Asante Mzee wa Busara!
Nimeumia sana kusoma thread hii hasa kwenye maoni ya kina Chris
wanaodhihaki msiba!
Wanaomfahamu Grace wanajua wazi alivyokuwa huru katika mawazo na
matendo. Hakumfuata kaka yake tu kwa sababu yeye ni kaka, alichoangalia
ni ile imani yake, na ilipobidi aende upande wa pili alifanya hivyo bila
kufikiria undugu na haikuwa uhasama.
Ni Grace, Graduate wa kwanza wa kozi ya Building Economics (quantity
Surveying) ya kilichokuwa Ardhi Institute sasa Ardhi University. Yeye ni
kati ya graduate wetu wa kwanza katika Chuo cha kitanzania katika fani
ya kukadiria gharama za ujenzi mwaka 1981. Amefanya mengi sio tu kwa
mashule, makanisa na jamii bali pia kwa sekta rasmi ya uma na ya
binafsi.
Mungu ailaze raha ya Grace mahali pema peponi!