Godbless Lema avuliwa ubunge

Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
nimepitia threads nyingi na sehemu nyingi ili kuona mawazo ya wanachadema na viongozi wao. nilichoona ni kuwa hawaaamini kama mahakama imetenda haki. bali si hilo tu wamediriki kuhisi kuwa ati mahakama imeamuriwa na ikulu kufikia maamuzi yaliofikiwa


nimesikitishwa sana na watu ambao siku zote hujihesabu makini kwa kauli zao za kuhusisha Ikulu na mahakama katika maamuzi.

inawezekana hukumu haikuwa tamu kwao, na wanahisi hawajatendewa haki, na ndio maana kwenye sheria kukawa na haki ya kukata rufaa ili kuhakikisha haki inatendeka. kwa hio ndugu zangu wa chadema kama mnahisi haki haijatendeka fateni taratibu za kisheria kudai haki zenu badala ya kuhubiri chuki na uongo


ndani ya chadema mna wanasheria wengi tu, watumieni ktk kuhakikisha haki inatendeka. na si kuwa nyny mkishinda tu haki imetendeka mkishindwa haki haijatendeka huko ni kutokuwa watu wa haki.

Well said!
 
Wapi Zitto,
Wapi Mnyika,
Wapi Dr Slaa,
Wapi Ephata Nanyaro...changamkieni senti hizo...Haba na haba!
 
Chadema siku wakichukuwa nchi mahakama zote zitakuwa chini ya Chadema...hukumu ipo wazi kweli Lema alikuwa anatoa kauli za kashfa kwenye mikutano yake 8 kati ya 60 aliyofanya.

...ambayo si tume ya uchaguzi wa msajili wa vyama walioona hayo, ila watu 3!
 
Ndugu zangu,


Kuna kila dalili, kuwa tunakokwenda ni kubaya. Tumefika mahala sasa, kuwa kwenye siasa tunaingiza hulka za ushabiki wa Simba na Yanga. Hii ni hatari kwa taifa.


Jana alhamisi, kabla ya jua la saa sita mchana, habari zililipuka na kusambaa kote nchini; Mahakama imemvua Ubunge Godbless Lema.


Ni ukweli, Godbless Lema ni mbunge kijana na maarufu sana hapa nchini. Lakini, imefika wakati Watanzania tukubali na tuamini, kuwa Mahakama inafanya kazi kama mhimili huru wa dola hata kama kunahitajika, kupitia Katiba mpya ijayo, kuboresha mhimili huo ili uaminike zaidi.


Ni kwa mantiki hiyo, kuwa mahakama ni mhimili huru wa dola, tumeshuhudia hata Serikali ikifikishwa Mahakamani na hata kushindwa kesi. Tumeshuhudia , katika historia ya nchi hii, Wabunge wa CCM , bila kujali majina na umaarufu wao wakifikishwa mahakamani na kushindwa kesi.


Kwa Godbless Lema, kutoa hadharani madai kuwa Rais wa nchi anahusika na hukumu yake ni kauli ya bahati mbaya sana anayopaswa yeye mwenyewe Lema, na chama chake, kuacha kuendelea kuitoa, haina mantiki. Inaidhalilisha Mahakama. Ni kauli iliyotolewa kwa haraka na isiyo na tija kwa taifa.


Tukubali kwa sasa, kuwa kule Arusha hukumu imeshatolewa. Kuna fursa pia ya kukata rufaa ya hukumu hiyo kwenye Mahakama iliyo juu zaidi. Hakika, kwa Godbless Lema na chama chake, huu ni wakati kutafakari hukumu hiyo na kuona ni namna gani ya kwenda mbele kisheria au kisiasa.


Haiwezekani kwa sasa kudai kuwa CCM inahusika na hukumu hiyo. Wakati kimsingi CCM imepata 'hasara nyingine ya kisiasa' kwa matokeo ya hukumu hiyo. Kwa anayechambua kwa undani sana, hukumu ya Lema ya kuvuliwa ubunge imekuja katika wakati mbaya sana kwa chama tawala, CCM.


Ni hukumu inayomtangaza na kumwongezea umaarufu Godbless Lema na chama chake cha Chadema. Leo, bila kufuatilia mwenendo wa kesi husika, kuna wanao-sympathy na Godbless Lema na Chadema, wakiamini CCM imetumia Mahakama kumhujumu Godbless Lema na Chadema. Na kama Lema atasimama tena kuwania kiti hicho, basi, yumkini kura zake zitaongezeka maradufu. Lema ana hakika ya kura nyingi pia za ' kuonewa huruma'.


Na ukweli mwingine ni huu, katika nchi yetu kwa sasa kuna kundi jipya la wapiga kura. Hawa naweza kuwaita " Wapiga kura dhidi ya hali iliyopo"- Aina hii ya wapiga kura inaundwa kwa idadi kubwa na waliokuwa wapiga kura wa CCM katika chaguzi za miaka ya nyuma na ambao sasa hawaridhiki na hali iliyopo ndani na nje ya chama chao.


Ndio, hawa ndio waliokuwa wapiga kura wa CCM na ambao sasa wanawachanganya sana CCM. Ndio hawa waliompigia kura Nassari Arumeru, ndio hawa waliowahakikishia viti vya udiwani Chadema kule Ruvuma, Mwanza na Mbeya.

Maana, ni wapiga kura wa kundi hili unaoweza kuwaona wakijaa kwenye mikutano ya kampeni za CCM, lakini, kwa vile hawapati majibu ya maswali yao ya namna gani CCM na Serikali yake, si tu itakavyorekebisha, bali inavyorekebisha sasa ' Hali iliyopo', basi, siku ya kupiga kura wanatumbukiza kura zao kwa wapinzani.


Ndio, ni ukweli pia , kuwa ' Ndani ya nyumba ya CCM' kwa sasa hakuna amani na utulivu. Makundi na mbio za kuelekea kwenye Urais 2015 zinawaacha wana-CCM wakivurugana wenyewe kwa wenyewe.


Focus sasa haiko kwenye kutekeleza ahadi lukuki walizowaahidi wapiga kura kwenye kampeni zilizopita. Kwa sasa kuna wenye kufikiria hatma zao za uongozi. Kuna waliojikita kwenye mnyukano wa kimakundi kwenye vita ya kuelekea Urais wa 2015. CCM ya sasa inaonekana kuwa mbali na wananchi na kero zao zinazowakabili. CCM ya sasa imeacha kuwa ' Kimbilio la Wanyonge' kama wakati mmoja alivyopata kukiri Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa. CCM ya sasa ni kimbilio la ' wenye nacho' wakiwamo wafanyabiashara.


Ndio, CCM imeanza kulipa gharama ya wananchi kutoridhika na ' Hali iliyopo'.


Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
 
Mwenzako Nape anasema hivi

NAAMINI MUNGU KAAMUA KURUDISHA AMANI YA MJI WA ARUSHA ILI SHUGHULI ZINGINE ZIENDELEE NA WATALII WAJE KWA AMANI, AJIRA ZIONGEZEKE, UCHUMI WA ARUSHA UKUE....
 
aisee wamlete tumpige frustration nyingine Lowasa.
Makalio ya sufuria hayaogopi moto, mahakama imeepua sufuria, sasa wapiga kura tunabandika the same sufuria.
Piga kura, linda kura ndo formula ya mchezo.
 
Tafsiri yako ina tafsiri inayoibua taswira nyingine kwenye ulingo wa siasa za Tanzania.
Kwasasa tusubiri tamko la chama kesho, tujue nini wamekijadili na wanasheria.
Je, ni Comrade Lema atasimama tena?
Je, Interpretation ya kile kifungu kilichotumika kumuengua inamruhusu kugombea bila kipingamizi?

Macho na masikio kwa wataalam wa sheria.
 
Mjengwa huna ya kumlaumu Lema kwa kuituhumu Ikulu kuhusika na kuhumu ile. Alikuwa yupo sahihi kabisa kwa sababu,

1.0 Nape aliwahi kusema kuwa kesi hii Lema lazima imtie kidole!!!!! Halafu tunakuja kupiga kambi ili kuchukua jimbo letu. Kauli ile ilimfanya aitwe mahakamani atoe maelezo na kukana kutoa kauli hiyo.
Hii inamananisha Nape alishajua nini kinaendelea, hivyo ni wazi Lema akimtuhumu Ikulu kuhusika na kesi ile.

2.0 Kimsingi madai ya kesi ya Lema yalikuwa madogo sana n hukumu yake inanoekana kutoendana na madai ya kesi. Swali la kujiuliza inakuwaje? Bila ya shaka kun exteral force.

Yote kwa yote kama kulikuwa na mchezo mchafu basi umefanyika katika bad timing na hivyo kuiweka CCM katika wakati mgumu kuwahi kujiri katika historia yake. Ni kama kuhumu hiyo inawafanya CCM KUCHAMBIA MAJI YA MOTO.
 
Nimepokea sms toka kwa jamaa yangu wa karibu ambaye ni kada mkubwa wa magamba kanidokeza kuwa kuna tetesi chama kimejipanga kumrejesha mgombea mwanamke na chapuo linamwendea Mbunge wa Viti maalumu Ndugu, Dada yetu Nameloki Sokoine. wadau mwasemaje? je huyu dada katolewa kafara ama magamba wanategemea kutumia historia ya baba ya binti huyu, waziri mkuu kipenzi cha watanzania Hayati edward moringe sokoine kwa manufaa yao? sielewi!

Nini Nameloki mleteni Tendwa au Kiravu
 
Ni kweli kabisa, mahakama kama ilivyo inatakiwa kuwa chombo huru, na kwa kiasi fulani imejitahidi kuwa hivyo, lakini ni ukweli usiopingika kuwa mahakama haipo huru kama inavyotakiwa, fikiria kamati za maadili za mahakama zinakuwa chini ya wakuu wa mikoa ambao ni wanasiasa wateule wa rais, Jaji mkuu mwenyewe alikiri hivyo kuwa serikali inaingilia uhuru wa mahakama.

Hivi kweli kwa mtu mwenye akili timamu, anapoona wabunge wa ccm pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali, wanalazimisha wakuu wa mikoa waendelee kuwa wenyeviti wa kamati za maadili, hapo utasema hakuna maslahi wanayoyapata kwa mfumo huu?

Tusisahau pia kuwa idira ya mahakama imekithiri kwa rushwa, kwa wale walikuwa na kesi kadhaa wataelewa suala hili, rushwa si pesa tu, ni pamoja na favor za kujuana, ahadi za vyeo n.k, mahakimu na majaji wanapokea rushwa sana, sasa katika mazingira hayo imani kwa mahakama inatoweka, hata kama hukumu ya haki lakini watu hawawezi kuamini.

Lakini, kwa kuwa suala hili ni la kisheria zaidi, na sheria si ya mtu mmoja, basi ngoja tuwe na subira wataalamu wa CDM wafuatilie mwenendo wa kesi na hukumu yake, kesho tupate majibu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom