Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,637
Godbless Lema ni mmoja ya wanasiasa mahiri, na uwa nampenda kwa misimamo yake, na hasa kipindi cha mwanzo alivyoingia Bungeni. Ila shida moja ambayo naona inazidi kukua na kutamalaki. Lema amekuwa muda mwingi anaongelea watu binafsi, si vibaya mara moja kujadili utendaji wa mtu katika majukumu yake. Lakini Lema muda wote nikuongea kuhusu watu. Mie nadhani watanzania wanataka kusikia nini ndoto au maono yako juu ya Taifa hili, ambalo limepiga makitaimu kwa muda mrefu kimaendeleo.
Tanzania inahitaji viongozi wenye maono ambao wataivusha nchi hii. Tunahitaji kusikia mikakati iliyopo, ya kuleta mabadiliko na si kulalamika kila siku na majungu ambayo utadhani ni vikao vya kinamama katika magenge ya ususi. Wananchi tunachoka kusikia kila siku mtu anamuongelea mwanaume mwenzie, mara huyu yuko hivi, mara huyu kapandishwa cheo. Kupandishwa cheo ni moja ya matakwa ya utumishi wa umma. Mtu hawezi kutumika miaka yote asipandishwe cheo.
Hizi siasa ni cheap politics, ni siasa ambazo hazina ufumbuzi kwa matatizo ya matanzania. Lema alipofungwa alijiita Mandela. Ukifuatilia maisha ya Mandela toka alipofungwa na kutoka gerezani hakuwahi kuongelea mtu. Hatukumsikia alivyotoka kuanza kumwongelea Kaburu na vyombo vya usalama vya nchi kuvidharau na kujiona yeye ndo yeye. Kaburu Botha alikuwa mkatiri, na alitumia polisi kuwaadabisha watu. Lakini hakuna sehemu Madela aliponyanyua ulimi kutoa majungu. Bali alitumia muda wa gerezani kuandika vitabu vya kiukombozi. Mafano wa Kitabu "No Easy Task" Mandela alijenga mioyo ya waafrika kusini kuwapa matumaini na kuonesha njia ya mapambano.
Lema achana na majungu ya kuongelea watu. "Don´t discuss about people" Tupe mbinu na mikakati ya kimaendeleo, ili tukuone una mind kubwa ya kuleta mabadiliko. Si tukilala tukiamka wewe ni kumsema, mtu, mara Sabaya, mara Mnyeti, mara sijui mkuu wa polisi wilaya fulani, mara sijui nini! Kama kweli hii ndo siasa basi wamama wa Saloon na magengeni wanaweza wakawa wanasiasa wazuri sana.
Wakati vyama vya siasa vinaanza, tulikuwa na wabunge machachali sana kama marehemu DR. Lamwai, Mabere Marando, na wengineo, sikuwahi ona wakitumia muda wao kuongelea watu binafsi. Hata nguli Maalimu Seif Shariff Hamad, hakuwai ongelea mtu. Yeye alijenga na kusimamia hoja zake. Na wananchi walimuelewa. Wapinzani inahitajika kutafakari, vinginevyo CCM itaendelea kubaki kutawala. Wananchi wa Tanzania wanaakili sana. Wanakusikiliza wanakuacha tu. Ila wanajua huyu hakuna kitu. Siku ya kura wanafanya maamuzi. Tutaendelea kulalamika tunaibiwa kumbe kosa letu.