Godbless Lema avuliwa ubunge

Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
Nimepokea sms toka kwa jamaa yangu wa karibu ambaye ni kada mkubwa wa magamba kanidokeza kuwa kuna tetesi chama kimejipanga kumrejesha mgombea mwanamke na chapuo linamwendea Mbunge wa Viti maalumu Ndugu, Dada yetu Nameloki Sokoine. wadau mwasemaje? je huyu dada katolewa kafara ama magamba wanategemea kutumia historia ya baba ya binti huyu, waziri mkuu kipenzi cha watanzania Hayati edward moringe sokoine kwa manufaa yao? sielewi!

Huyo dada namfahamu ni mshenzi sana na sijui alipateje pataje ubunge wa viti maalumu kupitia Monduli!!!!

Akigombea huyo hata kama CDM ikisimamisha kivuli, kivuli kitashinda tu na siyo yeye tu hata JK akija hapa atashindwa maana hata kura zar urais Arusha hazikutosha dhidi ya Dr. Slaa.
 
Naye analetwa ili 'afutwe machozi? Delusional CCM wamlete tu hamna shida.
 
Huyo dada namfahamu ni mshenzi sana na sijui alipateje pataje ubunge wa viti maalumu kupitia Monduli!!!!

Akigombea huyo hata kama CDM ikisimamisha kivuli, kivuli kitashinda tu na siyo yeye tu hata JK akija hapa atashindwa maana hata kura zar urais Arusha hazikutosha dhidi ya Dr. Slaa.

ushezi wake nini? mi nampenda
 
CCM haiwezi kushinda Arusha period. Arusha ni mji wa biashara na hakuna mfanyabiashara wa kweli Tanzania anayependa serikali hasa CCM. Kihalali CCM haiwezi kwa sasa kushinda Arusha mjini hata kama sokoine akifufuka leo.Hii ni kupotezeana muda na pesa tu vilevile inasababisha Chadema wawe mashuhuri zaidi.
 
Huyo dada namfahamu ni mshenzi sana na sijui alipateje pataje ubunge wa viti maalumu kupitia Monduli!!!!

Akigombea huyo hata kama CDM ikisimamisha kivuli, kivuli kitashinda tu na siyo yeye tu hata JK akija hapa atashindwa maana hata kura zar urais Arusha hazikutosha dhidi ya Dr. Slaa.
Huyu ushenzi wake ni upi mkuu? mbona anaonekana ni mstaarabu sana! nampa heshima zangu kwa heshima ya Marehemu Hayati sokoine!
 
Nakumbuka sana siku Lowassa alipokuja kumpigia kampeni AICC kupitia viti maalum.
Wamama walilalamika sana kitendo cha Lowassa kuja kumpigia kampeni hawara wake. Tena walidai kuwa Lowassa anataka kuwaweka hawara zake tu, maana Jimbo la Arusha alifanikiwa kumpitisha hawara mwingine ambaye ni Batilda.
 
Heeeeh! kumbe walikuwa wanafanya hako kamchezo eeeh? na yule mtoto je?
 
Hata mumsimamishe Slaa, hampati kitu hapa. CCM tumejipanga kulichukua hili jimbo hata kwa bilion 900. Mtajibeba!!!
Kwani Arumeru mlitumia ngapi?
Angalieni isije kuwa watanzania wameshajua namna ya kuwaadabisha mafisadi. Kula pesa yao kura wape wapinzani.
 
Kama CCM wanafagilia kusimamisha mwanamke kwani ni lazima wamsimamishe Mtoto wa kigogo?
Kwanini wasimpendekeze Katherine Magige?
 
Nimepokea sms toka kwa jamaa yangu wa karibu ambaye ni kada mkubwa wa magamba kanidokeza kuwa kuna tetesi chama kimejipanga kumrejesha mgombea mwanamke na chapuo linamwendea Mbunge wa Viti maalumu Ndugu, Dada yetu Nameloki Sokoine. wadau mwasemaje? je huyu dada katolewa kafara ama magamba wanategemea kutumia historia ya baba ya binti huyu, waziri mkuu kipenzi cha watanzania Hayati edward moringe sokoine kwa manufaa yao? sielewi!

Endeleeni kupiga ramli soon utasiki Ridhiwani.....
 
tuwekeni sawa,kama ukiwa mbunge wa viti maalumu unaruhusiwa kugombea tena ubunge wa kuchaguliwa!Inawezekana kumbe mtu mmoja ukawa viongozi duh ama kweli hii ndo magamba origional
 
Kuna Mtoto wa Sokoine tayari ni Mbunge; Kuna Mtoto wa Sokoine tayari yuko Ubalozini Canada hataki kukaa bongo Ameishi USA kwa Miaka 6 sasa yuko Canada kwanini Mnawapa hao watoto wa wakubwa; wana Ngo'mbe zaidi ya Elfu, wana nyumba wanasomeshwa na serikali ...

Ni sisi wanyonge tungependa kuwa Wabunge tusaidie wanyonge wenzetu, tusaidie nchi yetu angalau !!!
 
Nimepokea sms toka kwa jamaa yangu wa karibu ambaye ni kada mkubwa wa magamba kanidokeza kuwa kuna tetesi chama kimejipanga kumrejesha mgombea mwanamke na chapuo linamwendea Mbunge wa Viti maalumu Ndugu, Dada yetu Nameloki Sokoine. wadau mwasemaje? je huyu dada katolewa kafara ama magamba wanategemea kutumia historia ya baba ya binti huyu, waziri mkuu kipenzi cha watanzania Hayati edward moringe sokoine kwa manufaa yao? sielewi!

Kuna sms kanitumia rafiki wa karibu wa kaka wa mama yake huyo rafiki yako amesema magamba watamsimamisha REJAO kugombea.
 
Sioi Sumari katoka kufiwa juzi tu na Baba yake. Kaachiwa mzigo mkubwa wa kusomesha wadogo zake na kulea familia yake. Ni vema CCM ikaangalia hatima ya Sioi Sumari. Hana kazi jamani! Msaidieni mwenzenu huyu. Arusha ipo karibu na Kenya, ni rahisi kwa sioi kupata kura za wahamiaji.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom