sijui kama bado kuna strategic thinkers ndani ya CCM. kama bado hawajaona umaarufu wa Chadema basi warudi tena kwenye uchaguzi mdogo hivi karibuni. Kwa vyovyte vile watashindwa vibaya sana. na hii ina madhara makubwa sana kwao kama chama na taasis. kwa mtandao wa vyombo vya habari ulivyo na kwa aina ya kampeni zifanywazo kwa sasa, ni vigumu sana kwa kampeni ya uchaguzi mdogo kujikita kwenye masuala ya jimbo husika pekee. linakuwa ni suala la kitaifa ambalo kila raia analifuatilia. sasa kuitisha uchaguzi mwingine hivi karibuni na kushindwa tena vibaya ni mbaya kwa CCM kitaifa. CCM wanaweza jidai kuwa watatafiti na kusuka mikakati mipya na kutumia watu tofauti na waliotumika Arumeru Mashariki. Lakini wajuer kuwa CCM kama taasis haina watu wawezao kusimama na kubadili upepo wa kisiasa. ni kama kupambana na wimbi kubwa dhidi yao. hii ni kujipaka petroli na kupita juu ya moto. nawahurumia sana CCM lkn kwa mwenendo huu wanafanya kampeni ya urais ya Chadema kuwa nyepesi zaidi. na badala ya chadema kutumia muda na resources zao nyingine kwenda vijijini na kujiimarisha, sasa wamepata platform ya uhakika zaidi, ambayo kwa kusimama jukwaani katika jimbo moja, tayari inakujengea umaarufu mbali zaidi na ulipo. kwa kuhitimisha, Lema asikate rufaa mahakamani. arudi kwenye uchaguzi, ambao atashinda bila shida kubwa, mradi awe makini kudhibiti uchakachuaji, ambao CCM ndo silaha yao kubwa kwa sasa. kwa mara nyingine, Mungu anatuonesha watanzania kuwa anaipenda hii nchi na pumba zitajionesha tena hivi karibuni.