Kutoka Mahakamani: Rufaa ya dhamana ya Mbunge Lema yasikilizwa, yapigwa kalenda

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Baada ya juhudi kubwa za wanasheria wetu, hatimaye mahakama imekubali kusikiliza tena kesi ya Mhe.Lema leo tarehe 8 December 2016. Haya ni maombi mapya ya rufaa ya dhamana chini ya Jaji Dr.Rubby Aweri-Opio. Hongereni wanasheria wote mliofanikisha jambo hili, hongera Jaji Opio kwa kukubali kupanga tarehe ya leo. Tunawaombea haki ikapate kutendeka. Wakazi wa Arusha msiache kujitokeza kwa wingi mahakamani kusikiliza kesi ya mbunge wenu.Kesi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema .
imepangwa kusililizwa leo.

==========

Katibu Mkuu wa CHADEMA taifa Mhe.Vincent Mashinji ameongozana na Katibu wa kanda ya kaskazini na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mhe.Amani Golugwa tayari wamefika mahakamani.
IMG-20161208-WA0005.jpg
IMG-20161208-WA0003.jpg


Tupo mahakamani tunasubiri mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kufikishwa mahakamani
.
Updates. .....
Uamuzi kuhusu dhamana ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema utatolewa tarehe 14.12.2016.

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ataendelea kukaa magereza kisongo hadi Tarehe 14 Desember 2016 ambapo mahakama itatoa maamuzi ya Rufaa iliyosomwa leo mbele ya Jaji Dr Opio.
 
Back
Top Bottom