Godbless Lema avuliwa ubunge

Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
Kwanza nitoe pole zangu za dhati kwa Kamanda Lema.....lakini pili nimtie moyo kwamba asiwe na wasiwasi ubunge wa Arusha mjini ni wa kwake. Jambo moja tu lililonisikitisha katika mchakato wa kesi hii nalo ni 'inakuwaje hukumu inajulikana na watu wajigamba kwa mbwembwe wiki moja kabla ya hukumu kusomwa??
 
hata chadema wakisimamisha mbuzi mee....tutamchagua mbuzi meee...

Hivi preta huponagi tu hiyo malaria yako??? Unaongea na drip mkononi?? hakyamungu CHADEMA kweli mna kitu kama laana.
 
asee pole yake sana..ndo ataacha matusi next time..
 
Mkuu PJ,

Nadhani CDM & Lema hawana haja ya kukata rufaa upepo wa siasa unavuma vizuri hasa baada ya ushindi wa Arumeru Mashariki.
CCM walipanga double blow washinde Arumeru na wampige chini Lema lakini imekuja ndivyo sivyo. Ndivyo demekrasia ilivyo.
 
Angalisho liwekwe, maana kama kesi ilikuwa hivyo na hukumu ikawa hivyo, basi kuna mkakati mkubwa sana wa serikali na chama chake (CCM) wa kulitaka jimbo hilo la arusha kwa gharama yoyote

Chadema wawe makini sana na Kumsimamisha Lema, kama mahakama imesema Lema anaweza kugombea basi hapo kuna agenda ya siri inawekwa ili bwana Lema atakapotia jina tu basi Pingamizi litawekwa na kwa Mizengwe waliyoipanga ni lazima pingamizi litapita tu

kwa Mwenendo wa hukumu nzima Chadema inawapasa wawe makini mno, maana sasa wanashindana na nguvu kubwa zaidi

ni mtazamo tu
 
Hukumu ya mahakama Lema kashindwa,sasa mtaona hukumu ya wananchi dhidi ya CCM uchaguzi ukirudiwa
 
Hii ina matokeo chanya na inaimarisha upinzani, kama maamuzi ni ya hila basi hila hizo ni dhidi ya ccm na serikali yake!
 
Ooh no!
Lakini tukumbuke kwamba, hizi ndio harakati za ukombozi, zinakuwa na njia ngumu sana na zenye maumivu makali hata wakati mwingine umwagaji wa damu.
Mwaka huu naona kama mapambano ya ukombozi wa kweli wa Tanzania ndio yameziduliwa rasmi na CDM.
Naomba sana CDM isije kukata rufaa, kwani kufanya hivyo mahakama hizi za magamba zitatumia delaying tacts ili uchaguzi usirudiwe.
Aibu kubwa kuliko ie ya ARMR inakuja kwa ccm.
Aluta continua!!
 
hili tulichukue kwa tahadhari kubwa binafsi nashauri CDM wakate rufaa,ccm wanajua hawawezi kushinda,wanaweza kutokutanga hicho kiti kuwa wazi kwa muda mrefu hadi 2015 si mbali,we all know hatuna demokrasia na hatuna independent judiciaary shame on you judge uliyedecide hukumu hiyo,what goes around comes around.kama umepindisha haki ktk hili................u will see it very soon.Mungu ibariki Tanzania na ifishe ccm
 
Nipo hapa viwanja vya mahakama kuu kanda ya Arusha, Kilaza LEMA kapigwa chini. Semeni sasa nyie magwanda. Chezea CCM nyie!!!!! Niliwaambia jana mkaleta mboyoyo zenu

Kumbe ndicho kilichokuleta jana?? Sasa
unashangilia ushindi wa mezani? Unadhani kwenye ballot box CCM inaweza??
Join Date : 3rd April 2012
Posts : 43
Rep Power : 309
Likes Received3
Likes Given7
 
Hali ya mji wa arusha imechafuka watu wanamtaka mbunge wao.hii hela inajotumika kutuliza machafuko si ingelisha yatima na wajane

Usiwe na wasiwasi. Hali itadhibitiwa. Zana zilizokuwa Arumeru hazijaondoka. Mwenye kiherehere asubiri kuvunjwa kiuno.
 
Kuna msemo unasema haki si itendeke tu, bali ionekane kama imetendeka. Asilimia 90 ya post za hii thread zinaonyesha kuwa wadau wengi hawajaona kama haki imetendeka. Sasa mfumo wetu wa Judiaciary unakwenda wapi? Mimi sijui hata hivyo ni vigumu kumridhisha kila mtu!

Cha msingi ni kukata rufaa (kama anaona ameonewa), ingawa hata uchaguzi ukifanyika leo CDM lazima wachukue jimbo kwani kurudi kwenye uchaguzi kuna gharama kubwa sana (au ndio nchi ya siasa!). Hata hivyo suala zuri zaidi ni kwamba hukumu hiyo inamruhusu Lema kugombea tena. Sasa tusubiri hukumu ya Makongoro na ile ya Aeshi
 
na kawaida ya ccm ni kuiba mbaya zaidi tumeshajua namna ya kuzuia wizi wao watafanyaje?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom