Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Ghala la silaha Gongo la Mboto lalipuka!

Airport imesimamisha huduma kwa mda kwa sababu za kiusalama zaidi,tusubirini tupewe chanzo
 
poleni sana this time watu lazima wawajibishwe!!! for the second time? inamaaana kambi za jeshi hazikujifunza lolote kutokana na maaafa ya mbagala??? nothing was done kwenye kambi ambazo zipo karibu namakazi ya wananchi???? comon this is too much!!!!
 
Nategemea mpaka kesho asubuhi waziri wa ulinzi hussein mwinyi na mkuu wa majeshi jenerali mwamnyange watakuwa wamejiuzuru kabla ya kutakiwa maana hii ni mara ya pili inatokea wao wakiwa madarakani. Ukweli wameshindwa kazi na hasa baada ya mlipuko wa mbagala kutokea na wao kusema haitatokea teeeeena.

Mwinyi na mwamnyange must resign immediately
 
pole saana mpevuu,,
Allah atakujaalia wepesi wewe na familia yako
 
Hivi Katavi ni sawa Kova kuelekeza wananchni cha kufanya badala ya Jeshi mbona hawa jamaa mi wananichanganya, Sehemu ya JWTZ wanaongea Polisi, sehemu ya Polisi wanaongea JWTZ au siku hizi wanafanya kazi pamoja!!?
JWTZ wamesema watu wakae kilometa 10 kutoka eneo la kambi nae Kova anasema warejee majumbani, sasa sijui lichukuliwe la nani!
 
God help waathirika wa mabomu haya...nailaani serikari hii dharimu isiyo jifunza kwenye mambo yaleyale..poleni ndugu zangu.
 
Huu ndio upuuzi.

Unawezaje kusema ni ajali tu wakati hujachunguza? Kwa nini sio uzembe? Anajuaje kwamba sio njama?

This sucks. Majibu mepesi. Mkuu wa Mkoa anawaambia watu wakimbilie Tazara yeye anasema wakae nyumbani. Nyumba ikianguka kutokana na ufa? What is this?
 
Airport imesimamisha huduma kwa mda kwa sababu za kiusalama zaidi,tusubirini tupewe chanzo
Mkuu, unategemea nini toka kwenye tume itakayoundwa?...ni porojo tu, hutapata jipya!
Kwa inference ya kwanza NI UZEMBE MTUPU!..Ulisikia nchi za jirani kuna mambo kama haya?
Kama mkasa huu ulitokea Mbagala just the last year, kwanini wasijifunze??..
Usisubiri taarifa ya KIMA yeyote. ican assure you utakuwa discouraged na taarifa ya kijeshi!
 
Watu zaidi ya 5, wamekufa, wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa, by ITV

Tuwaombee wote wanaopatwa na janga hili. Poleni sana.
 
Tangu mwanzo wa dunia ajali ya magala ya mabomu kulipuka ilishawahi kutokea kweli? Na hasa ilishawahi kutokea katika nchi moja mara mbili?

Kama mkuu wa nchi anajichekesha mbele ya wananchi wenye umaskini jeshi litakuaje?
 
Mimi nko mbali na familia inayoishi Kipunguni na wasiwasi ni kwa kwenda mbele. Wamekimbilia Ubungo Kibangu na kuacha nyumba peke yake.
 
Watu zaidi ya 5, wamekufa, wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa, by ITV

Tuwaombee wote wanaopatwa na janga hili. Poleni sana.
Mkuu,
Mbona mi sioni wakitangaza lolote?...Au huku niliko ninakamata ITV ya KERICHO?
 
I suppose!..
Ila cha ajabu ni kwamba TV zimekomaa na matangazo ya kawaida...hawaonyeshi kitu zaidi ya sentensi za kuflash pale chini!
Taaluma ya habari bado haijakomaa TZ, matukio mengi yanaripotiwa kiushabiki au kwa maslahi ya watu fulani, mbona polisi wakipiga raia kwenye maandamano ya wapinzani TV ndo zinakuwa mstari wa mbele kurusha matukio live.
 
Nadhani mambo ni shwari sasa.nimewasiliana na mkazi wa banana anasema wamerudi kwenye nyumba zao.
 
Katavi acha Uongo. Hali imetuli kwa sasa. Mimi nimepangiana zamu na wife yeye kalala na watoto mimi nipo zamu hadi saa 8.00 namwamsha aendelee ili nami nipate usingizi kidogo. huwezi kulala kwani kama haya yanayoruka kuelekea sehemu zingine yakikukuta haupo macho ni hatari tu
Ahahahaah pole sana Nyati uongo wangu ni nini hapa? Umepata kahawa lakini, maana kukaa macho hadi saa nane.....!! Pole sana.
 
Back
Top Bottom