapewa watoto wa marehemu dada yangu waongee (shikamo mama.... jibu; ongea na wajomba zako mimi sina cha kuongea na wewe). nikienda kijijini hata chakula wakiivisha sipo wanakula sibakishiwi. Namshukuru Mungu wakati nina unafuu wa maisha nilijitahi kuboresha ustawi wa wazazi wangu hata nyumba nzuri nikawajengea. Nimeamua niende mbali na kijiji changu zaidi ya kilometa 800 nije nihangaike tena na sasa natafuta kwa tabu ili nipate tena nirudishe mahusiano mazuri na Mama yangu ambaye kumbe nikiwa na pesa ndo upendo unakuwepo. Tusiache kusaidia na kujitoa kwa ajili ya wazazi wetu.
 
Mimi ni mdogo kwake na nilikua namlipia yeye Ada wote walikua wanajua kama mimi nalipa ada kasoro yeye mwenyewe

Madeni yamenikuza chief nimekua nikiona Mama anakopa analipa maisha yanaenda na hata ada yake ni matokeo ya mchongo ulioanzishwa na pesa ya mkopo na huwa hatukopi fedha ya kutosha kama hatuna uhakika wa kulipa

Nia njema ninayo ndio maana sikuacha kulipa ada yake kuhusu kua na roho ya kichawi Mama ndie aliyesema kumbuka chief mtu hapewi ubaya kwa tukio moja kuna mfululizo wa matukio ya yeye kunifanyia mimi hadi hua nawaza ananichukia kwa nn au ndio mafanikio yangu na umri wangu mdogo kwake ni shida? Kumbuka Hakuna mama anaemchukia mwanae chief hivyo hawezi msingizia

Lakini sijawahi acha kusaidia kwani huez kumfundisha mtu kua mwema Kwa ubaya mi nimekua mwema kwake tokea siku ya kwanza kujua yeye kwangu ni Hater
Hongera mno kaka, hapo nimekuelewa. Umejibu vema mno. You have a good sense of humor, you are unique!
 
Watu wengi unaweza kua huna chuki naye. Ila yeye ndiye anayelazimisha mpaka Uwe na chuki nae.
Mtu umejitulizia zako haishi chokochoko na maneno juu yako. Majitu mengine ni ya ajabu sana humu Duniani.
 
Watu wengi unaweza kua huna chuki naye. Ila yeye ndiye anayelazimisha mpaka Uwe na chuki nae.
Mtu umejitulizia zako haishi chokochoko na maneno juu yako. Majitu mengine ni ya ajabu sana humu Duniani.
Hao nao ni wengi pia kwa,Na ndio raha yao kuchokoza watu na kuwakwaza.
 
Pia na hao ndugu wa damu nadhani bado haujawachunguza vizuri mkuu.

Yawezekana wewe ukawa poa sana kwa ndugu zako, ila wao sidhani kama watakuwa perfect kwa 100% juu yako.
Ndugu kuwa perfect ni ngumu,sema kuna mapungufu fulani unapotezea tu ili maisha yasonge;Hali ikiwa ngumu ndo unapiga chini.
 
Kwa akina mama hiyo huwa inatokea.Mimi mwenyewe mama yupo hivyo, yaani km hujamtumia pesa kwa muda mrefu siku ukimpigia utakuta ni km vile Hana muda na simu Yako,Mtu anakuuliza ulitaka kusemaje sasa?, Swali hili unaulizwa kabla ya kujuliana Hali.
Aisee poleni sana wakuu binafsi mama yangu anatakaga tumpigie simu basi hiyo ndiyo furaha yake mambo ya pesa huwa haombagi kabisa na huwa tunatuma pasipo yeye kuomba.
 
Pia na hao ndugu wa damu nadhani bado haujawachunguza vizuri mkuu.

Yawezekana wewe ukawa poa sana kwa ndugu zako, ila wao sidhani kama watakuwa perfect kwa 100% juu yako.
Yeah I agree with you coz hatuwezi kuwa the same hundred perse but ushirikiano upo na kubebeana madhaifu yetu ya hapa na pale ila hujitoa sana kwangu wallah
 
Naomba unisaidie mfano wa vitu vinavyoweza kumfanya mzazi asimpende tena mwanae.
Kuna kitu nataka kujifunza hapa.
Moyo wa mtu ni kichaka ni ngumu kujua mtu anapenda Nini na anachukia Nini.Kwa ufupi ili upendwe uwe na pesa na uwe mtoaji mzuri lkn ukitaka kuchukiwa uwe huna pesa.
 
Anaejifanya ni rafiki yako wa karibu, huenda ametumwa na maadui zako ili aweze kuchukuwa chochote kinachohitajika na mganga kwako . Wewe utafurahi na kumueleza Siri zako kumbe, ni shetani anaekuja kwa jina la malaika. Yamenikuta!! Jua tu watu ni wengi ila binadamu ni wachache.
 
Anaejifanya ni rafiki yako wa karibu, huenda ametumwa na maadui zako ili aweze kuchukuwa chochote kinachohitajika na mganga kwako . Wewe utafurahi na kumueleza Siri zako kumbe, ni shetani anaekuja kwa jina la malaika. Yamenikuta!! Jua tu watu ni wengi ila binadamu ni wachache.
Uko sahihi kabisa Mkuu, binadamu kumuelewa ni ngumu Sana, Maana umdhaniaye kuwa sivyo Kumbe ndiye.
 
Back
Top Bottom