Godbless Lema avuliwa ubunge

Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
Ikumbukwe kuwa msingi mzima wa kesi ni kuwa Lema alimdhalilisha Batilda Burian katika mojawapo ya mikutano ya kampeni. Kwamba, kuna maneno aliyasema ambayo yalikuwa ni ya udhalilishaji. Sasa hilo ni jambo linalowezakujadiliwa. Wale ambao mmesikiliza hukumu maswali yafuatayo yamejibiwa vipi. Binafsi sijaweza kuchukua msimamo wa hukumu yenyewe bila kuisoma vizuri na kuelewa reasoning ya jaji:

a. Mahakama imejuaje kuwa Batilda alidhalilishwa? - Bila kumuuliza yeye wanajuaej kuwa alijisikia kudhalilika. Vipi kama aliona ni ujinga tu wala haikumdhalilisha? Hivi mtu mwingine anaweza kwenda kusema "x ameibiwa" wakati yule ambaye anadaiwa kuibiwa anaona kila kitu chake kipo salama?

b. Imethibitishwa nini kuhusu alichosema Lema ambacho ni cha udhalilishaji? Alisema maneno gani, lini na wapi na ni ushahidi gani kuwa aliyasema hayo? Kwa mfano watu watatu wakija na walikuwepo kwenye mkutano wakasema hawakusikia maneno hayo na watu wengine watatu ambao walikuwepo kwenye mkutano huo wakasema walimsikia mahakama inaamua vipi kuwa hao watu watatu wanaosema walisikia wanasema kweli?

c. Binafsi kwa kweli sijashtushwa sana na Lema kuvuliwa ubunge - kama kuna ushahidi wa kutosha sidhani kama mahakam ailikuwa na uchaguzi mwingine- kilichonishtua zaidi na kinachonisumbua ni kuwa inaonekana hukumu ilishajulikana mapema zaidi almost a week kabla. Hili ni geni sana kwenye mahakama zetu. What happened?
 
Mkuu Kimbunga,
Safari hii utabiri wa Mwanakijiji umekwenda alijojo...

Alisema Lema atashinda kesi hiyo ya uchaguzi ana 99%99.

Hakasahau kuwa masuala ya sheria hayana uhusiano na utabiri.

Ritz

Umebadilika
 
Mahakama inasaidia tu kuwatafutia ccm aibu maana baada ya miezi 3 wataaibika tena kama walivyo aibika Arumeru. CCM hamtakiwi jamani! Ridhikeni na hayo majimbo mlopata kwa kuchakachua. Chaguzi ndogo zote mnazolazimisha hamtashinda hata mlete wapiga debe wenye matusi kuliko lusinde! Ahhhhhh!
 
Hukumu itolewe na wananchi wenyewe na wala si mahakama, kura zirudiwe tujue mshindi nani? kwa kesi kama hizi mahakama ziangalie maslahi ya nchi, kodi zetu zinatumika visivyo,wananchi wanazurumiwa vya kutosha!
 
Chadema wakisimamisha jiwe,ndo ligombee ubunge Arusha kwa tiketi yao still watashinda.Nawaonea huruma sana CCM.Waambieni Titanic imejaa maji,kinachofuata wanakijua wenyewe:kev:
 
yan sipati pcha cku watz wakianza kufanya silent assasn dhidi ya hawa wapuuzi walioamua kuchnganya siasa na kazi,itakuwa nchi gani hii.Pale ambapo njia za amani hazisaidii kuleta nafuu, bac revolution huwa haikwepeki.Vyama vizee ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi za kiafrika
 
Haki iko katika sanduku la kura, unaweza kumwaga damu ya ndugu zako na yako pia na Rais asiondoke Ikulu.
 
hakuna damu itamwagika Arusha mkuu..........watu wameelewa na tunasubiri kufanya maamuzi yetu kwenye sanduku la kura.....safari hii ni kimya kimya......



Well said, Preta! Tena nashauri hata kampeni haina haja maana mahakama wameshatufanyia kampeni tayari! A little affair like this one deserves the most minimum cost!

 
sasa nimeamini chadema mnapenda damu hata mawakala wenu mumewaua ili mpate sympathy
 
Another sad moment kwa wapenda haki na mabadiliko!
 
a. Mahakama imejuaje kuwa Batilda alidhalilishwa? - Bila kumuuliza yeye wanajuaej kuwa alijisikia kudhalilika. Vipi kama aliona ni ujinga tu wala haikumdhalilisha? Hivi mtu mwingine anaweza kwenda kusema "x ameibiwa" wakati yule ambaye anadaiwa kuibiwa anaona kila kitu chake kipo salama?
Sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985 inasema kuwa kesi ya uchaguzi inaweza kuletwa mahakamani na:
1. Mtu ambaye kisheria alipiga kura au alikuwa na haki ya kupiga kura kwenye uchaguzi unaohusu hiyo kesi.
2. Mtu ambaye anadai alikuwa na haki ya kuwa nominated au kuchaguliwa kwenye huo uchaguzi.
3. Mtu ambaye anadai kuwa alikuwa mgombea kwenye huo uchaguzi.
4. Mwansheria Mkuu wa Serikali

Kwa hiyo, ilikuwa sio lazima Batilda akafungue kesi mwenyewe. Nimeona watu wengi mpaka wanasheria wana-question inakuwa a thirdy party akafunge kesi. Lakini sheria ya uchaguzi inamruhusu mpaka mpiga kura kufungua kesi bila kuwepo kwa aliyeshindwa uchaguzi. Na hiki ndicho kilichofanyika kwenye kesi ya Lema.

b. Imethibitishwa nini kuhusu alichosema Lema ambacho ni cha udhalilishaji? Alisema maneno gani, lini na wapi na ni ushahidi gani kuwa aliyasema hayo? Kwa mfano watu watatu wakija na walikuwepo kwenye mkutano wakasema hawakusikia maneno hayo na watu wengine watatu ambao walikuwepo kwenye mkutano huo wakasema walimsikia mahakama inaamua vipi kuwa hao watu watatu wanaosema walisikia wanasema kweli?

Well, hapo inabidi mpaka kusoma huku yenyewe. Kuhusu mahakama itaamua vipi kama watu watatu walikuwepo kwenye mkutano wakasema hawakusikia maneno hayo na watu wengine watatu ambao walikuwepo kwenye mkutano huo huo wakasema walimsikia, issue ipo kwa ambao hawakumsikia. Inawezekana alisema lakini wao hawakumsikia. Unaweza ukawa kwenye mkutano wa hadhara na usisikie wanayosema waongeaji. Kama wangesema Lema hakusema kabisa basi hapo pande zote inabidi wadhibishe wanayoyasema. At the end of the day mahakama itaamnua on the balance of probabilities kulingana na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili.

c. Binafsi kwa kweli sijashtushwa sana na Lema kuvuliwa ubunge - kama kuna ushahidi wa kutosha sidhani kama mahakam ailikuwa na uchaguzi mwingine- kilichonishtua zaidi na kinachonisumbua ni kuwa inaonekana hukumu ilishajulikana mapema zaidi almost a week kabla. Hili ni geni sana kwenye mahakama zetu. What happened?
Inawezekana pia kwenye upande wa Lema hawakutilia maanani sana kama angeshindwa kesi hasa kwa sababu haikufunguliwa na Batilda mwenyewe. Yeye na timu yake were over-confident kuwa watashinda kesi, which I don't blame them really. Hata wewe si ulisema una uhakika kuwa Lema atashinda kesi? Lakini kuwa over confident inaweza kusabisha kutowa-scrutinize vizuri mashahidi. Hili ni fundisho kwa wengine. Whether kesi ni ndogo au kubwa kunahitaji umakini mkubwa sana hasa kwenye ushahidi unaotolewa.

Nimeona hata kwenye kesi ya Mnyika alipokuwa cross-examined kulikuwa na baadhi ya maswali alikuwa anajibu ovyo as if anajua zaidi mpaka jaji akamtahadharisha. Otherwise, hii inaweza kuwa moja ya sababu kwenye kwenye popular cases jaji anakuwa na humu mbili, halafu moja inakuwa leaked kupima upepo. Ikionekana poa, inasomwa hiyo hiyo. Taarifa kuwa Lema atashindwa kesi zilisambaa mitaaani kwa muda mrefu na hata Lema mwenyewe anadai aliambiwa na watu wa juu wa CCM na usalama wa taifa, lakini alichukua hatua gani?
 
Lema(23).jpg

Mbunge wa Arusha Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema


[h=2]Mahakama Kuu Kanda ya Arusha yamvua Ubunge Lema[/h]


NA ISSA MICHUZI



Mahakama Kuu ya mkoa wa Arusha imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema (pichani) mapema leo asubuhi.
Uamuzi huo umefikiwa leo asubuhi April 5. 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ua Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kessi y akupinga matokeo ya Ubunge ya Jimbo la Arusha Mjini yaliyowasilishwa an wanachama watatu wa CCm waliotaka Mahakam Kuu ya Kanda Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo.
Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).
Wanachama hao walidai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa kwa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.



CHANZO: NIPASHE

 
CCM waheshimu pesa za kodi za walalahoi. wanataka serikali igharamie uchaguzi mara ya pili kwenye jimbo ambalo sio lao?
 
iyo kete c ndo imefeli arumeru mashariki ni vp waitumie tena? baba ake sioi kafa juzi tu na watu wamegoma 'kumfuta machozi' sembuse sokoine
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom