Rais Samia ni shujaa katika vita dhidi ya ujinga, maradhi na umasikini

Political Jurist

Senior Member
Sep 6, 2021
115
92
Na.Amon Nguma

Baba wa Taifa letu Hayati.Mwl.Julius Nyerere alianzisha vita dhidi ya maadui watatu yani Ujinga,Maradhi na Umaskini na kwamba kama Taifa tukifanikiwa vita hii tutakuwa na maendeleo na hadhi nzuri ya maisha katika Taifa letu.

Kazi ilianza awamu ya kwanza na baadae awamu zilizofuata nazo zilifanya kazi kwa jitihada kadri ilivyowezekana ,hatimaye tumefika awamu ya sita chini ya Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan,ni kweli pasipo shaka kwamba Rais huyu ametangaza vita kamili kwa vitendo dhidi ya maadui hawa na tumepiga hatua kubwa na kwa uchache kama ifuatavyo -;

1). Vita dhidi ya Ujinga.
Katika Vita dhidi ya adui ujinga tumeshughudia jitihada kubwa zikifanyika katika kuboresha huduma za elimu wa wananchi wa Tanzania

-Ujenzi wa Madarasa zaidi ya 20000 nchi nzima .
- Ujenzi wa Shule za Sayansi za Wasichana kila Mkoa.
-Ugawaji wa vifaa vya TEHAMA kwa walimu na wakufunzi.
- Vibali vya ajira kwa kada ya Elimu kwa miaka mitatu mfululizo .
-Nyongeza ya kibajeti katika Mikopo ya Elimu ya Juu .
-Kutoa Mikopo ya Elimu kwa wanafunzi wa Vyuo vya Kati kwa mara ya kwanza .
-Kufadhili tafiti mbalimbali katika taasisi za elimu ikiwemo zinazohusu kilimo na mazingira.
-Ufadhili wa Masomo katika vyuo vya ndani na nje ya Nchi.
-Samia Scholarship .
-Nyongeza ya Mishahara na Motisha kwa watumishi wa Sekta ya Elimu .

Hizi kwa uchache na nyengine nyingi ambazo zinalenga kuondokana na adui ujinga na kujenga jamii iliyoelimika na rasilimali watu yenye tija katika utoaji huduma na ukuzaji wa Uchumi wa Taifa.

2).Vita dhidi ya Maradhi .
Katika eneo hili pongezi kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu kwa mapinduzi makubwa katika sekta ya Afya ,mengi yamefanyika na yafuatayo kwa uchache -;

-Ujenzi wa Wodi za ICU pamoja na kuongeza Vitanda vya ICU kutoka vitanda 258 vilivyokuwepo awali mpaka vitanda zaidi ya 1000 ,huduma ya ICU sasa inapatikana kila Mkoa .

-Huduma za Maji safi na salama kwa Watanzania ambapo miradi ya maji inatekelezwa nchi nzima.

-Ukamilishaji wa Hospitali za Kanda ikiwemo ya Kusini sanjari na ujenzi wa Hospitali za Rufaa Mikoa ya Katavi, Geita,Mara,Songwe na Shinyanga zenye Teknolojia ya kisasa .

- Uzinduzi wa Mitambo ya kisasa ikiwemo X-Rays ,CT Scans ,MRI,Fluoroscopy kwenye hospitali za Wilaya,Mikoa ,Kanda na Taifa ikienda sanjari na matumizi ya TEHAMA.

-Uzinduzi wa Kliniki kwa wagonjwa wa Selimundu( Sikoseli) katika hospitali za Wilaya na Mikoa kote nchini .

-Ajira kwa Watumishi wa Afya zaidi ya 20000 sanjari na uendelezaji wataalamu wa afya ndani na nje ya nchi.

-Ujenzi na ukamilishaji wa Kituo cha Mpango wa Taifa wa Damu salama Jijini Dodoma( Central Zone Blood Transfussion Center) .

-Uzinduzi wa Mitambo ya Cathlab na Carto3 kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) .

-Ununuzi wa Magari ya Wagonjwa zaidi 700

-Serikali kuzindua huduma za Ubingwa Bobezi ikiwemo Upandikizaji Uroto na nyingine nyingi .

-Uboreshaji wa Huduma za Bima sanjari na mpango wa Serikali wa kuja na Mpango wa Bima ya Afya kwa wote .

Haya kwa uchache ni baadhi ya kazi kubwa iliyofanyika ,huduma bora za Afya ni silaha muhimu na adhimu katika vita dhidi ya Adui Maradhi ,vita inayoongozwa na Jemedari Dkt.Samia Suluhu Hassan ,uungwana ni vitendo ,na kwa vitendo hivi ni dhahiri kuwa Rais Samia amedhamiria kupambana na adui maradhi na mafanikio na matokeo tunayaona .

3). Vita dhidi ya Adui Umaskini .
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais.Dkt.Samia imefanya kazi kubwa katika kuwakwamua na kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuepukana na adui umaskini na kwa uchache kama ifuatavyo -;

-Serikali inaendelea na Mpango wa kunusuru kaya maskini ( TASAF) ambapo familia nyingi nchini zinanufaika na mpango huu na kuwawezesha kujitegemea .

-Mapinduzi katika Kilimo ,Mifugo na Uvuvi ambazo ndizo sekta zilizoajiri asilimia zaidi ya 70 wa Wananchi ambapo serikali inaendelea na miradi ya umwagiliaji na uwezeshaji wananchi kupitia mikopo,ruzuku ,utafiti,teknolojia na uwezeshaji mbegu .

-Mpango wa Jenga Kesho Iliyo Bora ( BBT) mpango huu unalenga kuwainua vijana na wanawake ambapo vijana wanapewa ardhi ,elimu na uwezeshaji fedha .

-Mikopo ya Halmashauri ya asilimia 10.
-Utoaji wa Elimu ya Ufundi Stadi (VETA ) na JKT ambazo vijana wanapata ujuzi na kuutumia kuingiza kipato .

- Serikali kuvutia uwekezaji kupitia Diplomasia ya Uchumi ,mitaji kuingia nchini na kupelekea upatikanaji wa ajira kwa wananchi .

-Utekelezaji wa Miradi mikubwa kama SGR na na miradi kote nchini ambayo imetoa ajira za moja kwa moja na zile zisizo za moja kwa moja .

-Jitihada za Rais Samia za kukuza utalii zenye dhamira ya kuhakikisha rasilimali zinawanufaisha watanzania .

Jitihada hizi na nyengine nyingi zimeendelea kuwainua wananchi kiuchumi na kuwawezesha kumudu mahitaji yao muhimu na ya msingi na hii ndio dhana halisi ya vita dhidi ya umaskini .

Mwisho wa hatua moja ni mwanzo wa hatua nyingine ,maendeleo ni hatua ,na kwa kila hatua hatuna budi kujipongeza na kuboresha zaidi .Mafanikio yanatokana na uongozi bora na mzuri ,tunaye kiongozi jasiri na mpambanaji wa kweli Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ametuwezesha kufika hatua hii na kuisogeza vita dhidi ya maadui hawa kwa kasi na kiwango kikubwa sana .

Hongera sana Mhe.Rais wetu kwa kazi hii kubwa ,usife moyo chapa kazi ,watanzania tunakuombea heri na afya njema katika majukumu yako ,wito kwa wasaidizi wa Mhe.Rais na Watumishi wa umma kwa ujumla chapeni kazi ili kutimiza dhamira ya Mhe.Rais na watanzania kwa ujumla.


Tumetoka mbali ,tulipo ni pazuri ,tunapokwenda matumaini ni makubwa zaidi chini ya Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Kazi Iendelee .
IMG-20221225-WA0088(1).jpg
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom