Mara baada ya kuwa mbunge Mh Lema amekumbana na misukosuko ya hali ya juu kiasi kila binadamu mwenye utu alikuwa anamuonea huruma! Lema amepigwa sana na askari, amewekwa ndani,mara zote amekuwa anawindwa ili auwawe na sasa kavuliwa ubunge!
Ikiwa kama kifungu alichohukumiwa nacho ni cha 114 tafsiri yake anazuiwa kujihusisha na mambo ya siasa kwa kipindi kisichopungua miaka 5.
Sababu ya yote haya ni yeye kudai haki ya wananchi wake! Alisimama kidete kuupinga utaratibu uliotumika kumpata meya wa jiji la arusha sababu iliyopelekea maauaji ya raia watatu hivyo kupelea kuchukiwa na rais, waziri mkuu na spika wa bunge (yeye mwenyewe amedai hivyo) Inasikitisha sana!
Inapotokea binadamu wa kawaida ukafanyiwa hivi!! unafanya nini sasa???
Makundi hatari ya kigaidi kama Alqaeda, Alshabab na hamas yalianza kwa mtindo kama huu aliofanyiwa Lema! mwenyewe nimeshuhudia watu kadhaa wakitoa machozi pale walipopata taarifa kuwa Mh Lema kavuliwa ubunge!! sijui wanachofikiria kwa sasa masikini.
Kaza moyo Bro. Lema kwani Umeshinda!! Yesu wa nazareti alifanyiwa madhila zaidi ya hayo! lakini leo duniani kote ni Kwa jina lake!
God bless our lovely mp: Lema
Viva Lema, Viva Cdm Aluta continua!