Haka karafiki kangu kataniletea matatizo soon....!!!!!

Haka karafiki kangu kataniletea matatizo soon....!!!!!

Absolutely right Faizafoxy! Watu wa aina ya huyu jamaa wanatumia vijizawadi kutrick watoto wadogo na hatimaye kuwaabuse au kutrick mama zao kupitia watoto wao. Kwa ujumla sitaki kuona watu wa namna karibu na watoto wangu hata kidogo. Mtu mzima kuendekeza ujinga na watoto wa watu tena wa kike. Why?

acheni hizo, watoto wanahitaji kupendwa na jamii nzima, kuoneshwa kuwa wanajaliwa. dhamira ya mtu anaijua mwenyewe, si kila aliekaribu na mtoto ana nia mbaya. msisababishe watu wakawatenga watoto wenu kwa hizi kasumba mlizo nazo.
 
faiza hujamuelewa story yake unaanza kumshambulia na pre judgements zako hapa...soma story yake umuelewe then ndo utoe comments

Nadhani nyinyi ndio hamjanielewa. Nimemsoma vizuri sana na nna uhakika ana matatizo, amma anajijua yeye mwenyewe amma hajijui, lakini ana matatizo makubwa sana.

Mtu anaefanya urafiki na watoto wadogo ni hatari sana. Chunga.

Msome hapa:

Kwanza ninakawaida ya kuwapenda watoto sana bila kujali kama ni wa jinsia gani,kwangu nawakubali wote sana na wamekuwa marafiki wangu wa ukweli sana kwakuwa hawajui kupenda kwa masharti na wakikupenda wanakupenda ki-ukweli hasa

Sasa uswahilini kwetu kuna katoto kamoja ka miaka mi-4 hivi,jinsia yake ni ya kike huwa napenda sana siku nikiwa nyumbani au nikiwahi kurudi huwa nakaa nako na kupiga story nako sana na hunifanya mastress yangu ya kutafuta hela kuisha kama sio kupungua

Katoto haka kananipenda sana nami nakapenda sana kwani ni karafiki kangu sana,tatizo linakuja kwa mama yake,anadai kuwa inafika wakati wa usiku kanalia kaletwe kwangu nae anadai anakuwa hataki

Lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba huyo mama yake anadai eti napendeza sana kuwa baba yake huyo mtoto na anadai kwakuwa mtoto wake ananipenda nae ananipenda na ameanzisha visa wakati mwingine hukaleta hako ka rafiki kangu usiku wa saa 4 hadi 5 usiku akidai eti kanalia akalete nami huwa nakapokea na kukaa nako hadi kanapolala kisha nampa mama yake na kisha kuondoka

Mama wa haka karafiki kangu alikuwa ameolewa lakini ameachika kwa mumewe kwa sababu yule jamaa hakuwa ametulia

Sasa hizi vurugu zimekuwa zinazidi sana hadi naanza kukereka kwasababu sina mpango kabisa na huyo dada kwani ana mahusiano na jamaa mmoja hapa mtaani na nafahamiana nae sana

Naanza kuwaza kukakatia line kale ka rafiki kangu lakini roho inaniuma sana


Nimejaribu kumwambia aache tabia hiyo lakini naona kama nampigia mbuzi gitaa

Sijaamua kuchukua maamuzi yoyote hadi sasa lakini naona kama huyu dada ananiharibia urafiki wangu na huyu mtoto na hili sio halali na halikubaliki kabisaaa

Yaani hapa nina hasira sana na huyu mama wa rafiki yangu huyu na leo nikirudi nitakuwa nimeshapata dawa yake


Enyi akina dada hebu mtuache na hawa marafiki zetu na msituvurugie urafiki wetu bana!


Nakwambieni huyu mtu ni hatari kupita kiasi.
 
Ina maana bado hujagundua kuwa kutuambia tuna fall in love kwa vitu vidogo ni kutudhalilisha?
Hebu tutake radhi kabla sijanuna

Tatizo unapenda sana kutakwa radhi
Sasa hebu sema kudhalilishwa kunakujaje mtu anaposema mna fall kwa vitu vidogo?
 
Hiyo tabia yako ya kutembea na jojo na pipi filimbi mfukoni kwa ajili ya kutrick wake za watu kupitia watoto wao inatakutokea puani. Ati anakupenda!! Mtoto mdogo anakupendaje hivihivi kama siyo wewe kuintertain vijizawadi vidogo au kwenda nako maduka ya karibu na kumnunulia vijiazam?!. Ki ukweli ni tabia mbaya sana kuwa karibu na watoto wa watu, kama unapenda watoto kwanini usimzae wakwako? Una bahati huyo mama yake anaishi bila mume vinginevyo ungeshakatwa mapanga. Grow up man, acha utoto na watoto wa majirani!
watu kama nyie hata mkiona mtoto wa mwenzio anakosea huwezi kumrekebisha, wewe ni mtu hatari sana katika maisha ya uswahilini ambapo mtoto anakumbukwa kwao kama hayupo wakati wa kulala.
 
FaizaFoxy ulikuwa unatafuta mtu mwenye matatizo yale uliyoya copy na ku paste huyu hapa
Msaidie tafadhali!

Kijana una matatizo makubwa sana. Nenda kwa wataalam wakusaidie. Usijikwepeshe. Andiko lako linaonesha una kila dalili ya kuwa una matatizo ya kisaikolojia.

"hunifanya mastress yangu ya kutafuta hela kuisha kama sio kupungua" khaa! huna hata haya?
 
kuwapenda watoto au hata wakubwa hakulazimishi kuwe na ukaribu pia. punguza ukaribu usio wa lazma kwa hako katoto vile ushaona mazingira hayaruhusu. hivi wewe hauna mtoto eeh?

Sina mtoto
Lakini hiyo hainizuii kuwa na urafiki na watoto bana

Hakuna ukaribu usiokuwa wa lazima na watoto
Watoto ni rafiki zangu!
 
Hapo ndiyo umuhimu wa baba unaonekana huyo mtoto amekufanay kuwa kama baba yake baada ya kuona baba yake mzazi hamjali na ww umekuwa faraja ya mtoto sasa tatzo liko kwa mama anataka apate pa kupulia baada ya kuachana na mumewe na kwakuwa hauna mzuka naye kabisa mwambie ukweli tu kwamba hauko tayari kuwa naye ww rafiki yako ni mtot basii na usimruhusu kuingia kwako eti kwa kisingizio cha kumleta mtoto maana ipo siku atakuvulia nguo na uzalendo ukakushinda maana muda mwingine hawa viumbe wakiamua kufanya yao huwa hawashindwi kwa kuwa wanaua udhaifu wa mwanaume uko wapi,endelea tu urafik na mtot ila kuwa makini tu!

Mkuu nimeshamuambia lakini hasikii

Sijui nimfanye nini huyu!!
 
Tatizo unapenda sana kutakwa radhi
Sasa hebu sema kudhalilishwa kunakujaje mtu anaposema mna fall kwa vitu vidogo?[/QUOTE]

Kuombwa radhi kuna raha yake ujue!
Hapo kwa bold Anatusingizia,nami sipendi kusingiziwa sasa!
 
Sina mtoto
Lakini hiyo hainizuii kuwa na urafiki na watoto bana

Hakuna ukaribu usiokuwa wa lazima na watoto
Watoto ni rafiki zangu!
sasa baba paroko we endelea kuwa karibu na hako katoto yakishakufika uje kanisani ulie mazabauni. lol
 
Dah! Nakumbuka hata nami nilibatizwa jina nkaitwa baba flani{Jina la Mtoto} mara baada ya kuwa karibu na mtoto huyo ndipo na mama yake naye akataka kuwa karibu zaidi. Ila nashukuru Mungu kuwa haikuwa kama alivyotaka. Baada ya kushindikana basi pakawa na uadui baina yangu mimi na yule mama wa mtoto
 
acheni hizo, watoto wanahitaji kupendwa na jamii nzima, kuoneshwa kuwa wanajaliwa. dhamira ya mtu anaijua mwenyewe, si kila aliekaribu na mtoto ana nia mbaya. msisababishe watu wakawatenga watoto wenu kwa hizi kasumba mlizo nazo.

Unajua hii kitu iko hivi

Kwa mujibu wa kanuni za maumbile ni kwamba zile tabia ambazo mtu anakuwa nazo mara nyingi huziona kwa mwingine huku akidhani hazimhusu kabisa

Hiki ndicho kinachowatokea hao
Achana nao!
 
acheni hizo, watoto wanahitaji kupendwa na jamii nzima, kuoneshwa kuwa wanajaliwa. dhamira ya mtu anaijua mwenyewe, si kila aliekaribu na mtoto ana nia mbaya. msisababishe watu wakawatenga watoto wenu kwa hizi kasumba mlizo nazo.

Hakuna mtu asiyependa watoto lakini kuna mipaka ya urafiki wa mtoto na mtu mzima, kumbuka hilo.

Watoto zangu mimi niliwatenga sana na watu wanaojidai kupenda sana watoto, na hiyo ni kwa mafundisho kabisa ya namna ya kulea watoto vyema. Sioni hoja wala haja ya jirani kujifanya anampenda sana mwanangu kuliko mimi niliyemzaa.
 
Kijana una matatizo makubwa sana. Nenda kwa wataalam wakusaidie. Usijikwepeshe. Andiko lako linaonesha una kila dalili ya kuwa una matatizo ya kisaikolojia.

"hunifanya mastress yangu ya kutafuta hela kuisha kama sio kupungua" khaa! huna hata haya?

Hebu eleza tatizo la hiyo kauli kwanza kabla ya kuanza kukagua ambae hana haya kati yangu na wewe ni nani!
 
Hakuna mtu asiyependa watoto lakini kuna mipaka ya urafiki wa mtoto na mtu mzima, kumbuka hilo.

Watoto zangu mimi niliwatenga sana na watu wanaojidai kupenda sana watoto, na hiyo ni kwa mafundisho kabisa ya namna ya kulea watoto vyema. Sioni hoja wala haja ya jirani kujifanya anampenda sana mwanangu kuliko mimi niliyemzaa.

Kwana mtoto wako hawezi kumpenda mtu mwingine? Je unauelewa upendo ulliozungumziwa hapo?
 
Hakuna mtu asiyependa watoto lakini kuna mipaka ya urafiki wa mtoto na mtu mzima, kumbuka hilo.
Well,
Hebu tuambie ni mipaka gani hiyo ambayo haitakiwi kuvukwa na uueleze umma wa JF vile nilivyovuka hiyo mipaka
Watoto zangu mimi niliwatenga sana na watu wanaojidai kupenda sana watoto,
Mtu anajidai vipi?
Kujidai ni kufanya nini?
Ni kipimo gani unatumia hadi kujua mtu anajidai?
na hiyo ni kwa mafundisho kabisa ya namna ya kulea watoto vyema.
Mafundisho gani?
Yapi?
Ya wapi?
Sioni hoja wala haja ya jirani kujifanya anampenda sana mwanangu kuliko mimi niliyemzaa.
Bado hujasema kujifanya ni nini lakini bado unaendelea tu kulirudia hilo neno
Kuzaa sio kipimo sha mzazi kumpenda mwanae,wangapi wanadhuru watoto wao wa kuzaa?

Ni kitu gani kinakukereketa mtoto wako kuwa na mahusiano mema na jirani zake?
Au hujiamini?
 
Back
Top Bottom