Kwanza ninakawaida ya kuwapenda watoto sana bila kujali kama ni wa jinsia gani,kwangu nawakubali wote sana na wamekuwa marafiki wangu wa ukweli sana kwakuwa hawajui kupenda kwa masharti na wakikupenda wanakupenda ki-ukweli hasa
Sasa uswahilini kwetu kuna katoto kamoja ka miaka mi-4 hivi,jinsia yake ni ya kike huwa napenda sana siku nikiwa nyumbani au nikiwahi kurudi huwa nakaa nako na kupiga story nako sana na hunifanya mastress yangu ya kutafuta hela kuisha kama sio kupungua
Katoto haka kananipenda sana nami nakapenda sana kwani ni karafiki kangu sana,tatizo linakuja kwa mama yake,anadai kuwa inafika wakati wa usiku kanalia kaletwe kwangu nae anadai anakuwa hataki
Lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba huyo mama yake anadai eti napendeza sana kuwa baba yake huyo mtoto na anadai kwakuwa mtoto wake ananipenda nae ananipenda na ameanzisha visa wakati mwingine hukaleta hako ka rafiki kangu usiku wa saa 4 hadi 5 usiku akidai eti kanalia akalete nami huwa nakapokea na kukaa nako hadi kanapolala kisha nampa mama yake na kisha kuondoka
Mama wa haka karafiki kangu alikuwa ameolewa lakini ameachika kwa mumewe kwa sababu yule jamaa hakuwa ametulia
Sasa hizi vurugu zimekuwa zinazidi sana hadi naanza kukereka kwasababu sina mpango kabisa na huyo dada kwani ana mahusiano na jamaa mmoja hapa mtaani na nafahamiana nae sana
Naanza kuwaza kukakatia line kale ka rafiki kangu lakini roho inaniuma sana
Nimejaribu kumwambia aache tabia hiyo lakini naona kama nampigia mbuzi gitaa
Sijaamua kuchukua maamuzi yoyote hadi sasa lakini naona kama huyu dada ananiharibia urafiki wangu na huyu mtoto na hili sio halali na halikubaliki kabisaaa
Yaani hapa nina hasira sana na huyu mama wa rafiki yangu huyu na leo nikirudi nitakuwa nimeshapata dawa yake
Enyi akina dada hebu mtuache na hawa marafiki zetu na msituvurugie urafiki wetu bana!
Kwana mtoto wako hawezi kumpenda mtu mwingine? Je unauelewa upendo ulliozungumziwa hapo?
Dah! Nakumbuka hata nami nilibatizwa jina nkaitwa baba flani{Jina la Mtoto} mara baada ya kuwa karibu na mtoto huyo ndipo na mama yake naye akataka kuwa karibu zaidi. Ila nashukuru Mungu kuwa haikuwa kama alivyotaka. Baada ya kushindikana basi pakawa na uadui baina yangu mimi na yule mama wa mtoto
Hakuna mtu asiyependa watoto lakini kuna mipaka ya urafiki wa mtoto na mtu mzima, kumbuka hilo.
Watoto zangu mimi niliwatenga sana na watu wanaojidai kupenda sana watoto, na hiyo ni kwa mafundisho kabisa ya namna ya kulea watoto vyema. Sioni hoja wala haja ya jirani kujifanya anampenda sana mwanangu kuliko mimi niliyemzaa.
Fanya hivi:
Siku moja mkaribishe mpenzi wako nyumbani kwako na hakikisha hako Karafiki kako kanakuwepo,
Mtambulishe mpenzi wako kwa karafiki kako kama Mama yake Mdogo, tena ikiwezekana akapatie zawadi.
Baadaye Kasindikize Karafiki kako kwenda nyumbani ukiwa na huyo Mpenzi wako, tena ikiwezekana akabebe yeye.
Mkifika Mpenzi wako amkabidhi mtoto kwa Mama yake kisha amuage bye Mama Mdogo, katoto lazima katarespond the same.
Mama mtu ataipata meseji, asipojirekebisha basi Mchawi.
Sina mtoto
Lakini hiyo hainizuii kuwa na urafiki na watoto bana
Hakuna ukaribu usiokuwa wa lazima na watoto
Watoto ni rafiki zangu!
Nakuja!Inawezekana
Prove it!
hapo blue nakubaliana na wewe asilimia zote na ndio maana nimemshauri eiyer apunguze ukaribu na watoto na si kuacha kuwapenda. kwa namna unavyochangia ni kama vile mtoa mada anafanya makosa kuwapenda watoto. hapo red unaweza kumtofautisha vipi huyo anaejidai/jifanya kuwapenda watoto wako na huyo anaewapenda kweli?
Unatia huruma sanaHapo kuna zaidi ya upendo kwa mtoto, msome vizuri mleta mada. Hapo kuna urafiki aliojijengea kichwani huyu mleta mada kuwa ni urafiki wa kumuondelea stress, Huo ni urafiki gani kwa mtoto wa miaka 4?
Kuna tatizo au wewe ndio unaliona tatizo?Hapo anafikia mpaka kuona huyu mama anamuharibia urafiki wale na mtoto na kusema kuwa "nina hasira sana na huyu mama wa rafiki yangu huyu na leo nikirudi nitakuwa nimeshapata dawa yake"
Mpaka hapo hulioni kuwa ni tatizo kubwa na hii ni "child abuse"?
Hapo kuna zaidi ya upendo kwa mtoto, msome vizuri mleta mada. Hapo kuna urafiki aliojijengea kichwani huyu mleta mada kuwa ni urafiki wa kumuondelea stress, Huo ni urafiki gani kwa mtoto wa miaka 4?
Hapo anafikia mpaka kuona huyu mama anamuharibia urafiki wale na mtoto na kusema kuwa "nina hasira sana na huyu mama wa rafiki yangu huyu na leo nikirudi nitakuwa nimeshapata dawa yake"
Mpaka hapo hulioni kuwa ni tatizo kubwa na hii ni "child abuse"?
Una matatizo makubwa sana, wewe ni wa kufungiwa mbali sana na watoto.
Sina uhakika kama mtoa mada ana urafiki mbaya na huyo mtoto as you think. Kama swala ni kutoa stress sioni kama ni tatizo. Kuna time unaweza kukaa na moto mkapiga vihadithi kadha wakadha. ambazo kwa namna moja ama nyingine zikawa zinakufurahisha. Sidhani kama upo sahihi kusema kuwa hiyo ni Child Abuse
Mkuu nadhani sasa naanza kupata wazo
Nitatafuta mpenzi fake ili huyo mama wa karafiki kangu aipate fresh!
Tafadhali soma link niliyoiweka hapo juu, inaelezea vizuri sana, na ni matumaini yangu itajibu swali lako.