Msanii, Chino na kundi lake wapata ajali Kabuku, mmoja afariki Dunia

paul miteda

Senior Member
Jan 19, 2023
129
584
Ajali mbaya wamepata CHINO KID na group lake wakiwa wanaelekea Moshi kwenye show jioni ya leo mungu awasaidie wawe salama.
---
Msanii na Dancer, Chino, amepata ajali akiwa na wenzake safarini kuelekea kwenye show Mkoani Tanga ambapo gari alilokuwa amepanda na baadhi ya Madancer wake (Alphad nyeusi), limegongana na lori la mafuta.

Ajali hiyo imetokea mapema leo maeneo ya Kabuku ambapo Meneja wa Msanii huyo aitwaye Sweder ambaye alikuwa gari la nyuma lililokuwa likiongozana nao amesema “Tulikuwa tunaelekea Tanga katika show ya Mama yetu Ummy Mwalimu, ajali tumeipatia maeneo ya Kabuku, tuliondoka na gari mbili, gari alilokuwa amepanda Msanii lilikuwa imetangulia na Msanii alikuwa amekaa upande wa kushoto wa Dereva”
rrrr.JPG
“Gari alilopanda Msanii lilipamiwa na lori la mafuta, tuliweza kupata msaada wa haraka tukafika Hospitali ya Rufaa ya Tanga, alikuja Mama yetu Ummy kutupa sapoti alipofika alituonesha ushirikiano mzuri sana, hakuna aliyefariki, tunamshukuru Mungu, simu ya Msanii ninayo Mimi bado hajapewa ruhusa ya kutumia simu.

“Wote waliopanda kwenye hilo gari wameumia, walioumia zaidi wapo wanne, wengine wanatakiwa kufanya operesheni wameumia zaidi maeneo ya mguu wengine wamevunjika mguu, Dereva amepata mshtuko kwenye kichwa, wengine wamepata shida kwenye taya.”

UPDATE
Mwanafamilia wa kundi hilo anayefahamika kwa jina la Nabeel ambaye alikuwa ni dereva wa gari iliyopata ajali siku ya jana lililowabeba kina Chino Kidd amefariki siku ya leo.
IMG_9049.jpeg

Majeruhi wa ajali hiyo wamehamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu.
 
Mungu awasaidie gari hata plate namba bado imekula mzinga mungu awaponye
20231111_220213.jpg
 
Hivi kwann wasanni wengi wakiwa either wanaenda Tanga au wanatoka Tanga huwa wanapata ajali?

Poleni sana.
 
Hivi kwann wasanni wengi wakiwa either wanaenda Tanga au wanatoka Tanga huwa wanapata ajali?

Poleni sana.
Ile njia mkuu inataka umakini sana, sasa tena si unajua mambo ya vijana na alphard bado pwiru ukikanyaga hii hapa inaitika na zilikuwa mbili zikiongozana ndio basi tena kaka....kikubwa wapo salama maisha lazima yaendelee.

Mungu amfanyie wepesi Chino na kundi lake.
 
Back
Top Bottom