mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 7,281
- 20,990
Taasisi ya ndoa na mahusiano kwa ujumla ni taasis yenye changamoto nyingi san . wewe Ikiwa uko kwenye ndoa na mambo yanaenda vizuri , basi hiyo ni baraka kubwa sana na umshukuru sana baba muumba aliye juu Mbinguni.
Kisa hiki nachokupa kimetokea huko Kenya kwa majirani kwenye Kaunti ya kiambu.
Kisa hiki kinamwendea daktari bingwa wa upasuaji kutoka Kaunti ya Kiambu. Nadhani anaitwa Dkt. Dennis Nyambane.
Kwa nje kwa huyu daktari kila kitu kilionekana kuwa sawa. Alikuwa na kazi nzuri na alionekana kuwa anafanya vizuri katika maisha yake. Alikuwa na mke na mtoto mmoja wa kiume. Kwa mtu wa umri wake, angehitaji nini kingine?
Anyway lakini siku chache zilizopita, mke wake alifariki baada ya kupata jeraha la kuchomwa na kisu. Inaonekana kulikuwa na ugomvi na msukosuko kati yao yaani mume na mke.
Sasa mke amelala kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, huku mume akiwa kituo cha polisi kupisha uchunguzi
Mtoto wao wa miaka mitatu haelewi kinachoendelea. Hawezi kumuona mama yake, na pia hawezi kumuona baba yake.
Lakini jambo lililoshtua kuhusiana na tukio hili zaidi ni madai yanayotolewa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa daktari huyo. Wanadai kwamba kwa muda mrefu alikuwa akiteswa na kunyanyaswa na mwenza wake.
Kuna picha yake akiwa na jeraha kubwa usoni. Watu wanaodai kumfahamu wanasema aliwahi kupigwa na mke wake kwa nyundo. Wakati fulani mwezi Mei, inasemekana alilazimika kukimbilia kituo cha polisi na kutoa taarifa kuhusu yaliyokuwa yakitokea nyumbani.
Rafiki mwingine wa daktari huyo akachapisha ujumbe wao wa mawasiliano mtandaoni kuhusiana kilichokuwa kinaendelea. Katika ujumbe huo, rafiki yake anamsihi aondoke tu nyumbani pamoja na mtoto wake, akapangishe nyumba nyingine na kumzuia mke wake mwenye tabia ya vurugu na Fujo kumfikia.
Lakini daktari huyo alikuwa akisita kuondoka.
Sababu?
Alisema hakuwa na pesa. Inadaiwa kuwa mke wake alikuwa na namba yake ya siri ya benki (PIN) na alikuwa amechukua pesa zake zote.
Katika moja ya ujumbe, daktari huyo alimjibu rafiki yake:
“Nitarudi huko kwa sababu sina mahali pengine pa kwenda. Sidhani kama nitaishi.”
Daktari huyo pia alimtumia rafiki yake picha iliyokuwa imewekwa kuonekana mara moja tu (view once), na picha hiyo inadaiwa ilimshtua sana rafiki yake. Huenda ilikuwa moja ya picha zinazoonyesha majeraha aliyokuwa ameyapata.
Kisha akaandika:
“nilikabwa shingoni hadi nikakaribia kufa.”
Anyway
Kuhusu ukweli wa madai haya yote, ni wale waliokuwa ndani ya chumba hicho pekee wanaoweza kujua kilichotokea. Kwa sababu sasa mke huyo yuko kimya na amelala kwenye chumba cha kuhifadhia maiti — kimya cha m
ilele.