Wakuu niko Arusha nikiongozana na viongozi wa kitaifa waliokuja hapa kumpokea Kamanda Lema atoke, yapigwe maandamano mpaka NMC, kisha mkutano mkubwa. Aisee hali ni tete. Slaa katinga Mahakamani hapa wakati Mbowe akijiandaa kuzungumza na wana wa Arusha waliokuwa mahakamani. Kashangiliwa rais, rais, rais, rais...Kamanda mbowe ndiye pekee alikuwa anasubiriwa na watu waliokuwa nje ya mahakama atoe command ya nini kifanyike. Si polisi, wala mtu mwingine angeweza kuwasogeza watu wale hatua hata moja kutoka getini.
Rais Dkt. Slaa ameandamana na Kamanda Lissu. Patatosha hapa leo NMC.
Kilichotokea; hakimu aliyetakuwa kusaini COURT ORDER kachomoa. Nafikiri kwa maadili ya kazi zao kasema kuwa atakuwa amechukua uamuzi huo kwa shinikizo (kuwa ameshinikizwa), hivyo kachomoa na Lema hawezi tena kutoka kwa leo, mpaka Jumatatu. Ndo tuko hapa NMC, kusikiliza viongozi wanatumabia nini. Tutapata taarifa kamili ya nini hasa kilichojiri. Niko hapa rasmi kuwapatia upadates.
Samahanini wakuu. Nimesahihisha pale nilipoandika REMOVAL ORDER, ilipaswa kuandikwa COURT ORDER. Nshukuru wote waliojaribu kuhoji usahihi wa thread kwa maneno hayo yaliyoawachanganya. Nimefanyia kazi critiques zenu.