Godbless Lema, achana na Siasa za kuongelea watu, na majungu jikite nini utaifanyia nchi hii ya Tanzania

Mimi nimpenda HAKI na UHURU kwa binadamu wote siwezi kukuona wewe mpumbavu katika kuingilia uhuru na haki ya Lema kuongea chochote kile atakacho kuongea ambacho hakivunji sheria za nchi. Hivyo ujinga wako peleka lumumba siyo humu.
Ujinga ni huo uliona kudhani kutukana ndo njia pekee ya kutetea hoja. Hii inaonesha ujinga wa malezi uliopata!
 
Sijaongelea utumishi wa umma, nimeongelea mtu binafsi. Ndo maana Sabaya haja shitakiwa kama mtumishi wa umma kashitakiwa binafsi. Ingekuwa utumishi wa umma kungekuwa na taratibu zingine. Hivyo mtumishi wa umma hauondoi ubinafsi au hulka ya mtu.
Sabaya ameshitakiwa kwa yale aliyoyafanya akiwa mtumishi wa umma.

Weka ushahidi hapa wa kile kilichosemwa na Lema kuhusu hao viongozi wa umma ili tujuwe kama ni mambo yao binafsi.
 
Ingia you tube search, usingoje kutafuniwa kila kitu. Inaonesha hujui nini kinatenganisha binafsi na kazi. Watumishi wote ni watu binafsi. Kazi ni kuajiliwa tu haiondoi ubinafsi wao. Kwa Tanzania ni Rais tu ndiye si binafsi. Huyu analindwa na sheria.
 
Niingie YouTube tena na wakati hapa JF una uwezo wa kuweka link ili kusudi hoja yako iwe na mashiko? Kuweka link kama reference ya unachokiongelea ndiyo kutafuniwa?

Kazi za umma siyo kazi binafsi. Lakini watumishi wa umma wanaweza kutumia nafasi zao kwa masalahi yao binafsi. Au maslahi ya chama...Ni lazima wakosolewe.
 
Niingie YouTube tena na wakati hapa JF una uwezo wa kuweka link ili kusudi hoja yako iwe na mashiko? Kuweka link kama reference ya unachokiongelea ndiyo kutafuniwa?

Kazi za umma siyo kazi binafsi. Lakini watumishi wa umma wanaweza kutumia nafasi zao kwa masalahi yao binafsi. Au maslahi ya chama...Ni lazima wakos
Asiye jua maana aambiwi maana! Nadhani uelewi hata nacho kiongelea. Usinitoe nje ya mada. Lete mada yako nawe!
 
Hii mada ni mfano wa tatizo lililopo la copy & paste bila kuchanganya na zako.

Iko hivi, siasa inafanywa na watu, ndio wanaitwa wanasiasa, na hakuna siasa bila watu; mipango miovu, uvunjifu wa sheria na madudu mengine yote hufanywa na hawa watu wanaoitwa wanasiasa.

Wakikosea lazima wakosolewe, haiwezekani tuishi kwenye nchi yenye wanasiasa /viongozi wasiofuata sheria halafu waachwe tu ili tuongelee maendeleo/nini tutaifanyia Tanzania.

Hicho tutakachoifanyia Tanzania kitafanyika vyema zaidi kama misingi ya uhuru wa kisiasa na haki za binadamu vitalindwa na kuheshimiwa, hivi visipoheshimiwa akili za watu haziwezi ku-focus kwenye nini waifanyie Tanzania.

Muda wote watakuwa na hofu ya kufikiria usalama wao na ndugu zao, hivyo muhimu kwanza usalama wa raia bila kujali itikadi zao uheshimiwe na wanasiasa/watawala ili tuanze kufikiria kuisogeza mbele Tanzania.

Muhimu zaidi, hawa wanasiasa sio majini ni watu na wanafahamika, lazima watajwe kwa majina yao ili wakumbushwe majukumu yao kwa raia wa nchi hii bila kujali itikadi za vyama vyao.
 
Godbless Lema ni mmoja ya wanasiasa mahiri, na uwa nampenda kwa misimamo yake, na hasa kipindi cha mwanzo alivyoingia Bungeni. Ila shida moja ambayo naona inazidi kukua na kutamalaki. Lema amekuwa muda mwingi anaongelea watu binafsi, si vibaya mara moja kujadili utendaji wa mtu katika majukumu yake. Lakini Lema muda wote nikuongea kuhusu watu. Mie nadhani watanzania wanataka kusikia nini ndoto au maono yako juu ya Taifa hili, ambalo limepiga makitaimu kwa muda mrefu kimaendeleo.

Tanzania inahitaji viongozi wenye maono ambao wataivusha nchi hii. Tunahitaji kusikia mikakati iliyopo, ya kuleta mabadiliko na si kulalamika kila siku na majungu ambayo utadhani ni vikao vya kinamama katika magenge ya ususi. Wananchi tunachoka kusikia kila siku mtu anamuongelea mwanaume mwenzie, mara huyu yuko hivi, mara huyu kapandishwa cheo. Kupandishwa cheo ni moja ya matakwa ya utumishi wa umma. Mtu hawezi kutumika miaka yote asipandishwe cheo.

Hizi siasa ni cheap politics, ni siasa ambazo hazina ufumbuzi kwa matatizo ya matanzania. Lema alipofungwa alijiita Mandela. Ukifuatilia maisha ya Mandela toka alipofungwa na kutoka gerezani hakuwahi kuongelea mtu. Hatukumsikia alivyotoka kuanza kumwongelea Kaburu na vyombo vya usalama vya nchi kuvidharau na kujiona yeye ndo yeye. Kaburu Botha alikuwa mkatiri, na alitumia polisi kuwaadabisha watu. Lakini hakuna sehemu Madela aliponyanyua ulimi kutoa majungu. Bali alitumia muda wa gerezani kuandika vitabu vya kiukombozi. Mafano wa Kitabu "No Easy Task" Mandela alijenga mioyo ya waafrika kusini kuwapa matumaini na kuonesha njia ya mapambano.

Lema achana na majungu ya kuongelea watu. "Don´t discuss about people" Tupe mbinu na mikakati ya kimaendeleo, ili tukuone una mind kubwa ya kuleta mabadiliko. Si tukilala tukiamka wewe ni kumsema, mtu, mara Sabaya, mara Mnyeti, mara sijui mkuu wa polisi wilaya fulani, mara sijui nini! Kama kweli hii ndo siasa basi wamama wa Saloon na magengeni wanaweza wakawa wanasiasa wazuri sana.

Wakati vyama vya siasa vinaanza, tulikuwa na wabunge machachali sana kama marehemu DR. Lamwai, Mabere Marando, na wengineo, sikuwahi ona wakitumia muda wao kuongelea watu binafsi. Hata nguli Maalimu Seif Shariff Hamad, hakuwai ongelea mtu. Yeye alijenga na kusimamia hoja zake. Na wananchi walimuelewa. Wapinzani inahitajika kutafakari, vinginevyo CCM itaendelea kubaki kutawala. Wananchi wa Tanzania wanaakili sana. Wanakusikiliza wanakuacha tu. Ila wanajua huyu hakuna kitu. Siku ya kura wanafanya maamuzi. Tutaendelea kulalamika tunaibiwa kumbe kosa letu.
Mi nashangaa. Yaani hujajua hadi leo lema ni kaputi. He is not a person of ideas. Yeye ni mtu wa cheap politics. Shida ni mtu no book halafu ni mtu wa siasa za ubinafsi..siasa za maslahi binafsi.
 
Bora ya mjinga ukimuelimisha ataelewa kuliko mpumbavu, mpumbavu ni sifa kama urefu na ufupi huwezi kubadilishwa.

Wewe ni mpumbavu. Period.
 
Hii mada ni mfano wa tatizo lililopo la copy & paste bila kuchanganya na zako.

Iko hivi, siasa inafanywa na watu, ndio wanaitwa wanasiasa, na hakuna siasa bila watu; mipango miovu, uvunjifu wa sheria na madudu mengine yote hufanywa na hawa watu wanaoitwa wanasiasa.

Wakikosea lazima wakosolewe, haiwezekani tuishi kwenye nchi yenye wanasiasa /viongozi wasiofuata sheria halafu waachwe tu ili tuongelee maendeleo/nini tutaifanyia Tanzania.

Hicho tutakachoifanyia Tanzania kitafanyika vyema zaidi kama misingi ya uhuru wa kisiasa na haki za binadamu vitalindwa na kuheshimiwa, hivi visipoheshimiwa akili za watu haziwezi ku-focus kwenye nini waifanyie Tanzania.

Muda wote watakuwa na hofu ya kufikiria usalama wao na ndugu zao, hivyo muhimu kwanza usalama wa raia bila kujali itikadi zao uheshimiwe na wanasiasa/watawala ili tuanze kufikiria kuisogeza mbele Tanzania.

Muhimu zaidi, hawa wanasiasa sio majini ni watu na wanafahamika, lazima watajwe kwa majina yao ili wakumbushwe majukumu yao kwa raia wa nchi hii bila kujali itikadi za vyama vyao.
Katika siasa tumahitaji viongozi wenye maono. Tunahita viongozi ambao watatueleza sera na mikakati yao. Na hasa kutuondoa katika hizi shida tulizo nazo. Hii ni pamoja na hayo unayoyasema. Mfano, hao viongozi unaosema hawafuati sheria, unadhani dawa yao ni kupiga majungu kuwa watabadilika, au polisi itabadilika kwa kuwasema kama mipasho. Never.

Nini kinahitajika, Lema aje na hoja kuwa tunaviongozi ambao hawafuati sheria, yeye au chama kikipewa ridhaa na wananchi watabadili baadhi ya kada au nyazifa namna ya uteuzi au kupatikana kwa hao viongozi katika utumishi wa umma, na kusimamia nidhamu kazini. Then anatupa mikakati ni vipi atafanya.

Kama ni polisi atueleze akiingia madarakani nikimaanisha chadema watafanya reform katika polisi. Aelezee ni vipi polisi itabadilishwa kiwe chombo kisicho na mawaa.
Haya mambo ndo tunataka sikia, na mikakati kadhaa ya maendeleo. Mfano angefanya hata kongamano la online kuongelea wakulima, Chadema inaonaje wakulima na wafugaji wetu wa Tanzania. Wakawashirikisha wakulima mawazo na maono ya chama. Au wakaongelea juu ya elimu yetu nchini, akawashirikisha wadau kadhaa online. Hi itabadili mawazo ya watu taratibu na kuanza kujua Chadema inakusudi na maono mazuri.

Lakini kama ndo hayo majungu haisaidii na unaowasema wapo kwenye mamlaka. Uwezi badilisha kitu. Watu watakuona ni umbea tu unafanya.
Tunataka mawazo chanya hata aliepo madarakani ukiyatoa anaona wewe ni watofauti. Mfano nachukua kwa Zito, amekuwa anajikita kueleza nini kifanyike, analeta wazo mbadala. Si majungu ambayo mwisho wa siku haimsaidii mwananchi wakawaida unae taka akupe kura yake siku moja.
 
Bora ya mjinga ukimuelimisha ataelewa kuliko mpumbavu, mpumbavu ni sifa kama urefu na ufupi huwezi kubadilishwa.

Wewe ni mpumbavu. Period.
Upumbavu upo kwa mtu ambae hakufunzwa na wazazie. Uenda malezi yake aliyapata kusiko eleweka. Mpumbavu ni mtu ambae yeye udhani kutukana ni suluhu ya jambo. Mpumbavu ni yule adhaniae yeye ni mjanja. Hivyo ni sikulahumu kwani ilo neno limekujaa katika moyo wako. Litokalo kinywani ndo liijazayo nafsi ya mtu. Hivyo umejazwa na upumbavu unao uongelea. Na hii ni shida ya malezi.
 
Hapa hujaongea, ila umeandika tu, mpumbavu wewe.
Ili neno la upumbavu unadhani ni tishio kwangu. Wewe mie siwale atukanwapo anaogopa kutoa hoja, umechemsha. Kwanza inaonesha uwelewa wako ulivyo. Na kukimbilia matusi. Nayajua matusi. Ila nakuhifadhi. Kikubwa welevu wa mtu upimwa na maneno yamtokayo kinywani. Jipime mwenyewe! hapo umejioonaaa ati unajuaaa kutukana ha ha ha ! another one!
 
Back
Top Bottom