DODOMA: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa afariki dunia baada ya gari lake kuangukiwa na lori la mafuta

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
DODOMA: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa Mhandisi Ngusa Izengo afariki dunia baada ya gari lake kuangukiwa na lori la mafuta

========

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kongwa, Izengo Ngusa, amefariki asubuhi ya leo Aprili 15 kwenye ajali ya gari,

Taarifa zilizotufikia zinasema gari dogo alilopanda Mkurugenzi huyo, lenye namba za usajili T619 DMA aina ya Toyota Crown Athlete, liliangukiwa na lori lililobeba mafuta,

Ajali hiyo imetokea eneo la Mbande Makaravati mkoani Dodoma. Taarifa zilizotufikia zinasema Lori lililobeba mafuta limeiangukia gari ndogo na kuuwa wote walio kuwa kwenye gari hilo.


ded2.jpeg


DED.jpeg


>>>>>Updates
Juhudi za kulinyanyua lori zinaendelea ambapo gari ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Mhandisi Ngusa Izengo lilipata ajali ya kuangukiwa na lori hilo jana usiku huko eneo la Mbande, wilayani Kongwa Mkoani Dodoma

Juhudi.jpeg

Dereva atolewa vipande vipande
MWILI wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Izengo Ngussa ambaye alifariki dunia baada ya gari lake kugongana na lori la mafuta katika eneo la Mbande Makaravati wilayani humo juzi,....

...Jana ulilazimika kubebwa pamoja na kipande cha gari lake kwa ajili ya kwenda kutolewa na Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), kutokana na kung’ang’ania kwenye bodi.

Ajali hiyo ilitokea juzi majira ya usiku ambapo Mkurugenzi huyo alikuwa kwenye gari dogo akitokea Dodoma Mjini.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika cha habari, mwili wake ulikuwa umeungana na bodi ya gari lake na kushindwa kutolewa katika eneo la tukio.

Gari hilo aina ya Toyota Brevis lenye namba T619 DMA lilikandamizwa na lori la mafuta baada ya kulaliwa.

Chanzo hicho kilidai kuwa tangu jana majira ya asubuhi shughuli za utoaji mwili huo zilianza lakini zilishindwa kuzaa matunda kutokana mwili huo kung’ang’ania katika bodi hilo.

Kilisema kuwa majira ya saa nane mchana kipande cha gari kilibebwa katika gari la jeshi na kupelekwa katika ofisi za Temesa Dodoma ili bodi la gari liweze kutanuliwa na kutolewa mwili huo.

Mwili huo baadaye ulihifadhiwa katika Chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufani ya Dodoma.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi alithibitisha kutokea kwa ajili hiyo katika eneo hilo na kusema imehusisha magari mawili likiwemo la Mkurugenzi huyo.

“Ajali ilitokea usiku sana (na) taarifa zilianza kuzagaa alfajiri na alikuwa akitokea njia ya Dodoma mjini kuelekea Kongwa... alikuwa katika eneo lake la kazi,” alisema.

Alieleza kuwa kutokana na uhalisia wa tukio hilo walipata wakati mgumu kutoa wa mwili wake.

“Kutokana na nature (asili) ya ajali yenyewe lazima ugumu uwepo na tumehakikisha tumeutoa mwili salama baada ya kutanuliwa bodi la gari na lengo letu lilikuwa tuweze kuutoa mwili wa mwenzetu katika hali nzuri,” alisema.

Alisema vikosi vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Jeshi la Wananchi (JWTZ) vilifanya kazi kubwa katika zoezi la uopoaji.

Hata hivyo alisema mazingira ya ajali na chanzo taarifa yake itatolewa na Jeshi la Polisi kwa kuwa wanaendelea na uchunguzi.

Alisema amefanya kazi miaka miwili na Mkurugenzi huyo na alikuwa mwadilifu na ameisaidia wilaya hiyo kupata hati safi katika ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).

Naye, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk. Caroline Damian alithibitisha kupokea mwili wa Mkurugenzi huyo na kwamba umeumia sana katika maeneo ya kichwani.

Aidha alisema amevunjika mkono na mguu mmoja wa kushoto.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, White Zuberi alisema wilaya hiyo imepata pigo kwa kuwa aliwezesha kupiga hatua kimaendeleo na alikuwa na mchango mkubwa.

Kadhalika, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino, Athuman Masasi alisema kifo hicho kimempa maumivu makali kwa kuwa alikuwa anafanya kazi naye vizuri na kutokana na marehemu kuwa Mhandisi hivyo alikuwa akiwashauri mambo mbalimbali ya kiuhandisi.
 
RIP .....mbona mpiga picha kama umepiga picha kwa uwoga uwoga hivi ....kulikoni
 
Back
Top Bottom