Habari za afya ya Dr. Harrison Mwakyembe

Habari za afya ya Dr. Harrison Mwakyembe

Mwanjelwa,

Mimi natofautiana na wewe kwenye hili japo nakubaliana pia na baadhi ya hoja zako.

Kwenye maendeleo kuna vitu vitatu muhimu ambavyo ni resources, watu na uongozi bora. Nyerere aliweka vitu vinne kwa kuongeza siasa safi. Uongozi bora kwa mawazo yangu unajumlisha siasa safi.

Tatizo la sehemu nyingi Tanzania ni capacity ndogo ya watu. Watu wanaweza kuwa na resources kwa mfano ardhi na wao wenyewe wakawa na nguvu za kuchapa kazi lakini hawana capacity ya kujiletea mabadiliko katika maisha yao.
Ndio maana hapa duniani hata kwenye makampuni makubwa uongozi bora ni nguzo kubwa. Ndio maana hao watu wanalipwa mamilioni ya pesa.

Ndio maana team moja leo inakaribia kushuka daraja, akija kocha mwingine unakuta wanaanza kupanda juu mara moja, watu ni wale wale, resources ni zile zile, kinachobadilika ni uongozi.

Sasa kwa experience yangu ya Tanzania, uongozi bora ni tatizo kuanzia wilayani mpaka kwenye taifa. Mbunge anayejua wajibu wake anaweza kuwa chachu ya maendeleo kwa kuunganisha resources zilizopo na watu waliopo. Anaweza kuona gap iliyopo na kisha kutumia njia mbali kama technology transfer akaiziba hiyo gap na hivyo akawa amewaletea wananchi maendeleo.

Politicians wana role kubwa ya ku play katika jamii, na wamekuwa wakifanya hivyo kwenye nchi mbalimbali. Ndio maana kuanguka kwa Wakomunist ghafla tukaona baadhi ya nchi zinabadilika. Hata kwa Tanzania, mbunge ambaye ni makini anaweza kuleta mabadiliko katika jimbo lake.

Nikupe mifano michache ambayo wengine tumewahi kufanya kule tunakotoka. Katika pita pita tukagundua wananchi wanalanguliwa kweli kwa mikopo ya ajabu ajabu, asilimia 30% kwa miezi sita. Mimi sikupenda hicho kitu, kuuliza wilaya wanafanya nini kutatua tatizo hilo? Hakuna aliyekuwa interested. Kuuliza jamaa mbalimbali nikagundua PRIDE wanatoa mikopo kama hiyo kwa riba nafuu sana, nikawatafuta na kuwaambia, japo mwanzoni walisita, baada ya muda wakaenda kuchunguza na kugundua kumbe soko ni kubwa sana. Leo hii hiyo wilaya iko katika kumi bora za PRIDE na vijana wengi wamefaidika kwenye biashara zao. Kuna mifano mingine mingi ambayo ukitaka niandikie PM nitakuambia.

Kuna viongozi wako pale miaka na hawaoni ni tatizo, wakati mtu mwingine unaenda siku moja na kuona hili ni tatizo inatakiwa litatuliwe kwa faida ya wananchi.

Kwa mawazo yangu viongozi na hata politicians wana role kubwa ya ku play katika kuwaletea maendeleo wananchi. Tukisema kuwaletea maendeleo wananchi haina maana kutumia pesa zao, ina maana wao kuwa catalyst of change. Kuwa troubleshooters wa matatizo yaliyoko wilayani kwao na kuandaa strategies ambazo zitasaidia kutatua hayo matatizo na hivyo kusogeza maendeleo mbele.

I don't understand. How can you be ushered with abundant rosources at the same time you don't have capacity to utulise them! Do you need someone to tell you what to do? Are the politicians meant for this purposes?! Utakuwa ujinga sana kusubiri, ati Mwakyembe akuambie namna ya kutumia raslimali zako mwenyewe! Mwakyembe kama yeye yuko pale ili mjadiliane namna ya kuendeleza kile mlichonacho na si kuanzisha namna ya kutumia kile ulichonacho.
 
- Sasa nyie watu wa Kyela hebu tumegeeni jana huko Kyela kumetokea nini nasikia kulikuwa na vurugu sana, mbona mmekuwa mabubu kwenye hili la jana mengine mankuwa mbele sana kutuambia,

- Hebu sasa wekeni yaliyojiri jana nimesikia mengi sana yaliyojiri ambayo sio mema kwa kiongozi mnayemfagilia ndio maana hamtaka kusema, sasa tuambieni basi yaliyojiri jana huko tunasubiri, Engeneer, Lazaromtindi, na Mwanjelwa tupeni yaliyojiri jana huko wakuu!

Respect.

FMEs!
 
I don't understand. How can you be ushered with abundant rosources at the same time you don't have capacity to utulise them! Do you need someone to tell you what to do? Are the politicians meant for this purposes?! Utakuwa ujinga sana kusubiri, ati Mwakyembe akuambie namna ya kutumia raslimali zako mwenyewe! Mwakyembe kama yeye yuko pale ili mjadiliane namna ya kuendeleza kile mlichonacho na si kuanzisha namna ya kutumia kile ulichonacho.
Mwanjelwa,

Unafurahisha mbona tuna resources nyingi lakini hatuna capacity ya kuzitumia? Mbona tuna chuma Liganga kimekaa tu na hatuna uwezo wa kuichimba kwa maendeleo ya nchi yetu. Mbona tuna maji tele kila sehemu lakini wananchi hawana maji safi ya kunywa? hawana umeme wa kutumia? Why?

Labda kama huelewi maana ya capacity building, lakini ni wazi lack of capacity ni tatizo Tanzania.

Naona hapo juu unajichanganya mno na ni wazi si ajabu hujui unataka ku present vipi mawazo yako. Hivi katika mijadala yote hii kuna mtu amewahi kusema wabunge au viongozi wengine wawanunulie bati za kuezeka nyumba za wananchi? Au walipie ada za watoto wa wananchi wao? Sijui umetoa wapi mfano kama huu.

Mfano mdogo kuna tatizo la walimu kwenye shule mbalimbali za Tanzania, sasa kama wewe ni mbunge wa wilaya husika utafanya nini? Kwa taarifa yako kuna solutions nyingi sana, hizo solutions mbalimbali ndizo wananchi kule wanaweza wasijue, kama kiongozi unaweza kuja na mawazo ambayo yanaweza kusaidia kupunguza hilo tatizo.

Mfano mwingine kule Kyela kuna Cocoa ambazo nyingi zilipandwa miaka ya 60, muda wake umepita, imebaki kuwa miti ambayo uzalishaji wake mdogo sana, wao wananchi wanaona ni sawa kwasababu hawajui option nyingine ni ipi. Kama wewe ni kiongozi utashindwa kujaribu kutatua tatizo kama hilo?

Mfano mwingine Kyela kulikuwa na maji safi ambayo yalijengwa na Wascandinavia, walipoondoka kila kitu kimekufa, kama hiyo sio lack of capacity utasema nini? Kungelikuwa na kiongozi makini angetafuta solutions kuhakikisha hayo mabomba na vyanzo vya maji vinatunzwa.

Any way, naona Mag3 amekuelemisha vizuri kabisa hapo juu, kama huelewi si ajabu na wewe kuna gaps nyingi zinatakiwa kuzibwa (capacity building). Jiandikishe hata na Open University hapo uelemike. Wengine kila siku tukiona kuna gaps kwenye uelewo wetu basi tunatafuta course haraka haraka ili isaidie kuziba, elimu haina mwisho.
 
Hapana. Hakuna kujichanganya hapa. Na hakuna sababu ya kujichanganya. Labda wewe uwe umchanganykiwa! Yes! Ni kweli kabisa kuwa maeneo mengi sana sana nchini watu wana uwezo na hawawezi kufanya mambo kulingana na uwezo wao.
 
Habari yenyewe ni hii ingawaje mwandishi kakwepa kuandika yale madongo aliyokuwa anarushiwa mbunge.

Pia kwenye kura kuna makosa, 48 ndio walisema warudishiwe uanachama na nafasi zao za uongozi, 22 walikubaliana na Mbunge kwamba wafungiwe miezi sita, wanne walisema warudishwe bila sharti lolote.

Huyo diwani wa Ipinda ni mtu wa Musoma, ndiye pia alimwambia mbunge, tulipojua msomi wa sheria anakuja kwetu tulifurahi, tukafikiri atatusaidia kuisukuma wilaya yetu mbele, lakini wewe umeshindwa hiyo kazi, kibaya zaidi unashindwa hata kutusaidia kutumia sheria yako kuongoza hivi vikao kwa kufuata sheria na haki, tunaanza hata kuwa na wasiwasi na hivyo vyeti vyako vya sheria. Mwakyembe alichukia na kumwambia wewe huna uwezo hata wa kudiriki kuhoji qualifications zangu. Kuna mengi mengine lakini wacha Nsesi na Lazaros watusaidie.

CCM WAMBANA MWAKYEMBE

Na Israel Mwaisaka, Mbeya

HALMASHAURI kuu ya CCM ya wilaya Kyela imemtuhumu mbunge wao Dkt,Harrison Mwakyembe pamoja na mwenyekiti wa CCM wilaya Bw,Japhet Mwakasumi kuwa ndiyo vinara wa kukigawa chama hicho katika makundi na kusababisha viongozi kushindwa kuelewana miongoni mwao iliyopelekea hivi karibuni makatibu kata kuwapiga viongozi wa wilaya

Tuhuma hizo zilitolewa na wajumbe wa kikao cha halmashauri kuu ya CCM wilaya kilichoketi jana ili kujadili maamuzi ya halmashauri ya mkoa ya chama hicho baada ya kukataa mapendekezo ya kamati ya siasa ya wilaya Kyela ya kuwavua uanachama makatibu kata wanne waliowapiga viongozi wa wilaya na kumsababishia maumivu makali katibu wa wilaya Bi,Maria Mwambanga

Katika kikao hicho wengi ya wajumbe walimshushia makomboraDkt,Mwakyembe kuwa toka yeye awe mbunge wa jimbo hilo ametengeneza makundi ndani ya chama huku akidaiwa kummiliki mwenyekiti wake wa chama wa wilaya ambaye ameonekana kuyumbishwa katika maamuzi yake mbalimbali

Walisema kufuatia hari hiyo ndani ya chama hicho kumekuwaepo na kutoelewana miongoni mwao na uhasama mkubwa kitu ambacho kimepelekea baadhi yao kuonekana wananyanyaswa na hawana haki ndani ya chama hicho na kuamua kuidai haki hiyo kwa kutumia nguvu kama walivyofanya siku hiyo viongozi hao wa kata

Mmoja wa wajumbe hao Bw,Christopher Mulemwah na ambaye ni diwani wa kata ya Ipinda alisema kuwa kamati ya siasa ilikurupuka katika kufikia uamuzi wa kuwavua uanachasma makatibu kata hao badala ya kukaa na kufikiri nini chanzo cha viongozi hao kufikia hatua ya kuamua kuwapiga viongozi wao wa wilaya

Alisema yeye binafsi anajisikia raha kuona mbunge huyo yupo ndani ya kikao hicho hivyo ni bora akaambiwa ana kwa ana kwani hata kutokea kitendo hicho Mbunge ndiyo chanzo kutokana na kauli zake alizozitoa kwenye kikao kama hicho kilichopita ambacho inadaiwa kuwa aliwakashifu wajumbe baada ya kuulizwa swali na mjumbe mmoja juu ya yeye kudaiwa kuwatuma watu kugombea nafasi za udiwani maeneo mbalimbali wilayani hapa

Mjumbe mwingine ambaye hakupenda jina lake kutajwa kutoka katika kata ya Ikama ndani ya kikao hicho alidai kuwa wao walimshitukia mbunge wao toka zianze chaguzi ndani ya chama hicho alianza kutengeneza makundi na kutaka kupitisha majina ya baadhi ya wagombea aliokuwa anawataka yeye wapite kwa gharama yoyote lakini baada ya wao kubaini hilo wagombea wote waliokuwa wakipigiwa upatu na mbunge huyo waliangushwa vibaya

Alisema lengo la wao kuwaangusha wagombea wote waliokuwa wakipigiwa kampeni na mbunge ni kutaka kuonyesha kuwa wao hawawezi wakachaguliwa viongozi kwani wao kama wanachama wana utashi wao na kumbe kufanya hivyo kulikuwa na nia ya kutaka kuweka watu wake ili kundi lake liweze kupata nguvyu kubwa

Katika kikao hicho wajumbe wote kwa ujumla waliamua kuwasamehe makatibu kata hao waliowafanyia vurugu viongozi na kutaka wapewe karipio kali ili wasirudie kufanya kosa kama hilo tena na ukichukulia hilo lilikuwa ni kosa lao la kwanza

Mbunge Dkt,Harrison Mwakyembe kwa upande wake alijitetea na kudai kuwa makundi hayo yanayoendelea ndani ya chama hicho yanazorotesha maendeleo mbalimbali na kana kwamba haitoshi hari hiyo imewaambukiza hata watu wa Kyela waishgio jijini Dsm kujigawa kimakundi kwa sababu tu ya makundi yaliyopo Kyela

Alisema yeye binafsi hapendi kuona viongozi hao wanafikishwa mahakamani na kufungwa bali kilichopo ni chama kuchagua wazee wachache wenye busara kwenda kuwaombea radhi makatibu kata hao kwa katibu aliyepigwa ili mambo hayo yaishe

Katika mkutano huo kulikua na mvutano mkali miongoni mwa wajumbe hao ambapo wengine walisema kuwa wasamehewe bila masharti yoyote,wasimamishwe miezi 6 ambapo wengine walisema kuwa wapewe onyo kali lakini warudishwe kwenye chama na nafasi zao

Baada ya malumbano ya muda mrefu waliazimia kupiga kura ambapo wajumbe waliokuwepo walikuwa 77 na baada ya kura kupigwa wajumbe 48 walikubali kuwa makatibu kata hao wasamehewe na kupewa onyo,4 zilisema wafungiwe miezi 6 ambapo kati ya hizo moja tu ndiyo iliyoharibika

Na baada ya kura kupigwa na kutolewa matokeo chama kililidhia maamuzi ya kuwasamehe viongozi hao wa kata ila wapewe onyo kali na kulichukua kuwa ni kama pendekezo litakalopelekwa katika kikao cha halmashauri ya mkoa kwa maamuzi zaidi

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya Bw,Japhet Mwakasumi alipotakiwa kuzungumzia maamuzi hayo mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho alidai kuwa kwa sasa hawezi akalizungumza suala hilo bali wenye uwezo ni viongozi wa mkoa kwa maana kuwa pendekezo hilo ndiyo linapelekwa kwao
.
 
Wakuu,

Kyela japo tuna jambo moja la kujivunia, tuna diwani Chris ambaye anatokea mkoa wa Mara, kuna diwani Mahenge ambaye ni Mkinga toka Iringa. Tuna mbunge ambaye unaweza kusema anatokea wilaya ya Rungwe.

Nani alisema Kyela kuna ubaguzi? Kule wananchi wanachojali ni watu ambao wanaonekana wanaweza kusaidiana nao kusukuma gurudumu mbele.

Hongera wana Kyela kwa hilo.
 
.............Mfano mdogo kuna tatizo la walimu kwenye shule mbalimbali za Tanzania, sasa kama wewe ni mbunge wa wilaya husika utafanya nini? Kwa taarifa yako kuna solutions nyingi sana, hizo solutions mbalimbali ndizo wananchi kule wanaweza wasijue, kama kiongozi unaweza kuja na mawazo ambayo yanaweza kusaidia kupunguza hilo tatizo.

Mfano mwingine kule Kyela kuna Cocoa ambazo nyingi zilipandwa miaka ya 60, muda wake umepita, imebaki kuwa miti ambayo uzalishaji wake mdogo sana, wao wananchi wanaona ni sawa kwasababu hawajui option nyingine ni ipi. Kama wewe ni kiongozi utashindwa kujaribu kutatua tatizo kama hilo?

Mfano mwingine Kyela kulikuwa na maji safi ambayo yalijengwa na Wascandinavia, walipoondoka kila kitu kimekufa, kama hiyo sio lack of capacity utasema nini? Kungelikuwa na kiongozi makini angetafuta solutions kuhakikisha hayo mabomba na vyanzo vya maji vinatunzwa...........

sasa mshirikiane basi mpeni hizo solutions Mbunge wenu.........
 
