Godbless Lema, achana na Siasa za kuongelea watu, na majungu jikite nini utaifanyia nchi hii ya Tanzania

Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
726
1,000
Godbless Lema ni mmoja ya wanasiasa mahiri, na uwa nampenda kwa misimamo yake, na hasa kipindi cha mwanzo alivyoingia Bungeni. Ila shida moja ambayo naona inazidi kukua na kutamalaki. Lema amekuwa muda mwingi anaongelea watu binafsi, si vibaya mara moja kujadili utendaji wa mtu katika majukumu yake. Lakini Lema muda wote nikuongea kuhusu watu. Mie nadhani watanzania wanataka kusikia nini ndoto au maono yako juu ya Taifa hili, ambalo limepiga makitaimu kwa muda mrefu kimaendeleo.

Tanzania inahitaji viongozi wenye maono ambao wataivusha nchi hii. Tunahitaji kusikia mikakati iliyopo, ya kuleta mabadiliko na si kulalamika kila siku na majungu ambayo utadhani ni vikao vya kinamama katika magenge ya ususi. Wananchi tunachoka kusikia kila siku mtu anamuongelea mwanaume mwenzie, mara huyu yuko hivi, mara huyu kapandishwa cheo. Kupandishwa cheo ni moja ya matakwa ya utumishi wa umma. Mtu hawezi kutumika miaka yote asipandishwe cheo.

Hizi siasa ni cheap politics, ni siasa ambazo hazina ufumbuzi kwa matatizo ya matanzania. Lema alipofungwa alijiita Mandela. Ukifuatilia maisha ya Mandela toka alipofungwa na kutoka gerezani hakuwahi kuongelea mtu. Hatukumsikia alivyotoka kuanza kumwongelea Kaburu na vyombo vya usalama vya nchi kuvidharau na kujiona yeye ndo yeye. Kaburu Botha alikuwa mkatiri, na alitumia polisi kuwaadabisha watu. Lakini hakuna sehemu Madela aliponyanyua ulimi kutoa majungu. Bali alitumia muda wa gerezani kuandika vitabu vya kiukombozi. Mafano wa Kitabu "No Easy Task" Mandela alijenga mioyo ya waafrika kusini kuwapa matumaini na kuonesha njia ya mapambano.

Lema achana na majungu ya kuongelea watu. "Don´t discuss about people" Tupe mbinu na mikakati ya kimaendeleo, ili tukuone una mind kubwa ya kuleta mabadiliko. Si tukilala tukiamka wewe ni kumsema, mtu, mara Sabaya, mara Mnyeti, mara sijui mkuu wa polisi wilaya fulani, mara sijui nini! Kama kweli hii ndo siasa basi wamama wa Saloon na magengeni wanaweza wakawa wanasiasa wazuri sana.

Wakati vyama vya siasa vinaanza, tulikuwa na wabunge machachali sana kama marehemu DR. Lamwai, Mabere Marando, na wengineo, sikuwahi ona wakitumia muda wao kuongelea watu binafsi. Hata nguli Maalimu Seif Shariff Hamad, hakuwai ongelea mtu. Yeye alijenga na kusimamia hoja zake. Na wananchi walimuelewa. Wapinzani inahitajika kutafakari, vinginevyo CCM itaendelea kubaki kutawala. Wananchi wa Tanzania wanaakili sana. Wanakusikiliza wanakuacha tu. Ila wanajua huyu hakuna kitu. Siku ya kura wanafanya maamuzi. Tutaendelea kulalamika tunaibiwa kumbe kosa letu.
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,939
2,000
Viongozi na watumishi wa serikali wanapokosolewa, ni sahihi. Na wala siyo kuwaongelea watu binafsi. Naona umeguswa sana. Lazima wewe ni mmojawapo wa hao waliokosolewa.

Pia hayo unayosema yaliongelewa, yaweke hapa ili tuweze kujuwa usahihi wa hoja yako.
 
JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
315
500
Jaji siyani anasema hakuna sehemu yoyote katika Andiko lako lote ulipoonyesha wapi Lema ameongelea watu,amemuongela nai wapi na lini. hivyo madai yako ameyatupilia mbali kwa kukosa Mashiko.
 
Townchild

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
7,578
2,000
Maswali machache kwako, mbona wakati was wanasiasa hao machachari hukuwa mmoja wao, na je ni zipi strong politics na umewahi kuzijaribu wapi? Ila ujue kama umejichanganya kwenye 18 zake lazima akupe za uso. Hivyo yafaa utuambie nini kimekuthibu na sii kulalama humu.
 
Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
726
1,000
Mbona CCM na polisi zimejikita kupambana na watu badala ya umasikini.
Ndo shida ya watu, si lazima ufanye afanyacho mwenzio, njoo na wazo mbadala tuone kitu cha tofauti. Kama CCM na polisi wanafanya hivyo kwanini muwaige. Ili uwepo ushawishi tunahitaji kitu tofauti! Hupana wa mawazo.
 
Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
726
1,000
Maswali machache kwako, mbona wakati was wanasiasa hao machachari hukuwa mmoja wao, na je ni zipi strong politics na umewahi kuzijaribu wapi? Ila ujue kama umejichanganya kwenye 18 zake lazima akupe za uso. Hivyo yafaa utuambie nini kimekuthibu na sii kulalama humu.
Maswali mengine, unaweza cheka sasa unataka wote tuwe wanasiasa? Nimewatolea mfano kwasababu walikuwa ni wanasiasa makini. Swala la kuingia kumi na nane, mimi si kiongozi ila nimeshauri. Na sibabahiki na mipasho. Akili ndogo uongelea watu, hivyo kwangu nitampuuza mtu kama huyo. nacho taka ni kubadili fikira za wanasiasa wetu. Akili kubwa haina muda wa kuongelea mtu.
 
Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
726
1,000
Tatizo lako una upungufu wa akili kichwani!
Alie na upungufu ni wewe badala ya kujibu hoja unakimbilia kutukana. Rudi ufundishwe adabu na wazazio. Najiuliza malezi yako yalikuwa vipi! Make mwana mwenye malezi mema ni fahari kwa babaye.....Ila weye Mmmmh! Sijui
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Mimi nimpenda HAKI na UHURU kwa binadamu wote siwezi kukuona wewe mpumbavu katika kuingilia uhuru na haki ya Lema kuongea chochote kile atakacho kuongea ambacho hakivunji sheria za nchi. Hivyo ujinga wako peleka lumumba siyo humu.

Na wewe ni nani unae jipendekeza kwa Lema na kumsemea? Najua anae weza msemea Lema ni mke wake. We huko upande gani? Na ujinga unaosema huna haki ya kunikataza kutoa mawazo yangu we nani? Nyani haoni kundule!
 
Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
7,537
2,000
Alie na upungufu ni wewe badala ya kujibu hoja unakimbilia kutukana. Rudi ufundishwe adabu na wazazio. Najiuliza malezi yako yalikuwa vipi! Make mwana mwenye malezi mema ni fahari kwa babaye.....Ila weye Mmmmh! Sijui
Wewe ni mpumbavu!
 
Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
726
1,000
Unaelewa maana ya mtumishi wa umma?

Hao watumishi wa umma kina Mnyeti na sijui wakuu wa polisi kazi zao ni binafsi?
Sijaongelea utumishi wa umma, nimeongelea mtu binafsi. Ndo maana Sabaya haja shitakiwa kama mtumishi wa umma kashitakiwa binafsi. Ingekuwa utumishi wa umma kungekuwa na taratibu zingine. Hivyo mtumishi wa umma hauondoi ubinafsi au hulka ya mtu.
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
12,904
2,000
Godbless Lema ni mmoja ya wanasiasa mahiri, na uwa nampenda kwa misimamo yake, na hasa kipindi cha mwanzo alivyoingia Bungeni. Ila shida moja ambayo naona inazidi kukua na kutamalaki. Lema amekuwa muda mwingi anaongelea watu binafsi, si vibaya mara moja kujadili utendaji wa mtu katika majukumu yake. Lakini Lema muda wote nikuongea kuhusu watu. Mie nadhani watanzania wanataka kusikia nini ndoto au maono yako juu ya Taifa hili, ambalo limepiga makitaimu kwa muda mrefu kimaendeleo.

Tanzania inahitaji viongozi wenye maono ambao wataivusha nchi hii. Tunahitaji kusikia mikakati iliyopo, ya kuleta mabadiliko na si kulalamika kila siku na majungu ambayo utadhani ni vikao vya kinamama katika magenge ya ususi. Wananchi tunachoka kusikia kila siku mtu anamuongelea mwanaume mwenzie, mara huyu yuko hivi, mara huyu kapandishwa cheo. Kupandishwa cheo ni moja ya matakwa ya utumishi wa umma. Mtu hawezi kutumika miaka yote asipandishwe cheo.

Hizi siasa ni cheap politics, ni siasa ambazo hazina ufumbuzi kwa matatizo ya matanzania. Lema alipofungwa alijiita Mandela. Ukifuatilia maisha ya Mandela toka alipofungwa na kutoka gerezani hakuwahi kuongelea mtu. Hatukumsikia alivyotoka kuanza kumwongelea Kaburu na vyombo vya usalama vya nchi kuvidharau na kujiona yeye ndo yeye. Kaburu Botha alikuwa mkatiri, na alitumia polisi kuwaadabisha watu. Lakini hakuna sehemu Madela aliponyanyua ulimi kutoa majungu. Bali alitumia muda wa gerezani kuandika vitabu vya kiukombozi. Mafano wa Kitabu "No Easy Task" Mandela alijenga mioyo ya waafrika kusini kuwapa matumaini na kuonesha njia ya mapambano.

Lema achana na majungu ya kuongelea watu. "Don´t discuss about people" Tupe mbinu na mikakati ya kimaendeleo, ili tukuone una mind kubwa ya kuleta mabadiliko. Si tukilala tukiamka wewe ni kumsema, mtu, mara Sabaya, mara Mnyeti, mara sijui mkuu wa polisi wilaya fulani, mara sijui nini! Kama kweli hii ndo siasa basi wamama wa Saloon na magengeni wanaweza wakawa wanasiasa wazuri sana.

Wakati vyama vya siasa vinaanza, tulikuwa na wabunge machachali sana kama marehemu DR. Lamwai, Mabere Marando, na wengineo, sikuwahi ona wakitumia muda wao kuongelea watu binafsi. Hata nguli Maalimu Seif Shariff Hamad, hakuwai ongelea mtu. Yeye alijenga na kusimamia hoja zake. Na wananchi walimuelewa. Wapinzani inahitajika kutafakari, vinginevyo CCM itaendelea kubaki kutawala. Wananchi wa Tanzania wanaakili sana. Wanakusikiliza wanakuacha tu. Ila wanajua huyu hakuna kitu. Siku ya kura wanafanya maamuzi. Tutaendelea kulalamika tunaibiwa kumbe kosa letu.
Mkuu mbona umebadili ID?😂😂😂
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom