Godbless Lema avuliwa ubunge

Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
Du!! jimbo litabaki wazi hadi 2015. Inasemekana akikata rufaa kesi itaendelea hadi 2015 asipokata rufaa tume itasema haina pesa za kufanya uchaguzi mwingine.
 
tangu mwanzo nilishangazwa sana na magamba kukubali ghafla kushindwa jimbo la arumeru mashariki, nilijua kuna jambo linatafutwa kisayansi hapo. wameshapata kauli ya kujibu tayari, loh!
''mbona arumeru tumelubali? mbona segerea pia tumekubali??'' jimbo la arusha lina siri nzito sana, tangu Lema achaguliwe JK sidhani kama alishawahi kufika arusha na kuongea hata na makatibu wa CCM wilaya, achilia mbali wananchi. someni alama wakuu.
 
I second that mkuu! Na kama hukumu imetolewa kihalali, they better use that second chance effectively!
 
Ccm hata ikisimamisha jiwe itashinda Lema hajafanya chochote tangu awe mbunge zaidi ya sifa za kijinga za kukataa dhamana na kupelekwa mahabusu!

ccm ambayo imekuwa madarakani tangu miaka 50 iliyopita imefanya nini leo ili ishinde? Badala yake tunazidi kuona umasikini unazidi kuongezeka kwa mwananchi wa kawaida wakati viongozi wa ccm na serikali wanazidi kuneemeka. Wananchi wanazidi kufa kwa maradhi na kukosa matibabu wakati viongozi wa ccm na serikali wanatibiwa ng'ambo. Kina mama wajawazito wanazidi kufa wakati wa kujifungua, wakati wake wa viongozi wa serikali wanajifungulia nje ya nchi. Watoto wetu wanaketi chini na kufeli mitihani wakati viongozi wa ccm na serikali wanasoma nchi za nje. Serikali iliyopo madarakani inatakiwa kuleta maendeleo kwa wananchi wake, na sio kuleta dhiki. Kazi ya mbunge sio kuleta maendeleo katika jimbo lake, bali kuichoche serikali kuleta maendeleo.
 
CCM haipo juu ya Mungu. Lema usikate tamaa, mtumaini Bwana. Wizi, hila, na dhuluma haviwezi kushindwa wema hata siku moja. Tutakuombea usiku na mchana, na kuendelea kulaani janga la Taifa, chama cha makundi, magamba CCM. Tunajua Hakimu amepokea malekezo toka kwa CCM, maana ndo wanamlipa mshahara
 
Uchaguzi hata ufanyike kesho,Lema atashinda! Arusha tena!
 
Chadema msijazane ujinga bana ,bwana Lema ameona asikate rufaaa kwasababu anauhakika ashapoteza hivyo na kweli alifanya upuuzi kutoa lugha chafu, ,mbunge gani anafujo namna hiyo na kuutukana mkono uliomlisha toka akiwa mdogo, sasa kakua anajikuta na yeye anamabavu ya kuleta fujo na matusi sasa imemcost...
Mkonogani huo unao ambukiza taifa kipindupindu?
 
Ninachomuombea Lema ni afya njema na maisha marefu...Ubunge wa Arusha mjini ni wake hata kama CCM watasimamisha malaika...!
Tafadhali unapotaja Malaika utaje malaka wa giza kwa kua hao tuu ndio SiSIEMU wanashabihiana nao. Magamba watu wa nguvu za giza you know!!
 
ccm wamepiga mahesabu vibaya,hawakufikiria gharama za kushinda jimbo la Arusha,kwa kweli ni hasara kubwa sana kwa kuwa watashindwa vibaya kwenye uchaguzi na gharama yake itakuwa kubwa zaidi kwa chama,yetu macho
mkuu tatizo la CCM ilikuwa sio jimbo, tatizo ni mtu wao watakayemtumia, either awe CDM au chama kingine chochote, Lema hanunuliki mkuu, arusha kuna mengi yamejificha.
 
sikieni lema ni kweli kapigwa chini ila chadema tutawagaragaza ccm kuliko wanavyofikiri watapata aibu kubwa kuliko waliyopata arumeru mashariki wasubiri uchaguzi utangazwe lema achukue fomu chadema tuwagaragaze
 
Lema kavulia ubunge rasmi...

Hii ni taarifa rasmi toka hapa mahakamani!


hapa inatakiwa ccm wakate rufaa ili lema asivuliwe ubunge kwakuwa kuvuliwa kwake kutaifanya chadema izidi kupaa! kama jimbo laililokuwa linashikiliwa na ccm chadema wamelichukua je jimbo ambalo cdm ilikuwa inalishikilia je?
 
CCM hawatafuta pingamizi lolote tu......na tume ya uchaguzi tunajua imelalia upande gani

Kabla ya Chadema kuamua kutokata rufaa inabidi wapitie vifungu vyote husika vya sheria kama Lema anawezawekewa pingamizi. Inawezekana jaji kasema anaruhusiwa kugombea tena lakini still akawekewa pingamizi kama zipo sheria zozote za kumzuia. Kwa hili Chadema wanahitaji wasiwe na papara. Mwanasheria Mkuu anaweza kukata rufaa vile vile kwa jaji kutomzuia Lema kugombea. Wanasheria wa Chadema inabidi waingie library kwanza kubukua. Hapa ndio tutaona umakini wa Chadema.
 
Je Mwansheria Mkuu akikata rufaa? Huenda hii ngoma bado mbichi.

Mkuu je umoja wa washauri wa Mkuu wa Kaya kwenye haya masuala ya kisheria hasa mambo ya siasa!.
Hatua hiyo kisheria inaweza kumweka mkuu wa Kaya kwenye chati nzuri kidogo.Ila usisahau kumshauri katika madai yake mwanasheria Mkuu asisahau haki ya wana-Arusha kuwakilishwa Bungeni.Maana hilo ndilo linalogombewa.

Ila shida ninayoona ni kuwa mfumo wa mahakama umekwisha ingiliwa na mafisadi.
Ngoja tuone hukumu yenyewe imezingatia nini.
 
NI DHAHIRI BAADA SIKU TISINI, UCHAGUZI UTAFANYIKA, NA MH.G.LEMA a.k.a NELSON MANDELA ATARUDI TENA BUNGENI..,NAONA CCM WANA HAMU SANA YA KUMWAGA PESA ZAO KWENYE KAMPENI NA WANA RAHA SANA KUTUMIA RASILLIMALI ZA TANZANIA KWENYE CHAGUZI AMBAZO HAZINA MSINGI...,HII KWA G.LEMA NI KAMA LIKIZO TU YA MUDA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom