Sikonge
Karata mbili za mafisadi zitakazo weza kumjeruhi Dr ni
1. Kumtoa roho yake
2. Kuhakikisha wanaipeleka ahera kabisa maana wakiitoa na akaenda peponi itakuwa ni ushindi mkubwa sana kwake.
we endelea kuwaendekeza mafisadi na kuwapa moyo kwamba wana karata mbili. Ungekuwa unampenda kwa sababu umesema unazijua ungezimwaga hapa nasi tutamfikishia lakini hauna mapenzi naye yoyote zaid ya kumchukia si jui kwa lipi eti ana dharau! nikuorodheshee list ya enye dharau hapa na hujawahi kusema hata siku moja ila aliye wataja mafisadi ndiyo anadharau
Mhhh, naona unachanganya Yesu na Wayahudi? Hapo tu ni mwanzo wa mchanyato mzuri sana. Haya, Shaloom- unamaana Dr ni myahudi na yesu ni mwakipesile? kuwa straight ndugu
Shalom,
Mbona unakuwa kituko? Nilianza kukupa heshima na kufikiri ni mtu unayetaka hapa tuelimishane, kumbe wee somehow unaboil! Too sad.
Karata mbili ninazozifahamu mie, mbona waziuliza wakati mwenyewe umeziandika hapo juu? Si zi-copy hizo karata mbili na umpelekee Mwakyembe? Atakusifu sana kijana kuwa "wee kijana una akili sana" na milele hata kuja kusahau BUSARA zako na werevu wako ukiachilia mbali ujasiri wa kumpelekea KARATA za maana namna ile.
Mwakyembe huwa anakuja hapa na tulimwambia yeye INDIRECT/DIRECT. Tulijifanya hatujamfahamu ila kumbe tulishamgundua. Hata sasa hivi niko njiani kum-trace na hivi kipunde ntamgundua tena yuko kwa jina gani. Huwa akija anajifanya kukosea kila kitu na akibanwa hukiri tuliyokuwa tunasema. Tatizo yeye anafikiri yeye kwa sababu ni Dr. basi wengine wote ni mabwege. Inawezekana siye si Ma.dr. wa sheria ila kitendo cha yeye kuambiwa na Chriss kuwa "na kuwa mwana sheria unashindwa kuongoza kikao kwa kufuata sheria......" huo ni mzinga wa soo.
Kama tukiacha utani, karata hizo, moja alishaiandika humu ndani Field Marshal ES. Sintataka kukuambia iko wapi na ukitaka waweza kumuuliza. Nyingine ilijianika hata bila ya yeye kujua. Hii ilifumuka wakati wa mazishi ya Marehemu mama yake (RIP). Sasa kama yeye ana akili na ni Dr. wa sheria, mwambie hivyo tu na atajua ni kitu gani hicho alichojianika. Kama waliokuja kwenye Mazishi wakiwa ni ndugu, jamaa na marafiki hadi leo hawajamwambia, basi kweli hana ndugu, jamaa na marafiki wa kweli au ni kuwa dharau zake hata hao watu wake wa karibu wanaamua wamuache azame katika tope hizo chafu.
Muda wa MAFISADI bado sana. Nina imani watamfumua mwezi mmoja kabla ya uchaguzi na hapo hatapata hata muda wa kuamka tena. Kama unalaani sisi hatumuambii moja kwa moja, basi rudi nyuma na usome jumbe zetu. Tulimuonya zamani sana. Huwezi tenga watu hata kama ni Wanafiki. Wee kama Mwanasiasa, lazima ujuwe kuwa KINYONGA. Kama hujui basi utawezaje kuongoza watu wanaokupinga na wasiokupinga? Angelimaliza ugomvi na Mwakipesile (alikuwa na uwezo huo - Mfano wa Obama na Clinton), akawavuta wapinzani wake wote na kuwa nao chini, sasa hivi wala tusingelikuwa tunaongelea hili. Mbona Dr. Slaa kwake kimya?
Shalom, Mwakyembe siyo siri ana uwezo MKUBWA SANA SANA wa kufanya mambo makubwa na hata tuseme MAAJABU. Kinachomuuwa hi hizo sababu mbili nilisema mwanzo za Au uko na mimi au uko against me/Dharau. Angejirekebisha hayo makosa mawili, basi angelibaki na ugomvi na MAFISADI tu na sisi wote humu ndani tungelikuwa upande wake.
Mwisho usitutishe kuwa ANAWEZA KWENDA KUFANYA KAZI NYINGINE. Si aende akafanye hata leo hii, njia NYEUPE. Tuliimba/tuliimbiwa kuwa bila Nyerere, Tanzania ingelikuwaje, mbona ipo? Tanzania itakuwepo/Kyela itakuwepo bila ya kujali Mwakyembe yupo au hayupo. Mchimba shimo, kajiingiza mwenyewe na dharau zake.
Haya chukua ring la baiskeli, endesha mbio kwa Mwakyembe kamwambie yote uliyoyasikia hapa. Na kama wee ndiyo Mwakyembe mwenyewe, basi ujumbe umefika. Kama ni ndugu basi Msimlemaze ndugu yenu, mpeni shure kwani ukweli unauma ila kesho atakuja kusema ASANTE.