Kamwe na katu Lema hawezi kupita Ubunge Arusha Mjini chini ya Uongozi wa Makonda

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
14,957
9,378
Ndugu zangu Watanzania,

Msione Lema ameanza kuweweseka na kupiga mayowe mitandaoni kabla hata Mwamba Mwenyewe Makonda hajaapishwa na kwenda kutua katika ardhi ya Arusha na kitovu cha utalii Afrika mashariki na kati na kukabidhiwa ofisi ya mkuu wa mkoa.. Lema anafahamu na kuelewa wazi wazi kuwa ndio mwisho wake wa ndoto zake za kutaka ubunge tena kupitia Arusha mjini.

Lema anamfahamu vyema Mwamba Makonda,anafahamu kuwa Mwamba Makonda ni kiongozi jasiri na imara sana na asiyetaka mchezo mchezo wala masihara kazini.anafahamu Mwamba ni mtu wa maamuzi,misimamo na asiye yumba wala kubembeleza mtu. Lema anafahamu ya kuwa ujio wa Mwamba Mkoani Arusha ndio mwisho wa upinzani na makelele ya upinzani mkoani hapo na ukanda huo wa kaskazini.

Lema anafahamu ya kuwa kwa uchapa kazi na ubunifu wa Mwamba Makonda itapelekea upinzani kujifia wenyewe na kukosa ushawishi kwa wana Arusha.Lema anafahamu ya kuwa ndio mwisho wa siasa za kihuni huni na janja janja,ndio mwisho wa utapeli na ulaghai wa kisiasa,anajuwa ndio mwisho wa kupata kura za wana Arusha, maana Mwamba Makonda kwa uchapa kazi wake na ubunifu wake na kama mjumbe wa kamati ya siasa mkoa anakwenda kukichumia na kukikusanyia kura za ndio chama cha Mapinduzi CCM.

Arusha inakwenda kubadilika na kupaa kimaendeleo na hivyo wananchi hawatakuwa na sababu wala kufanya majaribio ya kuwapa kura ya ndio watu aina ya Lema ambao wakati wote wa ubunge wake alifanya kazi ya kulivuruga jiji la Arusha na kupandikiza migogoro na mivutano isiyokwisha wala kukoma ndani ya halmashauri na hivyo kukwamisha shughuli za maendeleo.kwa hakika wana Arusha hawawezi kukubali tena jiji lirudiye nyakati hizo.wana Arusha wanataka maendeleo na sasa wamepelekewa mpenda maendeleo na mchapa kazi Mwamba Mwenyewe Paul Makonda.

Kwa hiyo mkiona lema na CHADEMA wana weweseka na kupiga mayowe naomba muwapuuzeni ,maana maji yamewafika shingoni na wamebaki wanatapatapa kutafuta huruma na msaada wa watu wa kuwaokoa katika kifo cha kisiasa ambapo hata hivyo hakuna matumaini ya kupona.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Wamasai wanahutaji mtu wa kuwasemea, sema wenye maslahi yao wameamua kulinda maslahi Yao. Hakika haki ni mbinguni tu.
 
Wamasai wanahutaji mtu wa kuwasemea, sema wenye maslahi yao wameamua kulinda maslahi Yao. Hakika haki ni mbinguni tu.
Kama unayo kero ya aina yoyote ile basi wewe subiri kidogo muda siyo mrefu mwamba atakuwa hapo katika ardhi ya Arusha,wewe ukanyookage moja kwa moja mpaka ofisini kwake upeleke kero yako na itashughulikiwa kwa haraka sana.
 
Back
Top Bottom