Kengele ya hatari
lala salama. tutasikia na kuona mengi
 
CCM WAMBANA MWAKYEMBE
Na Israel Mwaisaka,Mbeya

Tuhuma hizo zilitolewa na wajumbe wa kikao cha halmashauri kuu ya CCM wilaya kilichoketi jana ili kujadili maamuzi ya halmashauri ya mkoa ya chama hicho baada ya kukataa mapendekezo ya kamati ya siasa ya wilaya Kyela ya kuwavua uanachama makatibu kata wanne waliowapiga viongozi wa wilaya na kumsababishia maumivu makali katibu wa wilaya Bi,Maria Mwambanga

Katika kikao hicho wengi ya wajumbe walimshushia makomboraDkt,Mwakyembe kuwa toka yeye awe mbunge wa jimbo hilo ametengeneza makundi ndani ya chama huku akidaiwa kummiliki mwenyekiti wake wa chama wa wilaya ambaye ameonekana kuyumbishwa katika maamuzi yake mbalimbali

Katika kikao hicho wajumbe wote kwa ujumla waliamua kuwasamehe makatibu kata hao waliowafanyia vurugu viongozi na kutaka wapewe karipio kali ili wasirudie kufanya kosa kama hilo tena na ukichukulia hilo lilikuwa ni kosa lao la kwanza

Mbunge Dkt,Harrison Mwakyembe kwa upande wake alijitetea na kudai kuwa makundi hayo yanayoendelea ndani ya chama hicho yanazorotesha maendeleo mbalimbali na kana kwamba haitoshi hari hiyo imewaambukiza hata watu wa Kyela waishgio jijini Dsm kujigawa kimakundi kwa sababu tu ya makundi yaliyopo Kyela

Mtanzania,
Nilisikia kuna jamaa waliompiga mwana CCM mwenzao kwamba walipokamatwa na POLISI wakasema kuwa wanadhaminiwa na Mbongo mmoja aliyeko UK, sasa imeishia wapi? Kumbe mpika majungu alikuwa Mwakyembe? Si tulisema hapa zamani?

Lazarus, tulikuambia kuwa Kosa kubwa la Mwakyembe ni kutengeneza makundu. Hizo siasa za au uko na mimi au wee ni adui yangu hazitamfikisha mbali. Sasa hivi angelikuwa kashafika mbali katika kujirudisha katika reli inayotakiwa. Mkabisha hapa weee na sasa kiko wapi? Kapoteza muda wa bure na kuzidi kujichowa nguo zake za heshima alizovalishwa siku anasoma riport ya Richmonduli. Mwisho sasa hata yeye kakubali kuwa makundi yanaumiza wananchi. Hata mie naanza kupata wasiwasi kama jamaa kasoma kweli na KUELIMIKA.

Mwakyembe, bado unaweza kubadika na kujiokoa wewe na Wanakyela. Tafadhali sikiliza ushauri wa bure unaopewa na watu humu ndani. Wanaokufahamu wanasema kuwa "Mtu una uwezo wee na busara kubwa sana.... ila zinakuponza dharau zako". Mwenyewe ulisema "Watanzania si mabwege tena, sasa kwa nini wewe mwenyewe unaanza kuwaona Watanzania ni Mabwege?"
Kama sikosei utakuwa Mmoravian kama mimi. Sasa nikwambie kuwa hata kwenye Biblia yetu imewemwa "Kumbuka ulipoangukia, nenda sasa ukatubu...." Kama hutakumbuka uliangukia wapi, basi kazi unayo na jiandae kuumbuliwa mara kwa mara kama hiyo jana.
Vinginevyo wee rudi tu UKAFUNDISHE maana huko hakuna anayebisha kuwa uwezo upo. Dr mzima kupurukushana na vitoto vya from 4? Wakati mwingine Pesa siyo kila kitu. Hata Mziray alikimbia Simba na Yanga na kwenda kuwa mwalimu wa michezo UDSM.
 
sasa mshirikiane basi mpeni hizo solutions Mbunge wenu.........
Ogah,
Wengine tumejaribu kushirikiana, lakini ili ushirikiano uwepo si ni lazima pande zote mbili ziwe tayari kushirikiana?

Suala la Kyela mimi sasa nimejiondoa kuongelea watu hivyo sitaingia ndani zaidi.

Mbona hujatupongeza kwa kutokuwa wabaguzi? Hata dadako na wajomba zako wanaruhusiwa kugombea vyeo Kyela.
 
Mtanzania,
Nilisikia kuna jamaa waliompiga mwana CCM mwenzao kwamba walipokamatwa na POLISI wakasema kuwa wanadhaminiwa na Mbongo mmoja aliyeko UK, sasa imeishia wapi? Kumbe mpika majungu alikuwa Mwakyembe? Si tulisema hapa zamani?
Sikonge,

Mbongo huyo huyo wa UK sasa wanapita makanisani kupandikiza chuki kwamba misaada anayosaidia, kapewa pesa na Lowassa, ndio siasa zetu za Tanzania, ni mufilisi. Jamaa mwenyewe anasaidia kwao kila mwaka kuanzia miaka ya 90, basi huyo Lowassa keshamjaza jamaa mapesa mengi kweli kweli.

Jamaa mwenyewe huko aliko anacheka tu. Boksi linachosha bwana, wacha jamaa akunje pesa za EPA naye atanue kidogo kwi kwi kwi!!!

Vijana mnaotaka kwenda huko mwakani jiandaeni kweli kweli kwa vita.

Ila uzuri wa dunia hii ukipandikiza chuki utavuna chuki, ukipandikiza neema unavuna neema. Watanzania sio mabwege tena!
 
Ogah,
Wengine tumejaribu kushirikiana, lakini ili ushirikiano uwepo si ni lazima pande zote mbili ziwe tayari kushirikiana?

Suala la Kyela mimi sasa nimejiondoa kuongelea watu hivyo sitaingia ndani zaidi.
.

Mkuu Mtanzania, tafadhali usijiondoe kwenye huu mjadala. Shule unayotoa hapa si ya kitoto. Hongera sana and keep going man.
 
Tukizungumzia maslahi ya Taifa na sio Binafsi..Mbinu za kumchafua Mwakyembe haziwezi kushinda... inajulikna kwamba kuna kundi linataka kuona Mwakyembe, Mama Kilango, Sitta na baadhi wabunge hawarudi ktk uchaguzi wa mwaka 2010 kwa sababu wabunge hawa wamekuwa chachu ya chama hicho hata kusababisha kundi kubwa la viongozi kuondolewa madarakani..
Kwa hiyo yatasemwa mengi sana, lakini ukweli unabakia kwamba makundi ndani ya chama hayakuanzishwa na Mwakyembe.. tunayaona Busanda na kila kata, wilaya mkoa kwa sababu hakuna kiongozi asiyetaka kukaa meza kubwa ktk kugawana umaskini..
Na Machafuko ndani ya CCM yanaweza kuwa sababu kubwa ya ushindi kwa vyama vya Upinzani hivyo wao waendelee tu kujimaliza na siasa uchwara za kupigana makonde wakati sinia la ubwabwa linaisha.
 
Ninachoogopa ni kumfrustrate Dk. and at the end of a day ajikute yuko peke yake. Lets hope for the best maana hata yeye ni DEEP GREEN.
 
Mtanzania

Kwa kweli unafurahisha sana katika arguments zako kuhusu Kyela. Kwako ni kujitahidi uj8ionyesha wanakyela hawna wanalolifanya zaidi yahao watu wako hao wawili unaowatetea kwa nguvu zote kupitia kibwagizo cha ukabila.

Pengine nianze na huyo DC kwa kukuliza maswali yafuatayo;

1. Hivi alipotimuliwa U-DC wakati wa Mkapa nayo ilikuwa ni sababu ya majungu na ukabila wa watu wa Kyela!
2. Je alipofunaniuwa na mkewe hata akasimamishwa na RC Mwakipesile kumkaimisha DC wa Ileje tena kwa kumuapisha, na maelezo yake kwamba mwenzetu kapata ajali ya ndoa; haya nayo yalifanywa kutokana na majungu na ukabila wa watu wa Kyela!
3. Je unaelewa hao wafanyakazi wa Kiwira aliowahadaa ndio waliovujisha siri ya DC huyo kuhongwa VX (japokuwa unapotosha hapa kwamba niliandika kuwa wafanyakazi hao masikini wamemhonga DC vx) kwa shilingi laki sita? na habari ilipotoka kwenye vyombo vya habari hakukanusha!
4. Hivi kukaa naye ofisini akakupa maelezo yake ndio kumuelewa sawa sawa kwamba alikuwa mchapa kazi, na kwamba watu anaofanya kazi nao kila siku hawamfahamu sawa sawa ile wewe uliyeoko UK!

Pili ni huyo diwani wako unayedai anaandamwa kwa sababu ya ukinga wake, hivi Kyela kuna Mkinga mmoja tu! Na kama ana madhambi ikiwemo nyumba yake kutumika kuharibu watoto wa shule pale mjini, watu wasiseme kwa sababu itakuwa ni ukabila!

Je unao ushahidi gani kwamba Dr Mwakyembe alituma vijana wake wamuorodheshe huyo Diwani kwenye tuhuma za wanaofanya biashara ya viungo vya albino? Wakati hata taarifa za hizo kura hazijatolewa mwenzetu wa UK umezipataje au ndo majungu yenu na wewe na huyo rafiki yako DC aliyeondolewa!

Hivi ni kwa lipi hasa Dr Mwakyembe amuandame huyo diwani wakati hata huo udiwani aliupata kupitia mgongo wake kutokana na kutokubaliwa na wakazi wa kata hiyo ya Kyela Mjini ambayo ghata hivyo wakazi wake wengi ni mchanganyiko!

Kupitia hoja zako ni wazi unayo ajenda yako dhidi ya wilaya ya Kyela hivyo ni vema ukawa muwazi, watu wakakuelewa na si kuwapaka matope wanakyela pasipo sababu za msingi.

Wana Kyela walioko Dar ambao wewe unawaita kuwea mtaji wa Dr Mwakyembe wanafanya mengi makubwa kwa ajili ya wilaya yao na si kuendekeza majungu kama ufanyavyo. Wakazi wewe unaziona habari za mafuriko ya Kyela kuwa za kutafutia misaada, wenzio wanayachukulia mafuriko kuwa janga hivyo wanapeleka misaada ya hali na mali kwa wahanga kama ilivyokuwa mwaka jana.

Mtanzania huna uchungu wowote na Kyela kama unavyotaka watu wakuelewe, una interests zako, time will tell.

Nsesi,
Unachemsha mtu wangu.Data zako sio za Ukweli.
Tunakuuliza,Mwakyembe kafanya yapi?.Jibu Kimya

Kikubwa alichofanya hapa ni kuwagawa watu.Ulikuwepo jumamisi pale community center?.mavi yalimbana na mpaka aliomba kujuzuru.

Achana na ujinga unaotwandikia hapo.Yeye akagombee Dar ambako itakuwa rahisi kwake kupambana na mafisidi wake.
 
Waandishi wa Mkwakyembe utawajua tu. Mwanzo karukaruka wee hadi mwisho kakiri kuwa yeye ni Mwandishi. Haya, mwanzo anadai haya ni majungu ila mwisho anasema kuwa ALIKUWEPO KWENYE MKUTANO. Too sad indeed.
.

Ndugu yangu Sikonge.

Huyo Lazoro Ntindi ndiye Mwakyembe wenyewe.
Niliwahi kumkuta akilitumia jina la Mtindi kupotosha watu.

Ndugu yangu Ntindi huo ndio usanii wenyewe.
 
Mtanzania,
Nilisikia kuna jamaa waliompiga mwana CCM mwenzao kwamba walipokamatwa na POLISI wakasema kuwa wanadhaminiwa na Mbongo mmoja aliyeko UK, sasa imeishia wapi? Kumbe mpika majungu alikuwa Mwakyembe? Si tulisema hapa zamani?

Lazarus, tulikuambia kuwa Kosa kubwa la Mwakyembe ni kutengeneza makundu. Hizo siasa za au uko na mimi au wee ni adui yangu hazitamfikisha mbali. Sasa hivi angelikuwa kashafika mbali katika kujirudisha katika reli inayotakiwa. Mkabisha hapa weee na sasa kiko wapi? Kapoteza muda wa bure na kuzidi kujichowa nguo zake za heshima alizovalishwa siku anasoma riport ya Richmonduli. Mwisho sasa hata yeye kakubali kuwa makundi yanaumiza wananchi. Hata mie naanza kupata wasiwasi kama jamaa kasoma kweli na KUELIMIKA.

Mwakyembe, bado unaweza kubadika na kujiokoa wewe na Wanakyela. Tafadhali sikiliza ushauri wa bure unaopewa na watu humu ndani. Wanaokufahamu wanasema kuwa "Mtu una uwezo wee na busara kubwa sana.... ila zinakuponza dharau zako". Mwenyewe ulisema "Watanzania si mabwege tena, sasa kwa nini wewe mwenyewe unaanza kuwaona Watanzania ni Mabwege?"
Kama sikosei utakuwa Mmoravian kama mimi. Sasa nikwambie kuwa hata kwenye Biblia yetu imewemwa "Kumbuka ulipoangukia, nenda sasa ukatubu...." Kama hutakumbuka uliangukia wapi, basi kazi unayo na jiandae kuumbuliwa mara kwa mara kama hiyo jana.
Vinginevyo wee rudi tu UKAFUNDISHE maana huko hakuna anayebisha kuwa uwezo upo. Dr mzima kupurukushana na vitoto vya from 4? Wakati mwingine Pesa siyo kila kitu. Hata Mziray alikimbia Simba na Yanga na kwenda kuwa mwalimu wa michezo UDSM.
.

Sikonge.
Mwamie na Lazaro Ntindi pia.
Huyo ndiye Mwakyembe junior
 
Ndugu angu Sikonge,
Mwakyembe hawezi kubadilika.Hiyo ni tabia yake.
Kuna Taarifa ya leo na ninahisi niyeye mwenyewe ameiandika kwenye gazeti la majira.Sasa anaonekana kuomba huruma ya wananchi.

Mwakyembe dharau,Kiburi na kutotekeleza majukumu yako kwa wanakyela ndicho kitachokuondoa madarakani.
 
Tukizungumzia maslahi ya Taifa na sio Binafsi..Mbinu za kumchafua Mwakyembe haziwezi kushinda... inajulikna kwamba kuna kundi linataka kuona Mwakyembe, Mama Kilango, Sitta na baadhi wabunge hawarudi ktk uchaguzi wa mwaka 2010 kwa sababu wabunge hawa wamekuwa chachu ya chama hicho hata kusababisha kundi kubwa la viongozi kuondolewa madarakani..
Mkuu Mkandara,

Mbunge akiwa mchapa kazi, hata kuwe na nguvu vipi, hawezi kuondolewa na wapiga kura wake. Tumeona akina Dr. Slaa wanavyoandamwa lakini kule kwao wanapeta tu. Tumeona akina Ndesamburo nao wanapeta tu.

Kyela nako itakuwa hivyo hivyo, kama wananchi wataridhika na utendaji wa mbunge wao basi watampa nafasi nyingine. Wakiamua kumtoa ni kwa mapenzi yao, haya mambo ya kwamba wanatumwa na watu wengine ni dharau kubwa kwa hao wananchi.

Tusubiri mpambano wa 2010 na tutasikia mengi sana kabla ya hapo.
 
Nsesi,
Unachemsha mtu wangu.Data zako sio za Ukweli.
Tunakuuliza,Mwakyembe kafanya yapi?.Jibu Kimya

Kikubwa alichofanya hapa ni kuwagawa watu.Ulikuwepo jumamisi pale community center?.mavi yalimbana na mpaka aliomba kujuzuru.

Achana na ujinga unaotwandikia hapo.Yeye akagombee Dar ambako itakuwa rahisi kwake kupambana na mafisidi wake.
...bado tupo ktk zoezi la kutambua aliye upande wetu na aliye upande wa mafisadi. Hatumtetei Dr. hapa ila tunaweka maslahi ya Tanzania kwanza. Kama wewe unaona kyela haijaathirika na mafisadi basi itabidi tukutafutie mawani ya kifikra maana mwenzetu huoni hapo ulipo.

Kwa hiyo unasema mafisadi wa Dr. hawana madhara kwa taifa? Is that it Samweli, ni kweli samweli, samweli hayo ni kweli???
 
Back
Top Bottom