Mitandao ya simu Tanzania ina staff wanajua biashara au "wezi"

Mitandao ya simu Tanzania ina staff wanajua biashara au "wezi"

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2018
Posts
1,484
Reaction score
2,892
Wanabodi,
Moja ya mambo ya ajabu na ya "hovyo" yanayofanywa na mitandao mingi hapa Tanzania ni kuongeza gharama kwa mteja/wateja wao juu kwa juu.

Unashangazwa kifurushi ambacho umenunua wiki jana week hii unakuta bei imeongezeka au kwa bei hiyo hiyo dakika na bando zinaminywa.

Hapo ndipo swali la msingi linaibuka, tuna wafanyabiashara wanaojua customer service ili ku-retain wateja au tuna "wanyang'anyi" ambao hawatupi punguzo kwa kuwa mteja/wateja kwa kuwa loyal kwao.
Makampuni mengi ya ndege, au baadhi ya hotels kwa regular customer with time anapata bonus na punguzo.
Hawa wanaofanya biashara kwetu hapa ni Watanzania. Badala ya kufikiria kutengeneza products mpya ziongeze mapato, wao wazo lao ni kumnyonya mteja kwa nyongeza ya bei kwa vifurushi au kuminya vifurushi ili kwa fedha ambao mara kwa mara ulikuwa unapata dakika na bando jamaa wanaminya.

TCRA sijui ni kwanini hawana mfumo kama EWURA au Latra (SUMATRA zamani) kwenye udhibiti wa huduma. Sitaki kufikiri wanatakuwa wanafaidika "kimtindo" kwa nyongeza ya gharama.

Nchi za wenzetu bei ya bidhaa au huduma mara kwa mara huwa zinakuwa stable hata kwa miaka 2 mpaka mitatu kwa bei hiyo hiyo.
Ila hawa jamaa wa simu wanaboa.
No wonder Watanzania tunahama sana mitandao kutafuta unafuu.

Ukiacha kutumia mtandao, unashangaa sms kila siku zikija kwa line ambayo hainunui tena vifurushi na promotion chungu mzima.

Si sawa. Inawezekana mnapuuza malalamiko ya Watanzania; ila kinachofanyika sio sawa.

Nadhani terms and conditions applied linatumika vibaya. Liko upande mmoja wa mtoa huduma za simu na sio kwa mnunuzi wa huduma (Mteja).

TCRA; kwa namna mnavyodhiiti na kuwang'amua wahalifu wa mitandao kwa haraka, iko haja kuwadhibiti watoa huduma wa simu pale wanapopandisha bei juu kwa juu hali kadhalika pale wanapouza vifurushi kwa kuminya wateja.

Unyonyaji sio mzuri. Ni wizi tu kama wizi mwigine.

Wasalam
 
HASA VODACOM. Ni majambazi wakuu, wasio na staha. Hawana adabu hata chembe. NI WEZI WA WAZIWAZI MAANA WAO GB MOJA UNAANGALIA VIDEO MOJA YA DAKIKA TANO YOUTUBE. Voda acheni wizi.
 
Back
Top Bottom