Habari za afya ya Dr. Harrison Mwakyembe

Mzozo wa Mizozo

JF-Expert Member
May 26, 2008
426
9
Kuna mtu yoyote ambaye ana taarifa sahihi husiana na hali ya kiafya ya Mh. Mwakyembe maana mtaani kuna habari tata mno.

Naomba tushirikiane.
 
Kuna mtu yoyote ambaye ana taarifa sahihi husiana na hali ya kiafya ya Mh. Mwakyembe maana mtaani kuna habari tata mno.

Naomba tushirikiane.

Huo ni uvumi tu, wala hakuna kitu, Dr. Mwakyembe ni mzima tu ukiachia matatizo ya jana ambayo ni ya kawaida kama alivyosema yeye mwenyewe.

Mimi mwenyewe nimeusikia lakini nina uhakika Dr. ni mzima tu.

Inaelekea Watanzania tunawaogopa sana mafisadi, hawana kitu hao, wanapoona tunawaogopa ndivyo wanavyozidisha vituko vyao.
 
Aliugua jana ghafla wakati wa mwanzo wa siku ya Bunge, akapelekwa kliniki ya Bunge kwa huduma ya kwanza na baadaye akatakiwa apumzike, na sasa anapumzika nyumbani. Anaendelea vizuri na yuko kwenye mipango ya kufanyiwa uchunguzi zaidi na kama kutakuwa na mahitaji ya matibabu au uchunguzi wa kitaalamu zaidi basi atafanya hivyo.
 
Mwanakijiji,

Wenzako wanaeneza uvumi kwamba Dr. kafariki. Watanzania tumezidi uwoga.
 
Kuna mtu yoyote ambaye ana taarifa sahihi husiana na hali ya kiafya ya Mh. Mwakyembe maana mtaani kuna habari tata mno.
Naomba tushirikiane.

Hahahahaaa...wewe unakuja Jamiiforum kuuliza habari zenye utata? Hapa ni worse kuliko hata huko mitaani....
 
Hahahahaaa...wewe unakuja Jamiiforum kuuliza habari zenye utata? Hapa ni worse kuliko hata huko mitaani....

Jamani dokta ni mzima kabisa. Hizi ni taarifa za uhakika. Aliamua kuzima simu yake kukwepa usumbufu na alipokosekana hewani kwa muda nmrefu ndio huu uvumi kuwa ameaga dunia ukaanza kusambaa. Naomba kuwahakikishieni kuwa bado anaendelea na mapumziko na hali yake wala si mbaya.
 
Mtanzania hilo la kifo lilianzishwa humu mapema leo, na nikalizima kwa kuzungumza na Dr. mwakyembe mwenyewe.. na kuwaambia watu kuwa ni mzima (kwa maana yuko hai) lakini bado anajiandaa kufanyiwa uchunguzi zaidi.
 
Jamiiforums watu huwaga wanakufa halafu wanafufuka....'memba me?
 
Jamiiforums watu huwaga wanakufa halafu wanafufuka....'memba me?

I remember your tragic death and quick resurrection!!! Licha ya wewe Nyani Ngabu, hata Mzee wa Vijisenti alienda kuzimu akarudi siku hiyo hiyo, siyo baada ya siku tatu!!! Yetu macho na masikio ila kwa huyu Mzalendo Mwakyembe naamini huu ni uvumi tu kwani nimepiga simu kwa watu watatu mbali mbali huko Dodoma wanakanusha na kushangaa!! wana JF tumuombee shujaa wetu apate nafuu mapema kwani twamuhutaji bungeni kwenye mijadala mizito ijayo.
 
Watanzania tunaanza kuanza tabia ambazo siyo za kawaida. Inashangaza mtu kuanzisha uvumi wa kifo bila kuwa na uhakika. Tumwombee Harrison afya njema na roho za kuzimu zishindwe.
 
..si uwoga, ni ushenzi, tabia mbaya na ukosefu wa adabu!! wanamchulia babu wa watu...kitu kidogo tu, kafa, mara oooh kafa....utafikiri kufa kumeanza leo (yaani ni kitu kipya)!!! waTZ na TZ yenyewe ovyo sana......inakera.

Uwoga niliousema ni kwamba kuna watu wanaamini Mafisadi wana nguvu sana, wanaogopa mafisadi mno. Mafisadi hawana kitu wala hawawezi kumwua Dr.
 
Na wewe ufe na usifufuke...
 
Bunge limetoa taarifa kuwa Mwakyembe hajafa. Alikwenda kwa Spika kumuaga kuwa anakwenda dar na atarejea Jumapili. Sasa kwa wanaoeneza uvumi wakae tayari, Bunge limesema jeshi la Polisi limeanza kuwasaka walioeneza uvumi huo ili wachukuliwe hatua. Aliyesema na naibu Katibu wa Bunge, Dk Thoams Kashilila
 
Uwoga niliousema ni kwamba kuna watu wanaamini Mafisadi wana nguvu sana, wanaogopa mafisadi mno. Mafisadi hawana kitu wala hawawezi kumwua Dr.

Mkuu tema mate chini bro, hivi umesikia yaliyomjiri Ditopile? I mean unapoona viongozi wote wakubwa wa taifa hawataki kualikwa kwenye dinner isiyokuwa na buffet, yaani ya kila atakayehudhuria aonekane anachota mwenyewe chakula chake mbele ya hadhara,

Halafu watangulie watu wengi kabla kiongozi hajaingia kwenye line naye kuchota tena pale pale walipochota wananchi wengine, mkuu ujue kuna jambo, sisemi ndiyo yaliyomkuta Mwakyembe, lakini wallahi hapa kuna kuna maneno! Haya ndio masharti mapya ambayo viongozi wote wa juu hudai ili wahudhurie tafrija yoyote ya chakula siku hizi!

Ndugu yangu, muamini Mungu lakini funga na funguo milango ya gari lako, usije ukaenda bongo kichwa kichwa!
 
Bunge limetoa taarifa kuwa Mwakyembe hajafa. Alikwenda kwa Spika kumuaga kuwa anakwenda dar na atarejea Jumapili. Sasa kwa wanaoeneza uvumi wakae tayari, Bunge limesema jeshi la Polisi limeanza kuwasaka walioeneza uvumi huo ili wachukuliwe hatua. Aliyesema na naibu Katibu wa Bunge, Dk Thoams Kashilila

Mkuu kweli inawezekana mafisadi ndiyo wanavumisha hizi habari hili wapate ushindi. Si tulitegemea bunge hili lifanye kazi? Nafikiri hivi vinaweza kuwa ni vitisho hili waliokuwa wameamua kufanya kazi wasiweze kuwazungumza akina Makapa et al
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom