Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,148
Huenda labda mambo ni mengi au yako kasi kupita maelezo mpaka yamenipita au nimeshindwa kuyaelewa. Hili la kuibuka ghafla mitandaoni na mitaani, chuki na dhihaka dhidi ya waalimu bado sijalielewa kabisa.
Nimehisi huenda labda limeletwa na mojawapo kati ya haya mambo mawili lakini bado sioni muunganiko wa moja kwa moja.
1. Walimu kuwepo kwenye orodha ya makarani wa sensa huku watu wengi wasiokuwa na kazi kukosa. (Binafsi sioni kama hili lina uzito mnoo, kwa kuwa tangu hapo awali kama jadi miaka yote, zoezi la sensa hufanywa zaidi na walimu kama ilivyo suala la uchaguzi)
2. Nyongeza ya mishahara iliyotangazwa ilivyotumika kuwalaghai watumishi wa umma na mwisho wa siku watumishi wamekuja kugundua kuwa wametapeliwa na serikali! (Sijui walimu kipekee linawagusaje? Labda wao ndio walilishabikia zaidi hapo kabla? Ama huenda walimu wamefaidika na hii nyongeza kuliko kada zingine? Au walimu hawajaona tatizo na wamepongeza hii nyongeza?)
Wenye ufahamu zaidi wanaweza kutusaidia katika hili fumbo, nini chanzo cha kuibuka ghafla kwa chuki na dhihaka dhidi ya waalimu hapa Tanzania?