Habari za afya ya Dr. Harrison Mwakyembe

Habari za afya ya Dr. Harrison Mwakyembe

Yaani wewe mpaka utafute kwenye MTANDAO? Mie nilishawahi kukaa na WAYAHUDI wenyewe na ninafahamu maana yake bila ya kufungua kwenye Internet. Ndiyo maana nikakuambia kuwa Wanatuma Wayahudi. Sasa kwenda kuhangaika na kupoteza muda kote huko kulikuwa kwa nini? Pole sana MJOMBA. Mwisho nilikuambia hili wala si MUHIMU, lilinifurahisha tu kuona WAYAHUDI na YESU wamesimama sehemu moja.

Maadamu Unawapenda wote, si waambie wote WALETE MAHALI KWA MZEE?? Yes, sasa ndiyo nachemsha!!

ndiyo maana unampinga Dr naona umekaa kimwakipesile mwakipesile hivi!

ILa nakuhusia ndugu yangu Yesu hataniwi, afanyiwi mdhaa wa dhihaka ya aina yoyote. Usije sema sikukuonya ndugu yangu
 
Viongozi gani mliwowachagua Tabora! mzee naona ujumbe wako nimzito au unafukuzia tenda
 
ndiyo maana unampinga Dr naona umekaa kimwakipesile mwakipesile hivi!

ILa nakuhusia ndugu yangu Yesu hataniwi, afanyiwi mdhaa wa dhihaka ya aina yoyote. Usije sema sikukuonya ndugu yangu

Huyu Mwakipesile alikuwa kama viongozi wa Tabora. Watu wa Kyela wakaamua kumtosa na baada ya kusikiliza hotuba za Mwakyembe na mambo yake, wote wakaamini huyu atakuwa si tu kiongozi, ila mshikaji. Aliposhinda, watu wakamwambia, nenda kapatane na Mwakipesile. Siku hizo Mwaki alikuwa looser fulani hivi. Jamaa kwa kuwa kashashinda, akaanza kufungua makucha. Akatukana kabisa, kuwa yeye na looser ni mbalimbali. Siku kadhaa zinapita, jamaa kawa mkuu wa mkoa, KIKO WAPI? Angelikuwa kashapatana naye, saa hizi wangelikuwa washikaji.

Bado naamini Mwakyembe ana uwezo MKUBWA SANA. He can do better than that. Mie ni mshabiki sana wa Mwakyembe ila nisikufiche, nilipopewa hizi habari, nilitaka kulia. Sikuamini mtu niliyeanza kujenga imani kwake kubwa namna hiyo, anafanya vitu kama hivi.

Amini usiamini, ningelikuwa simpendi Mwakyembe, wala nisingelikuwa naandika hizi habari. Hawa wote sijawahi kuwaona hata siku moja live. Mie mtu wa Sikonge huku ila nina jamaa/ndugu zangu Kyela. Jamaa wakiwa Sikonge, wakiwa kwangu ni kuwa wako nyumbani. Najiandaa na mie kwenda Kyela maana undugu ni kutembeleana.

Sasa kijana, hujui wimbo wa "Yesu kwetu ni RAFIKI...?" Yesu ni rafiki yetu ila Mungu mhhhh KIGINGI. Hapo ndiyo siwezi hata kuweka utani. Ila Jesus ni wetu sana. Tunaweza hata kumtania. Kwani unafikiri wanafunzi wake walikuwa hawamtaninii? Si ajabu walikuwa wanamsakizia hata totoz. Ehhh Yesu, hebu cheki kitu hicho, kimejaza paja la nguvu kama la Mnyakyusa.

Viongozi gani mliwowachagua Tabora! mzee naona ujumbe wako nimzito au unafukuzia tenda

Mzee, viongozi wa Tabora, kwi kwiii kwiiiiiiii. Duu mzinga wa SOOO!!! Yaani ni Choo kirefu haswa haswa. Ukianzia na Seleli aliyemfunga Rage, ukija na Papa Aziz sijui Nyangumi Aziz? Weka na Saidi Nkumba.

Ngoja nikuambie juu ya Saidi Nkumba, mbunge wa Sikonge. In fact jamaa ni FISI sana. Bungeni siku zote husubiri wengine wauwe mnyama na yeye aje tu kuongeza "....Ni kweli jamani, hii haiwezi kuwa..." Sanasana yeye HUTAKA KUJUA....... Ila kali zaidi ngoja nikuambie. Nilipata habari kuwa hata akija pale Bungeni Dodoma na mchuma wake na kwa sababu ana nidhamu ya WOGA, jamaa huwa wa kwanza. Akifika pale basi parking ya magari huwa nyeupeee, hivyo badala ya kuweka gari lake mbele kabisa, basi FISI yule huenda MBAAALIII kabisa kama siyo mwishoni na kuweka mchuma wake kule. Kisa ni kwamba, HATAKI KUZIBA NAFASI ZA AKINA MWAKYEMBE. Hili jamaa lilikuwa linashinda kwa sababu tu baba yake alikuwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Tabora. Ila sasa hivi hayupo tena na nina imani mwakani KWISHIENI.

Duuu, mzee, eti Viongozi wa Tabora, hahaa haaaaaa hahaaa. Yaani umenifanya niwe na furaha badala ya majozi. Sijui nihamie tu Kyela? Ila tu sijui toto za Kyela zikoje. Wanyamwezi unajuwa tena, toto zenye rangi nyeupe nyeupe (kama Warangi vile/Wambulu) twalipa ng'ombe wengi.

Ngoja nicheke zaidi, eti viongozi wa Tabora, Haaa haaa!!!!!!!!
 
Mkuu Shalom.
Kajitahidi kafanya nini?.Kawafanyia nini wanachi waliomchagua?
Kuandikwa na magazeti ya mengi ndiyo kujitahidi?.

Ameshindwa kuunganisha nguvu ya wanachi na kufanya kazi nao pamoja.
Ofisi yake muda wote imefungwa na yeye yuko dar kula kuku.

Samwel, nimesoma post zako nyingi na ni za kusikitisha.They are narrow minded and mediocre.
Dr Mwakyembe has come to prominence , nationally, kwa kuwaumbua mafisadi kwa ufanisi na kwa muda mfupi kuliko hata ilivoweza kufanya PCCB.
Hivi Nyere rekwa muda wake wa miaka karibu 24 madarakani aliwafanyia nini watu wa Musoma na Butiama?
Upuuzi wa kimawazo kama huu usiruhusiwe kwenye fikra za watu waliozoea kupewa "kitu" mkononi na mafisadi ili waone kuna kitu cha maana kimefanyika.
Lazima tuwe broad minded.
 
Sikonge na connection za Kyela...........I like that
 
Sikonge na connection za Kyela...........I like that

Kyela ni ndugu zetu katika mengi. Sisi wote ndiyo member wakubwa wa kanisa la Moravian. Hata ukiwa Dar es Salaam, baada ya misa utasikia tu Kinyakyusa na Kinyamwezi. Pia sisi ni jirani na watani.

Mie ni Mtanzania hasa. Maadamu timu yetu ya Taifa haifanyi vizuri basi hushabikia Brazil. Sasa maadamu kwetu watu wamelala, naona heri nishabikie Tarime, Kyela, Buswanda nk ambako labda watu wangu wataanza kupata mwanga wa jinsi wenzao wanafanya.

Sasa hivi kuna vimipango vinafanywa na VINARA au niseme CREAM ya watu wanaotokea Sikonge. Ila nafikiri itakuwa wanasubiri kwanza Mbunge yule Mzembe aondolewe na nasikia kashajenga tayari nyumba yake Mole (ni shamba huko wala huwezi amini) na acha aende akalime tumbaku. Hivyo, Sikonge ikianza kuamka, Kyela hamnioni..... 🙂
 
Samwel, nimesoma post zako nyingi na ni za kusikitisha.They are narrow minded and mediocre.
Dr Mwakyembe has come to prominence , nationally, kwa kuwaumbua mafisadi kwa ufanisi na kwa muda mfupi kuliko hata ilivoweza kufanya PCCB.
Hivi Nyere rekwa muda wake wa miaka karibu 24 madarakani aliwafanyia nini watu wa Musoma na Butiama?
Upuuzi wa kimawazo kama huu usiruhusiwe kwenye fikra za watu waliozoea kupewa "kitu" mkononi na mafisadi ili waone kuna kitu cha maana kimefanyika.
Lazima tuwe broad minded.


Mkuu Lole Gwakisa.
Naona wewe umechoka sana

Nyerere aliwahi kuwa mbunge musoma?.Mwambie Mwakyembe agombee urais ili kupunguza lawama jimboni kwake.
 
..siyo kweli kwamba Nyerere hakusaidia kabisa kwao.

..kuna makala iliyoandikwa na Manyerere Jackton ikielezea jinsi Butiama ilivyokuwa na hali nzuri wakati wa utawala wa Baba wa Taifa.

..pia kuna msaada wa dola laki 4[sina uhakika] toka kwa Gaddafi kwenda kwa Waislamu wa Butiama ambao ulitokana na urafiki wake na Baba wa Taifa.

..pia kulikuwa na kiwanda cha nguo Musoma.

NB:

..kuna dhana kwamba kiongozi bora ni yule anayesahau kwao. naamini dhana hiyo ni potofu.

..wengine tunafikia mpaka kuwasifia Mawaziri ambao ni wabunge kwa kutoyaendeleza majimbo yao.
 
Mkuu Lole Gwakisa.
Naona wewe umechoka sana

Nyerere aliwahi kuwa mbunge musoma?.Mwambie Mwakyembe agombee urais ili kupunguza lawama jimboni kwake.

Hivi kuongelea mambo ya kitaifa mbunge haruhusiwi mpaka kwao kukae sawa!
Kama ndivyo basi kuna kaazi kweli kweli kwa hii myopic view!
 
Samwel,
Mkuu wangu unajua hadi sasa hivi hujaandika kitu ambacho mimi naweza kusema kina hitilafu kubwa kwa kiongozi huyu..
Kugawa watu ni jambo ambalo hata mimi ningelifanya kama nafahamu kuna mbinu za kuoniondoa kutokana na msimamo wangu kwa Mafisadi..Siwezi kusubiri hatma ya yote haya wakati Mafisadi wanajijenga kuniondoa. Hivyo aidha upo nami au upo na Mafisadi.
Kama wewe unampinga Mwakyembe nje ya maswala ya Ufisadi basi kwa nini usitumie vigezo vingine nje ya haya ya Mafisadi ikiwa ni pamoja na yaliyotokea..Mwakyembe ni mbunge pekee ambaye sasa hivi tunamzungumzia kuhusiana na uchaguzi wa mwaka 2010..Hii inanipa mimi wasiwasi hasa pale mnapotumia vigezo vya kujiona msomi na kugawa watu.

Nitasema hivi viongozi wote wasomi Tanzania hasa wale ambao hawakuwa wanasiasa ila wamevamia fani hii wana tabia hizo..Ni tabia mbovu sana ya viongozi wengi sana Tanzania toka serikalini hadi ktk mashirika kwani NDIVYO TULIVYO na Mwakyembe hana tofauti yoyote.

Mimi nitapenda sana kuona mtu akijimwaga kugombea dhidi ya Mwakyembe kwa nia njema kwa wananchi na sio kutumia mifano ya Rostam na magazeti yanayomponda. Na itakuwa rehema kubwa kama mtu huyo atatoka hapa Kijiweni kwa sababu nadhani imefikia wakati mazungumzo yetu yaingie hatua nyingine.

Mwakyembe ni mfuasi mkubwa wa Kikwete na watu mmechoka na Uvasco..hivyo nafasi kama hii msiiachie, ni wakati wa mashambulizi ya kifikra nasi tutakuwa nyuma yenu ili kesho tupate huhadithia.. Binafsi nipo Chadema na nitasema tena kwamba simkubali Mwakyembe kwa sababu he is on the otherside..Na simkubali Kikwete kwa sababu hiyo hiyo kwani CCM kwangu mimi ni punda aliyechoka! Kinyume cha hapo hawa jamaa ni good people.. I will vote for them anytime kama watakuwa upande wangu.

Na umenishtua sana uliposema unajua fika kwamba Mafisadi wanajiandaa kumwangusha kwa mbinu mbili ambazo wewe unazijua!..Hapa mkuu wangu, unanifanya nigune kidogo..Unayajua ya Mafisadi!..kisha unataka mkuu huyu akae kimya tuu hadi mwakani!..

Na ilikuwaje mbona alipofika Kyela alipokewa kwa dshangwe na kuitwa shujaa isipokuwa baadhi viongozi wa jimbo hilo ndio hawakufurahia!..something is very wrong na nitashukuru sana kama utatumwagia dataz zinazomhusu Mwakyembe kama Mbunge wa Kyela na mapungufu yake..Kuligawa kanisa lako haina maana yoyote zaidi ya kutuambia kwamba wapo watu kanisani wanaompiga vita..
Sasa ikiwa kanisa linatumia mwanasiasa kugawanyika ina maana kanisa hilo lina mapungufu yan viongozi wake na pengine sii sehemu ya Ibada isipokuwa Siasa..Ndio haya yaliyomkuta Ustadhi mwinyi akapigwa kibao na mtoto ndogo kwa sababu sehemu ya ibada ni ibada na kama Mwakyembe analeta siasa kanisani na kuna watu wanamsikiliza basi hilo kanisa lina matatizo!.. Utanisamehe lakini, ni mawazo yangu kukutaarifu kuwa msikubali mwanasiasa kulitumia Kanisa kujineemesha, hiyo ni sehemu ya YESU - mpe la Kerbu! unless nyie wote mnalitumia kanisa hilo kisiasa.
 
Mkandala,

Naona umeadika Samwel ila umechukua maneno yake na yangu.

Ni mie nilisema kuwa nazifahamu kesi mbili/tatu tayari ambazo nina imani Mafisadi mwakani WANAWEZA kuzitumia kummaliza Mwakyembe. Nimeandika kabisa hizo kesi zote mbili na sikuzificha. Kesi ya kwanza aliiandika kwa kurashia FMes hapahapa JF na kama sikosei iko kwenye hii thread. Ukitaka zaidi waweza kumuuliza. Kesi ya pili inafanana sana na hiyo, sema ya kwanza ilifanyika Dar na ya pili imekuja kujianika bila kukusudia kwenye mazishi ya mama yake.
Kesi ya tatu hiyo hata wewe unaifahamu na siyo siri ingawa mie niseme nilikuja kuipata humuhumu ndani na hiyo ni wakati wa Uchaguzi Zenji (Utawala wa Mkapa). Sijawahi ifahamu vizuri ila ina uhusiano na kipigo kilichotembea Zenji.

Sasa si unaona zote tunaziweka hapa ili kumpa muda ajiandae? Kama tungelikuwa hatumpendi unavyofikiri, tungelikaa kimya. Nimesema tangu mwanzo kuwa Mwakyembe ana uwezo mkubwa ila anajiharibia mwenyewe.

Mkandala, tatizo la Mwakyembe anataka kujifanya Rostam wa Kyela. Yaani lazima uwe na yeye tu na akisikia ulienda kwenye party kwa Mwakipesile (Boiler la kutupwa) basi siku hiyohiyo unakuwa mbaya wake. Analazimisha uwe na marafiki anaotaka na uhusiano na watu wale tu unataka. Ukifanya kivyako basi kwishieni. Ni sawa aje hapa akute mmekubaliana na Zitto juu ya jambo fulani basi hapohapo urafiki kwisha. Anakuwa kama Mwanaume mwenye wivu. Kila akiona mke wake kasimama na mwanaume basi ugomvi. Namhurumia huyo mwenyekiti wa CCM aliyemfanya mali yake na jamaa hajui hata afanye nini maana anaendeshwa na Mbunge na huku sheria/katiba ya CCM inamdai afanye vile. Nafikiri binadamu ili uishi na wengine lazima ujifunze kuwaamini. Vinginevyo, nenda kashike chaki.

Juu ya MAFISADI kama watataka kummaliza, nina imani wanazo kali zaidi ya hizi tunazozifahamu sisi hapa. Si uliona kwenye swala la umeme, walimtekenya kidogo na akaanza kuhaha kila sehemu?

Juu ya kupaka watu, juzi kampaka kijana mmoja aliyeko UK kuwa analeta mambo jambo. Na kibaya zaidi, imetoka kwenye geazeti la MAJIRA ukurasa wa mbele wakat jamaa yuko busy na Mabox yake UK, huku analimwa eti anataka kugombea. Haya magazeti nayo sijui yakoje, habari ya MBEBA mabox mnaiweka ukurasa wa mbele, kisa makala ya Mwakyembe? Na kwa ufupi ni kuwa alishaanza muandama jamaa siku nyingi sana. Na amekuwa akija hapa kwa kutumia jina la LAZARUS MTINDI (Soma nyuma jumbe zake - Ninaamini kwa asilimia 90 kuwa ni yeye). Ila jamaa wa UK naona mwisho atafikia sasa achoke na aamuwe kwenda kugombea. Akishaamua kufanya hivyo basi usiwe na wasiwasi, NITAKUJULISHENI <> kama ninataka kwenda kugombea (heeee Sikonge...🙂

Hizo sababu mbili kwa kweli zimekaa vibaya sana. Itabidi kumtafuta Dr. mzuri sana wa Plactic Sugery ili kuondoa hayo makovu aliyojiwekea. Mwakyembe alimtoa Mwakipesile kwa kumtolea uvivu na madudu kibao na moja wapo likiwa hilo la kugawa watu. Yeye anafanya hayohayo.
Anyway, madudu mengine sintayaweka kwa hisani ya ndugu zangu wa Kyela. Ila siku ikifika basi nitayaanika. Ila lazima ujuwe kuwa kama kuna sehemu mwakani uchaguzi utakuwa katika hadhi ya KIMATAIFA, basi Kyela utakuwa namba 1. Hapa hatuongelei pesa ila mbinu za kivita. Watu watakaa chini na kuchora Algorithm ya kushinda.
 
Sikonge,
Mkuu shukran sana na namwomba radhi sana ndugu Samwel kwa kuchanganya majina.. unajua tena uzee huu jamani kuna siku ntakuja changanya jina la mke na hawala hadharani..Lol!
Mkuu wangu nataka kufahamu kitu kimoja, hivi huyu Mwakyembe amekuwa akisema haya ktk gazeti la taifa - Majira, kuhusiana na kijana huyu wa UK kuhusiana na gani?..Uchaguzi wa mwaka 2010 huko Kyela!.. naomba dondoo za yale yaliyotangulia. Kisha huyu Lazarus Mtindi akiwa ni Mwakyembe huoni kama unavunja sheria na utaratibu wa kijiwe hiki!.. na imetokana na kitu gani haswa ukamtaja wakati wapo wengi tu hujmu wanatumia majina bandia..Kweli unayafanya haya kwa mapenzi!

Mkuu wangu usiseme unampenda au kumchukia Mwakyembe, hapana hakuna mtu anasema humpendi isipokuwa naiona chuki..Unamchukia Mwakyembe kwa visa alivyofanya kwani chuki hutanguliwa na Upendo..siwezi sema humpendi kwa sababu sii lazima kutompenda mtu kukaambatana na chuki.. unaweza kutompenda mtu na usimchukie na unaweza pia kumpenda mtu ukawa na chuki naye hii yote inatokana na kutopendezewa na vitu fulani..

Mimi nataka sana mtu asimame kwa hoja na Mwakyembe.. Hizi habari za mwakyembe kasema hivi kafanya hivi na vile ni mambo ya jikoni, watu wanasubiri mpunga mezani. Hivyo unapomweka Mwakyembe na Mafisadi nitamchagua Mwakyembe..Mwakyembe na Mwakipesile nitaenndoka na kijana wangu Mwakyembe.. Mwakyembe na Ukuta nitaendelea kumchagua Mwakyembe kwa sababu he is the only MP mwanamme from CCM ameweza kusimama dhidi ya Mafisadi hata Mh. Kikwete mwenye kofia kashindwa..
Hayo maswala ya Mafisadi kumbana kuhusiana na Umeme hainipi shida kabisa mimi kwa sababu natazama nje ya sanduku..Na kama sisi Watanzania wote tungefikiria kama navyofikiria mimi basi Kikwete angeweza kuwasimamisha kina Lowassa na Rostam kizimbani kwa sababu Kikwete ni mhusika pia ktk baadhi ya maswala he is not clean... No one is Clean Tanzania, hivyo ni lazima watasema mabaya ya Kikwete kumhusisha na Ufisadi..ambao wao kama viongozi wameshindwa kusema siku zote ila siku watakapo shtakiwa wao. Na kwa ujinga wetu mtu kaiba benki na kufikishwa mahakamani tunamhukumu mshtaka kuwa hata yeye kisha wahi kuiba NSSF hivyo hatuna kesi ya wizi wa benki!..ONLY in Tanzania.
Ndio hayo ya Rostam na mradi wa Umeme Singida.. I mean huyu mtu alikuwa mweka Hazina wa chama CCM, mjumbe wakamati zote zenye nguvu ndani ya chama, akaingizwa Miundombinu asiyaseme yote haya ya Ufisadi wa Mwakyembe hadi siku alipokataliwa na kuhusishwa yeye na Dowans..Na asivyokuwa na aibu akatumia report ya Mwakyembe ati jina lake halikutajwa!.. kweli hawa Mafisadi wamejiandaa kweli au wanataka kucheza mchezo mchafu tu.

Je, kama Mwakayembe asingekuwa ktk kamati ile ya rais na ya Bunge ina maana tusingejua lolote kuhusiana na Mwakyembe!..Besides, inatakiwa ujasiri mkubwa sana kuwataja kina Rostam na Lowassa kuhusika na Richmond/Dowans wakati unafahamu lako linakuja!.. viongozi wachache sana wanaweza kusimama na naweza sema ni Dr. Slaa peke yake kafanya hivyo...
Kwa hiyo mimi namwomba sana huyo kijana wa UK asimame, agombee Kyela ili wananchi wapate kuona ushindani wa haki. Kumlaumu Mwakyembe kwa hili ama lile wakati hana mshindani ni kutafuta mchawi tu. Vijembe na visasi ni vitu ambavyo vinatakiwa kufika uwanjani kama ushabiki wa mpira..ingieni ktk chaguzi zetu na mchango kama huo tawasaidia sana wana Kyela..
 
duh; kwa hiyo hakuna cha ajali wala nini! na kuna watu wanasema imetangazwa itv!
 
Mkandara,

Naona tuko pamoja kabisa. Ila labda mie nakuja na msimamo wa kusema "Kumdekeza mtu ni kumlemaza.." Nimesema tena na tena, uwezo wa Mwakyembe ni Mkubwa sana na anaweza kufanya maajabu. Ilitosha tu kuunganisha watu na afanye vitu vyake bila ya kujali mambo mengine. Yeye yuko busy na kutafuta nani anamhujumu kiasi kwamba amekuwa too sensitive na kila mtu anayeonekana na wapinzani wake.

Mkandara, kwako wewe unaweza kuona jambo dogo ila kwa Kyela imeanza kuwa kero. Ukisikia hadi watu wamepigana si jambo dogo. Ukisikia watu wanasimama na kuanza kumwambia moja kwa moja yale ambayo tumekuwa tukisema hapa kuwa Mwakyembe usigawe watu, ujuwe kuwa watu wamechoka. Matatizo ya Mwakyembe (kama nikifumbia aliyoyafanya zamani) ni kidogo sana na anaweza kujibadili. Tatizo ni mtu ambaye akitekenywa kidogo tu basi huanza kukosa mwelekeo kwa kusema kupita anayotakiwa kusema. Sasa hivi jamaa kwa kumuudhi, wanamwambia kijana wa UK anakuja kugombea. Kijana wa UK tulishamwambia tangu zamani sana agombee lakini amekuwa akikataa. Mwaka 2005 kila mtu alijua sasa muda muafaka, bado akakataa. Yeye na ndugu zake/jamaa zake wakawa nyuma ya Mwakyembe. Yeye na Mwakyembe wanafahamiana sana tu. Ila aliposhinda, akawafanya maadui zake namba moja. Kuna yule kijana mfanya biashara, alimsaidia sana Dr. kwenye uchaguzi ila kama mfanya biashara, lazima ajuwe kuishi na Vigogo. Aliposikia Mwakipesile kawa mkuuwa mkoa, akaenda kumpa HONGERA. Kitendo hiki kilimuudhi sana Dr. Kumbuka kuwa kijana wa UK alimwambia mara aliposhinda kuwa "dr nenda kapatane na Mwakipesile...." Majibu aliyotoa yanasikitisha, na kibaya zaidi muda haujapita jamaa kawa mkuu wa mkoa. Hapa hatuongelei UFISADI. Hapa hatuongeleo uchapa kazi wa Dr. Tunachosema ni kuwa MWAKYEMBE, MWAKA 2005 ULIUNGANISHA watu kibao, nini kimetokea hadi jamaa wawe maadui zako?

Mwisho ni kuwa, pamoja na mapungufu yake hayo, i wish angelikuwa Mbunge wa Sikonge maana huku kwetu, duuu. Nitaendelea KUMHUKUMU Mwakyembe kwa sababu moja kubwa sana nayo ni kuwa "Naelewa Dr anauwezo wa kupanda Mount Everest, sasa mtu asije niambia kuwa akipanda mlima wa Uruguru kwa shida, tumpe HONGERA wakati naelewa uwezo wake ni zaidi ya huo..." Mwakyembe, you can do better than that. Acha kutafuta conflict na watu wote. Chapa kazi, weka imani kwa wengine, rudisha kundi lako uliloshinda nalo uchaguzi mwaka 2005 na mwisho, nenda kwa Mwakipesile hata kama kwa kupitia kwa Mchungaji/Askofu na malizeni tofauti zenu. Siku zote watu wanashinda vita kwa kutumia kichwa na si MAGUVU.

{NYONGEZA: nakuombea afya njema kwa ajali iliyokupata.}
 
Mods kuna uwezekano wa kuunga hii na ile ya mrema apata ajali?
 
Back
Top Bottom