HAIKUBALIKI: Mitandao ya simu kutumia simu zetu kama bango lao la matangazo ya biashara, WAKOME!!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,664
18,039
Hii haikubaliki hata kidogo na nawaomba wamiliki wenzangu wa siomu za mkononi tukatae kwa nguvu zote makampuni ya simu kutumia simu zetu kama bango lao la biashara!

Wanatujazia mameseji kibao wakitangaza biashara zao. Simu ninunue mimi halafu wewe uitumie kwa matangazo yako ya biashara bure bila kunichangia chochote. Halafu matangazo mengine ya wizi kabisa!!

Niliwahi kupata message toka Vodacom ikisema ""umefanikiwa kujiunga na..." wakati siyo kabisa. Au "namba yako imechaguliwa kwenye draw ya kushindania".

Uhalali ni kuwa kila message ya kutangaza bidhaa zao wailipie shilingi kadhaa na waniingizie kwenye akaunti yangu ya M-pesa, tigo pesa nk. Utakuta simu imejaa mameseji hadi kero!! Hii haikubaliki!!
 
Tena bando wanapandisha bila huruma huku wanatutugemea kuwafanyia promosheni bure.
 
Ukinunua laini ya simu ukaiweka hewani na ukaanza kuitumia, tayari unakuwa UMEKUBALI kitu kinaitwa VIGEZO na MASHARTI
 
TCRA inabidi watueleze uhalali wa makampuni ya simu kutumia simu zetu kama bango la matangazo yao bure!!

TCRA ni jipu!! inabidi likamuliwe tu bila ganzi! TCRA watajiteteaje kama wakituhumiwa kuwekwa mfukoni na makampuni nya simu kwa kitu kidogo?
 
Vodacom wameandika ujumbe leo kuwa kama hutaki sms zao andika neno Ondoa

Ukiwa mmoja wa wateja wetu wa thamani, Vodacom tutakutumia taarifa juu ya ofa zetu kwa njia ya SMS. Ikiwa hutopenda kuzipokea, tuma neno ONDOA kwenda 15030.
 
Vodacom wameandika ujumbe leo kuwa kama hutaki sms zao andika neno Ondoa

Ukiwa mmoja wa wateja wetu wa thamani, Vodacom tutakutumia taarifa juu ya ofa zetu kwa njia ya SMS. Ikiwa hutopenda kuzipokea, tuma neno ONDOA kwenda 15030.
Hawapaswi kuleta meseji zao na hawapaswi kunipa kazi ya kuandika ondoa! Wao waseme kuwa anayetaka meseji zetu za matangazo atuarifu ili tumletee meseji hizo, na wazitume kwa wale tu watakaoridhia!!
 
Raia wanatamani kusema kitu ila ndo ivyo asilimia 70% tunapatia ridhiki kupia mitandao Sasa serikali inapochukulia poaa swala la vifurushi hii mitandao itazidi kujifanyia.

Mambo itakavyo pia 89% ya watanzania hivi Sasa wapo kidigitari Yani Wana smartphones Sasa sijui tunaelekea wapi?

Kwangu Mimi ni kheri waondoe dakika sms lakini bando jamani liwe limeshiba maana ndo napatia ridhiki hapo🥹.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Waziri mwenye dhamana pia ni jipu!! kila siku yeye ni kutetea tu makampuni ya simu ambayo ni wezi wakubwa! Wewe fikiria utapeli kama huu: " ukitaka kupeleka ujumbe wa maneno bonyeza kitufe chochote" kabla hujafanya chochota ujue wameshaanza kurekodi mesejhi hewa na bwanakata pesa!1 mtu anapokea ujumbe ambao hauna maneno maana ulirekodiwa kwa lazima kwa ujanjaujanza wakijua kwa makosa kuna uwezekano wa kubonyeza kitufe chochote ikiwemo kitufe cha kukata simu!!
 
TCRA njoni hapa mweke kauli yenu, maana tunawatuhumu kushirikiana na makampuni nya simu, maana si kwa ukimya huu!!Malalamiko kibao hadi wabunge wanalalamika lakini mko kimyaaaa!!
 
Hata yule Waziri aliyesomea kupiga ngoma mwenye Wizara ni Ntu ya dili, hana uwezo na akili za Kuongoza Wizara nyeti kama aliyopo.

Kwakuwa Nchi iko mikononi mwa wajanja tunasema endeleeeni kula kwa urefu wa kamba ila ipo siku yaja.
 
Back
Top Bottom