nimepitia threads nyingi na sehemu nyingi ili kuona mawazo ya wanachadema na viongozi wao. Nilichoona ni kuwa hawaaamini kama mahakama imetenda haki. Bali si hilo tu wamediriki kuhisi kuwa ati mahakama imeamuriwa na ikulu kufikia maamuzi yaliofikiwa
nimesikitishwa sana na watu ambao siku zote hujihesabu makini kwa kauli zao za kuhusisha ikulu na mahakama katika maamuzi.
Inawezekana hukumu haikuwa tamu kwao, na wanahisi hawajatendewa haki, na ndio maana kwenye sheria kukawa na haki ya kukata rufaa ili kuhakikisha haki inatendeka. Kwa hio ndugu zangu wa chadema kama mnahisi haki haijatendeka fateni taratibu za kisheria kudai haki zenu badala ya kuhubiri chuki na uongo
ndani ya chadema mna wanasheria wengi tu, watumieni ktk kuhakikisha haki inatendeka. Na si kuwa nyny mkishinda tu haki imetendeka mkishindwa haki haijatendeka huko ni kutokuwa watu wa haki.