Haka karafiki kangu kataniletea matatizo soon....!!!!!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,261
2,000
Kwanza ninakawaida ya kuwapenda watoto sana bila kujali kama ni wa jinsia gani,kwangu nawakubali wote sana na wamekuwa marafiki wangu wa ukweli sana kwakuwa hawajui kupenda kwa masharti na wakikupenda wanakupenda ki-ukweli hasa

Sasa uswahilini kwetu kuna katoto kamoja ka miaka mi-4 hivi,jinsia yake ni ya kike huwa napenda sana siku nikiwa nyumbani au nikiwahi kurudi huwa nakaa nako na kupiga story nako sana na hunifanya mastress yangu ya kutafuta hela kuisha kama sio kupungua

Katoto haka kananipenda sana nami nakapenda sana kwani ni karafiki kangu sana,tatizo linakuja kwa mama yake,anadai kuwa inafika wakati wa usiku kanalia kaletwe kwangu nae anadai anakuwa hataki

Lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba huyo mama yake anadai eti napendeza sana kuwa baba yake huyo mtoto na anadai kwakuwa mtoto wake ananipenda nae ananipenda na ameanzisha visa wakati mwingine hukaleta hako ka rafiki kangu usiku wa saa 4 hadi 5 usiku akidai eti kanalia akalete nami huwa nakapokea na kukaa nako hadi kanapolala kisha nampa mama yake na kisha kuondoka

Mama wa haka karafiki kangu alikuwa ameolewa lakini ameachika kwa mumewe kwa sababu yule jamaa hakuwa ametulia

Sasa hizi vurugu zimekuwa zinazidi sana hadi naanza kukereka kwasababu sina mpango kabisa na huyo dada kwani ana mahusiano na jamaa mmoja hapa mtaani na nafahamiana nae sana

Naanza kuwaza kukakatia line kale ka rafiki kangu lakini roho inaniuma sana

Nimejaribu kumwambia aache tabia hiyo lakini naona kama nampigia mbuzi gitaa

Sijaamua kuchukua maamuzi yoyote hadi sasa lakini naona kama huyu dada ananiharibia urafiki wangu na huyu mtoto na hili sio halali na halikubaliki kabisaaa

Yaani hapa nina hasira sana na huyu mama wa rafiki yangu huyu na leo nikirudi nitakuwa nimeshapata dawa yake

Enyi akina dada hebu mtuache na hawa marafiki zetu na msituvurugie urafiki wetu bana!
 
HOPECOMFORT

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
3,260
2,000
Nawewe pia upo single?? Kama upo single basi anaona labda trick yako ya kucheza na mtoto ni namna ya kumpata yeye ndo mana ana kurahisishia kukuletea mtoto ucheze nae hata usiku.

Ebu msome kwanza kama vipi kuna siku ataamua kufunguka kama ataona ausomeki then mchane uepuke usumbufu.
 
miss strong

JF-Expert Member
Jul 4, 2012
7,014
2,000
Cheka na mbwa uingie nae msikitini......kata line kiaina hakawii kuletea kesi yakubaka au hata kumfungia katoto kake!!!!Mazoea kias tu yakizid sana ni hatar.
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,261
2,000
Nawewe pia upo single?? Kama upo single basi anaona labda trick yako ya kucheza na mtoto ni namna ya kumpata yeye ndo mana ana kurahisishia kukuletea mtoto ucheze nae hata usiku.

Ebu msome kwanza kama vipi kuna siku ataamua kufunguka kama ataona ausomeki then mchane uepuke usumbufu.

Hebu soma mada tena
Inaonekana hujaielewa!!
 
Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
29,563
2,000
Kwanza ninakawaida ya
kuwapenda watoto sana bila kujali kama ni wa jinsia gani,kwangu
nawakubali wote sana na wamekuwa marafiki wangu wa ukweli sana kwakuwa
hawajui kupenda kwa masharti na wakikupenda wanakupenda ki-ukweli hasa

Sasa uswahilini kwetu kuna katoto kamoja ka miaka mi-4 hivi,jinsia yake
ni ya kike huwa napenda sana siku nikiwa nyumbani au nikiwahi kurudi
huwa nakaa nako na kupiga story nako sana na hunifanya mastress yangu ya
kutafuta hela kuisha kama sio kupungua

Katoto haka kananipenda sana nami nakapenda sana kwani ni karafiki kangu
sana,tatizo linakuja kwa mama yake,anadai kuwa inafika wakati wa usiku
kanalia kaletwe kwangu nae anadai anakuwa hataki

Lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba huyo mama yake anadai eti napendeza
sana kuwa baba yake huyo mtoto na anadai kwakuwa mtoto wake ananipenda
nae ananipenda na ameanzisha visa wakati mwingine hukaleta hako ka
rafiki kangu usiku wa saa 4 hadi 5 usiku akidai eti kanalia akalete nami
huwa nakapokea na kukaa nako hadi kanapolala kisha nampa mama yake na
kisha kuondoka

Mama wa haka karafiki kangu alikuwa ameolewa lakini ameachika kwa mumewe
kwa sababu yule jamaa hakuwa ametulia

Sasa hizi vurugu zimekuwa zinazidi sana hadi naanza kukereka kwasababu
sina mpango kabisa na huyo dada kwani ana mahusiano na jamaa mmoja hapa
mtaani na nafahamiana nae sana

Naanza kuwaza kukakatia line kale ka rafiki kangu lakini roho inaniuma
sana

Nimejaribu kumwambia aache tabia hiyo lakini naona kama nampigia mbuzi
gitaa

Sijaamua kuchukua maamuzi yoyote hadi sasa lakini naona kama huyu dada
ananiharibia urafiki wangu na huyu mtoto na hili sio halali na
halikubaliki kabisaaa

Yaani hapa nina hasira sana na huyu mama wa rafiki yangu huyu na leo
nikirudi nitakuwa nimeshapata dawa yake

Enyi akina dada hebu mtuache na hawa marafiki zetu na msituvurugie
urafiki wetu bana!

Ninapata mashaka unapo tueleza kwamba huyo dada aliachana na mumewe kwakua jamaa alikua hajatulia
 
Pukudu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
3,133
2,000
Khaaa! Hii mambo acha mi kipindi nakaa Uswaz nilizoeana na vitoto vya Kitaa balaa, kila mmoja nikipita utasikia ticha! Ticha Sasa siku moja katoto ka kike kalikuwa STD 6. Usiku Kama wa saa 4 Baba yake alitaka kukaadhibu, katoto si kakambia kwao kakaja kwangu kanalia kanasema baba yake atampiga amuue..... Basi mi nikaona isiwe kesi nkakarudisha kwao, kufika kwao wacha Baba yake anichenjie eti! Kwa nini kamekimbilia kwangu Mimi ndo nakafanya tabia mbaya! YAANI Kama sio Bibi wa Yule mtoto, yangekuwa mengine....
 
Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,707
1,225
Hahahahaaaa!
Hata mimi napendaga sana vitoto na vinanikubaligi sana. So, naomba nö ya mama katoto!
 
miss strong

JF-Expert Member
Jul 4, 2012
7,014
2,000
Khaaa! Hii mambo acha mi kipindi nakaa Uswaz nilizoeana na vitoto vya Kitaa balaa, kila mmoja nikipita utasikia ticha! Ticha Sasa siku moja katoto ka kike kalikuwa STD 6. Usiku Kama wa saa 4 Baba yake alitaka kukaadhibu, katoto si kakambia kwao kakaja kwangu kanalia kanasema baba yake atampiga amuue..... Basi mi nikaona isiwe kesi nkakarudisha kwao, kufika kwao wacha Baba yake anichenjie eti! Kwa nini kamekimbilia kwangu Mimi ndo nakafanya tabia mbaya! YAANI Kama sio Bibi wa Yule mtoto, yangekuwa mengine....

Yaan ni noumar..........kaa mbali kabisa na vitoto vya kike haswa uswahilin wengine mitego ya pesa!!!
 
HOPECOMFORT

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
3,260
2,000
Hebu soma mada tena
Inaonekana hujaielewa!!

That mama mtoto ana mtu mtaani kwenu nawewe una unamfahamu,Mtoto wake wa miaka mi nne ni rafiki yako sana, then anadai unapendeza sana kua baba wa mtoto. Ndomana nikakushauri kama nilivyo kushauri.
 
Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,261
2,000
Khaaa! Hii mambo acha mi kipindi nakaa Uswaz nilizoeana na vitoto vya Kitaa balaa, kila mmoja nikipita utasikia ticha! Ticha Sasa siku moja katoto ka kike kalikuwa STD 6. Usiku Kama wa saa 4 Baba yake alitaka kukaadhibu, katoto si kakambia kwao kakaja kwangu kanalia kanasema baba yake atampiga amuue..... Basi mi nikaona isiwe kesi nkakarudisha kwao, kufika kwao wacha Baba yake anichenjie eti! Kwa nini kamekimbilia kwangu Mimi ndo nakafanya tabia mbaya! YAANI Kama sio Bibi wa Yule mtoto, yangekuwa mengine....

Khaaaa!!!!!!!!
Hii kwangu haiwezi kutokea,nakuwa makini sana na mienendo yao na umri pia kama kana jinsia tofauti kakianza kukua nabadili mazoea na kuwa makini sana

Ila kwa hili naona mama wa haka karafiki kangu anataka kuutumia urafiki wangu na mwanae kama nafasi ya kufanikisha yake

Hili ni gumu sana kufanikiwa!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom