Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,693
- 23,044
Awali napenda kusema mimi si chawa wala mshabiki wa chawa wa DP world na si mfuasi wa Dr Slaa au Mwabukusi bali natoa maoni yangu kama nilivyochambua masuala yalojitokeza hususan suala la kukamatwa Dr Slaa na Mwabukusi na wenzao na kisha kubadilishiwa makosa kutoka kuwa ya uchochezi hadi kuwa ya uhaini.
Kuna jambo moja ambalo serikali mbalimbali hufanya ili kuwanyamazisha wanasiasa ambao huitwa "firebrand" walopitiliza, hutumia njia ya kukusukuma pembeni au kukutoa kwenye kundi au kwenye ulingo wa siasa.
Neno "Purge" ni neno la kiingereza likimaanisha kutapisha au kuondoa kwa ghafla. Sasa Hapo mtu au kundi fulani huondoshwa ghafla kutoka katika jukwaa la siasa, michezo na maeneo mengine lakini lengo likiwa ni kukumaliza kisiasa, kimichezo na kukupoteza kabisa kwenye macho ya jamii.
Kiongozi yoyote yule ambae hushindwa kuvumilia mijadala, malumbano ya hoja na kuhojiwa ni lazima atumie mbinu hii ya "Purge" ili kumaliza mzozo.
Viongozi wengine hutumia njia hii kwa "level" ingine kabisa ambayo wengine hufikia kuagiza fulani ashughulikiwe kisawasawa na hata nchi kama Marekani sasa hivi raisi wa zamani Donald Trump yuko na msukomsuko kuhakikisha hagombei uraisi wa nchi hiyo ingawa msukomsuko huo wazidi kumuongezea umaarufu na uhakika wa kuwa raisi tena.
Sasa Dr Wilbroad Slaa na wakili Mwabukusi na wengine, ni watu ambao wamekosea namna yao ya uwasilishaji hoja zao. Hoja zao zaweza kuwa sahihi kabisa na hata watu wengi wakaona ni hoja sahihi kabisa kuhusu suala la mkataba wa serikali na DP world, lakini namna au mtindo wa uwasilishaji wake ndo umekuwa tatizo.
Mimi nimeishi ughaibuni na nimeishi na watu mbalimbali na nikajifunza kuwa hata ukiwa watoka Tanzania ukifika ughaibuni ni lazima utabadilika tu katika kuwasilisha hoja zako hata uwe na jazba kiasi gani. Utaweza tu kutumia lugha zisizo na ustaarabu ukiwa mitandaoni lakini katika majukwaa ya kisiasa kamwe hutamsikia mwanasiasa au mtu yoyote akizungumza lugha kali ya vitisho na ya kudharau mamlaka.
Ndo maana ughaibuni hata mbunge akitoa lugha ya ukakasi kama vile kusema mbunge mwenzake ni mwongo, au laghai au apenda kudanganyadanganya, ataamrishwa na spika wa bunge afute kauli yake hiyo vinginevyo ataondolewa bungeni.
Na wakati mwingine mbunge huyo akitoa kauli za kudhalilisha mamlaka hutakiwa kuomba msamaha palepale bungeni na mambo huendelea.
Hapa ndipo nnapokuja kwa mwanasiasa Tundu Lissu ambae kadri muda unavyozidi kwenda amekuwa makini sana na mtindo wa uwasilishaji hoja zake katika hadhira hata kama lugha hiyo pengine yaonekana ni ya dharau. Mara nyingi ametumia maneno makali sana na ya kustua lakini amekuwa ndani ya mistari wa haki yake ya kutoa maoni kikatiba.
Lakini nyuma ya pazia hatufahamu ni kwanini Tundu Lissu atumia mtindo ule wa kisiasa katika kuwasilisha hija zake na ni kwanini akiwa ndani ya Chadema yuko na kinga zaidi kuliko huko nje aliko Dr Slaa na akina Mwabukusi na asipatwe na madhara yoyote kutoka kwenye mikono ya jeshi la polisi?
Lakini Dr Slaa amejiamini kupita kiasi kwa kuzingatia kuwa alikuwa balozi na akadhani kuwa labda alivuka mstari mwekundu huenda akafikiriwa. Hatufahamu ajenda zingine alizonazo Dr Slaa lakini huenda waloamua akamatwe na apachikwe makosa ya uhaini kutoka kwenye makosa ya uchochezi wao wanafahamu mengi likiwamo suala la Dr Slaa kutaka kugombea uraisi mwaka 2025.
Kulikuwa na mada kadhaa za tetesi humu JF kwamba Dr Slaa alikuwa mbioni kujiunga na cha kisiasa au kutaka kupewa nafasi ya kuwa mgombea mahala fulani jambo ambalo litakuwa lilizisha mtafaruku miongozji mwa watesi wake kisiasa wakiwemo wanachama wa CCM. Dr Slaa ni mtu makini na anafahamu kuwa ukivuka mipaka matokeo yake ni nini, lakini kwa hili la sasa lilomkumba baada ya mambo kama haya kumkumba mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na kisha kuachiwa kwa msamaha maalum kupitia mpango wa maridhiano kuna uwezekani mkubwa kuwa kuna mpango mahsusi wa kumfanyia Dr Slaa kitu hicho kiitwacho "Purge".
Hivyo hii "purge" hatufahamu itakuwa ni ya muda gani na kama itachukua muda zaidi hadi uchaguzi wa 2025, lakini ni sambamba na wakili Mwabukusi ambae aonekana tu kwamba amejiingiza katika eneo ambalo hana uzoefu nalo yaani siasa chafu.
Ni kweli wakili Mwabukusi amesoma tena amesoma kwelikweli kiasi cha kufikia kuwa wakili wa kujitegemea. Lakini siku zote ukiwa msomi ni lazima usome alama za nyakati na pia usome mienendo ya hali mbalimbali khasa siasa. Wakili Mwabukusi kujitoa katika kujadili suala la DP world tayari alijiingiza katika siasa za fitna bila kufahamu. Wengi walijitokeza kutaka kumfahamu, kumrekodi kwa asilimia 100 maneno yake mstari kwa mstari na pia baadhi ya waandishi kumuuliza mara mbilimbili kurudia kauli zake ambao kwa mtindo wa vitisho alikuwa akitoa lugha kali sana kumzidi hata Tundu Lissu.
Lakini wakati Dr Slaa na wakili Mwabukusi wanatoa kauli kali na za vitisho dhidi ya mamlaka hawakutambua kuwa miongoni wa walowazunguka wapo wanafikina mandumilakuwili ambao waliwenda kuketi na kuchambua kauli zile na kisha kuzikabithi kwa wahusika yaani jeshi la pili kwa ajili ya kufanya "analysis" zaidi.
Lengo la serikali kufanya "purge" ni nini?
Serikali kwa sasa imedhamiria kuwatolea mfano Dr Slaa na wakili Mwabukusi ili iwe funzo kwa wale wanotaka kuendeleza mjadala wa DP World. Serikali imetumia Bunge ( ambalo kidemokrasia ni wawakilishi wa wananchi) kama "rubber stamp" kuridhia mchakato wa DP world, hivyo serikali yenyewe na CCM wameamua hivyo na yaonyesha kuwa jambo hilo sasa ni rasmi na kinongojewa tu ni raisi Samia kuweka saini kuwa sheria.
Lakini hapohapo serikali imejipambanua kuwa haijiamini na lolote italosikia itafanya "purge" jambo ambalo ni hatari kwa kuwa lazuia raia kutumia haki yao ya msingi ya kuhoji na kujadili. Pili serikali kupitia mihimili yake ya mahakama na jeshi la polisi imeonyesha kuwa nchi yetu uko nyuma sana katika kuruhusu uhuru wa kusema na kutoa maoni, ingawa katika hili Dr Slaa na wakili Mwabukusi wamevuka mipaka ambayo ni dhahiri kuwa wamekashifu na kutishia mamlaka hivyo kushikishwa makosa ya uhaini.
Serikali chini ya raisi Samia S Hassan bado ina wajibu wa kuurejea mchakato wa DP world na kuangalia wapi pana hitilafu hususan ni bandari zipi zitakuwa chini ya DP World pamoja na maeneo mengine ambayo yamekwishaainishwa. Watanzania hatukatai DP world au hatukatai uwekezaji lakini ni lazima hatua sahihi na kuzingatiwa kwa maslahi ya nchi kwatimiliwa maanani.
Nchi hii ni yetu sote na hakuna mwenye haki miliki ya kudai nchi hii ni ya kwake, hakuna utawala wa kisultan ambao hufanya kila kitu ni mali yake. Pia mali za nchi hii ni mali za taifa na zingine huwa tawaziita nyara za serikali kama wanyama.
Tanzania ilifikia uchumi wa kati kati ya mwaka 2019 na 2020 na leo hii uchumi huo umepotea tena. Sababu kuwa ni usimamizi mbovu wa vyanzo vya mapato na matumizi mabaya ya fedha za umma. Bado serikali ya Tanzania chini ya raisi Samia ina kila sababu na wajibu wa kuhakikisha nchi yetu hii yapata maendeleo kwamba umeme wasambazwa nchi nzima na kuachana na mkaa, maji ya uhakika, elimu bora na watoto kuketi kwenye madawati na huduma bora za afya.
Bado kiu ya wananchi ipo palepale kuona kwamba nchi yawa na viwanda vitavyotoa ajira, kuboresha maisha ya watanzania, na kwa maoni yangu ni kwamba serikali ina kazi kubwa ya kuhakikisha kunakuwepo uwiano sawa kati ya miji na vijiji ili kuharakisha maendeleo ya pamoja jambo ambalo kwa CCM itakuwa imefanya kazi ya maana zaidi kuloko kukamatana na wanasiasa huko mabarabarani na kufanya "purges" ili kuzia hoja na mijadala.