Endeleaaa
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 1,485
- 740
Fedha zangu za kodi jamani oneni huruma!!!!!!!!!!!
Waambie wakurudishie kama zinakuuma sana. Mbona zinapoliwa hulalamiki?
Fedha zangu za kodi jamani oneni huruma!!!!!!!!!!!
Nimeanza kuwa na mashaka na wewe.Kama mbwai mbwai tu, chadema ikate rufaa.
Huyu jaji anadhihirisha wazi bila kificho kwamba ametoa hukumu isiyo halali kama kweli kifungu alichokisoma mbele ya kadamnasi sicho alichokiandika kwenye ruling yake, na kwa namna hiyo atakuwa ameidhalilisha sana mahakama na kuishusha mno hadhi yake, na kwa hali hiyo anaifanya mahakama iendelee kutoaminiwa na wananchi.
Ni jambo ambalo halikutarajiwa kwamba ubunge wa Lema utenguliwe halafu asizuiwe kugombea, tangu mwanzo nilikuwa sijaamini taarifa hiyo kwakuwa ccm wanaamini mwiba mchungu kwao ni lema, kwahiyo ni lazima wamuweke benchi. Lakini uzuri mmoja wa arusha ccm hawawezi kushinda ubunge hata lema asipogombea.
Serikali ina hela za mchezo. Chezeiya JK wewe!Hizi chaguzi zimekuwa too much sasa.
Anazuiwa kwa sababu gani? Kuna suala la kutumia rushwa kama hukumu ya Waryoba dhidi ya Wassira?
nimepokea sms toka kwa jamaa yangu wa karibu ambaye ni kada mkubwa wa magamba kanidokeza kuwa kuna tetesi chama kimejipanga kumrejesha mgombea mwanamke na chapuo linamwendea mbunge wa viti maalumu ndugu, dada yetu nameloki sokoine. Wadau mwasemaje? Je huyu dada katolewa kafara ama magamba wanategemea kutumia historia ya baba ya binti huyu, waziri mkuu kipenzi cha watanzania hayati edward moringe sokoine kwa manufaa yao? Sielewi!