Haka karafiki kangu kataniletea matatizo soon....!!!!!

Haka karafiki kangu kataniletea matatizo soon....!!!!!

Hapo kuna zaidi ya upendo kwa mtoto, msome vizuri mleta mada. Hapo kuna urafiki aliojijengea kichwani huyu mleta mada kuwa ni urafiki wa kumuondelea stress, Huo ni urafiki gani kwa mtoto wa miaka 4?

Hapo anafikia mpaka kuona huyu mama anamuharibia urafiki wale na mtoto na kusema kuwa "nina hasira sana na huyu mama wa rafiki yangu huyu na leo nikirudi nitakuwa nimeshapata dawa yake"

Mpaka hapo hulioni kuwa ni tatizo kubwa na hii ni "child abuse"?

hayo ya kawaida, mbona wengine wapo jf lengo ni kuondoa au kupunguza stress na huwa wana hasira sana na computers zao zinapokuwa zipo slow. lol.
 
hayo ya kawaida, mbona wengine wapo jf lengo ni kuondoa au kupunguza stress na huwa wana hasira sana na computers zao zinapokuwa zipo slow. lol.

Hicho kibibi kitakuchosha bure
Hebu njoo tuendelee kutoana stress ...lol!!
 
acheni hizo, watoto wanahitaji kupendwa na jamii nzima, kuoneshwa kuwa wanajaliwa. dhamira ya mtu anaijua mwenyewe, si kila aliekaribu na mtoto ana nia mbaya. msisababishe watu wakawatenga watoto wenu kwa hizi kasumba mlizo nazo.

Hata father Kimaro wa Kanisa Katoliki Changanyikeni Dar, alikuwa anajifanya kuwa karibu na watoto, kilitoke nadhani unakumbuka vizuri; alimlawiti mtoto wa watu hadi akafumaniwa. Haikutokea bahati mbaya, alijifanya kipenzi cha watoto, wazazi wakamwamini kwa kuwa ni padri lakini mwisho wa wale watoto ukawa mbaya.

Sitokuwa tayari kuona jitu la watu linajipendekeza kwa watoto wangu ati anapenda watoto. Huo ujinga akajifanyie kwa mahayawani. Hata huyo Eiyer anajua anachokifanya hakikubaliki ndiyo maana anatafuta watoto wa wamama wasioishi na waume zao, mbali na hapo angeshakula kichapo kitambooo! Ingekuwa na yeye ana watoto, then watoto wake wangekuwa marafiki na huyo mtoto wa jirani hiyo caring kwa mtoto wa jirani ingeleta maana kwa sababu angekuwa anamjumuisha na watoto wake katika fun mbalimbali.

cc: Eiyer
 
Khaaaa!!!!!!!!
Hii kwangu haiwezi kutokea,nakuwa makini sana na mienendo yao na umri pia kama kana jinsia tofauti kakianza kukua nabadili mazoea na kuwa makini sana

Ila kwa hili naona mama wa haka karafiki kangu anataka kuutumia urafiki wangu na mwanae kama nafasi ya kufanikisha yake

Hili ni gumu sana kufanikiwa!!
Ngoja waku babu seya ndio utajua
 
Maandiko yako ya post #1 yanadhihirisha na yanathibitisha niliyoyaandika.

Hayathibitishi chochote zaidi ya wewe kuandika kile unachokiona kwenye fikra zako

Kama kuna chochote ambacho ni valid si ukiseme hapa?
 
Tafadhali nipatie namba ya simu ya huyo mama nikutane nae nimpe darsa la watu kama wewe.

Nakushauri uonane na wataalam wa saikolojia, unahitaji msaada wa haraka sana. Kabla hujapoteza maisha ya watoto na yako mwenyewe.

Woman, are you high on something?
 
hahahaah! anitumie nauli fasta nikawe mamdogo fake. hiyo kazi naiweza sana na huyo mama mtoto ataisoma namba.

Tena wakati unakaaga "Karafiki" jifanye unakachum mbele ya maza'ake.
Kuonesha ni Jinsi Gani Bwana na Bibi Eiyer mnavyokapenda Karafiki kenu.
Mkimaliza siyo mbaya mkaenda kupongezana na "Kamoja" ka fasta nyumbani kwa Eiyer.

Ngoja nitaku DIPU soon!!

Matter resolved.... :coffee:
 
watu kama nyie hata mkiona mtoto wa mwenzio anakosea huwezi kumrekebisha, wewe ni mtu hatari sana katika maisha ya uswahilini ambapo mtoto anakumbukwa kwao kama hayupo wakati wa kulala.

Nadhani hatujaelewana, kinachotokea hapa ni mtu kujaribu kutrick wake za watu kwa kujifanya kuwa kipenzi cha watoto wao. Katika mahusiano kama hayo mambo mawili hutokea; aidha mtu kujenga mahisiano ya kimapenzi na mama mtoto au kumfanyia mtoto mwenyewe ukatili wa kijinsia hasa sexual harassment. Haya mambo yapo na yameshatokea mara nyingi. Lazima mzazi uwe makini na watu wa namna hii na ikibidi hakuna haja ya kuendekeza watu wa namna hii.
 
Khaaaa!!!!!!!!
Hii kwangu haiwezi kutokea,nakuwa makini sana na mienendo yao na umri pia kama kana jinsia tofauti kakianza kukua nabadili mazoea na kuwa makini sana

Ila kwa hili naona mama wa haka karafiki kangu anataka kuutumia urafiki wangu na mwanae kama nafasi ya kufanikisha yake

Hili ni gumu sana kufanikiwa!!

kumbuka pia wanaume wachache sana waliweza kujinasua ktk mitego ya wanawake waliokuwa wakiwahitaji, kama kweli huna mpango naye, vunja hiyo link iliyopo (mtoto) ndo utaeleweka hutaki mazoea, vinginevyo unavyoongea then anarudia na unakubali anakuona kama sitaki nataka, mwisho atakunasa nawe hata kama si mpango wako
 
Back
Top Bottom