Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
Lema akiongea na radio one.."nimepigikiwa simu tangu jana kuhusu uamuzi huu...na hata H.Mdee amenitaarifu mapema asubuhi kuwa amepata habari kwa mtu nyeti kuwa nimeshindwa kesi...polisi wamezingira ofisi ya mbunge alfajiri na hata mahakamani kabla ya uamuzi hii inaonyesha ilishapangwa...makamba aliongea na mtu wa ccm kumtaarifu ajiandae kwa kura za maoni....hata wakirudia uchaguzi bado nitashinda...nasubiri tamko la chama ndio niwajuze wananchi nini cha kufanya".
 
Nyambafuuuuuu kumbe huna akili hujui mnazidi kujidhalilisha ngojeni kitakachowakuta. CDM forever. Unajisahau tu kuwa nyie ni wakoloni yaani mpo tu toka enzi ila hamuwezi kushindana na nguvu ya umma. Nyambafuuuuu:tape2:
 
January Makamba.
Wana ccm tumefurahi kuwa uchaguzi wa Arusha utarudiwa....tulijua sisi wanaccm kuwa Lema atashindwa...tumefanya utafiti mitaani na kuona kuwa kesi kwa Bwana Lema angeshindwa..

Aiseeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!
 
mzee wa vipedo na malapa

Taifa hili litaendelea kuongiozwa na wasiopendwa kwa sababu ya kasumba zenu hizi! Ifike mahali tuwe kitu kimoja tuache kejeli na matusi baina yetu. Misri wakristo na waislam hawakuangalia dini zao waliangalia mustakbali wa nchi yao ndio wakafanya maamuzi sisi labda baada ya miaka 6000!. Ni ushauri wangu tu.
 
CDM haina haja na rufaa.CCM imsimamishe tena Burian.Uchaguzi huend ukawa Julai mosi au Julai 7.Hivyo Lema anapumzika kwa miezi miwili tu kuwepo nje na atarudi tena.Fomu ya kugombea tutamlipia.

Wanabodi,
Sio haki hata kidogo kwa walipakodi. Rufaa ikatwe manake hamna hoja ya kurudia ubunge hapa. Hizo pesa zikahudumie jamii za wamasai kwa kuwaboreshea shule au Majosho.
 
Utabiri wa Mwanakijiji leo ujafanya kazi? alitabiri %99.99 Lema anashinda kesi...Mwanakijij upo Mkuu wangu! mambo ya kisheria hayana uhusiano na utabiri.
 
Nimejiuliza Sana! Hivi CCM mna agenda gani (Kufa au Kuishi, Kuzirai au kuzimia). Arusha mjini ni nani atasimama mbele ya MAKAMANDA na Nguvu Ya Uma! Je, Mkapa (Atasema hamtambui baba yake Mbowe, baada ya kushindwa jaribio la kutomtambua Vicent), Wasira (Atasema Slaa hajawahi kuwa Padri baada ya kushindwa jaribiola uongo uliovuka mipaka juu ujio wa Papa dhidi ya Slaa na Pesa za michango, sijui hii itakuaje!), Mwigulu na wenzake (Wao wanategemea majira yatakuwa ya Mvua au Kiangazi). CHADEMA itadumu milele. Mungu ibariki CHADEMA.
 
hii yote ni kuwatia wananchi hamasa ya mabadiliko na ukombozi .... this is an automatic promo to CDM and yes united we stand
 
Kwa CCM pamoja na kwamba Lema kavuliwa ubunge lakini hawana cha kufurahia, sana sana wataendelea kujiabisha tu uchaguzi utakapoitishwa!
 
hawa magamba ni bure wanajisumbua hata wafanye nini Arusha mjini watachukua watambue kwamba hapa hawana chao tena.
 
Ofcoz hili ni tatizo na Wana Arusha tunawanyima haki yao ya msingi ya Kupata maendeleo kwa CDM ni wakati mzuri wa Kujitangaza na kujiongezea umaarufu coz ushindi lazima ila kwa hili LEMA na yeye ajifunze manake ya Lusinde sasa ni ya wanaCCM wote na sasa CDM tusha advance sana jamii imeanza kupata imani na matumaini na Mchama. Poleni wana CDM na wana Arusha Wote
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom