Gerson Msigwa: Filamu ya Royal Tour hazikutumika fedha za Watanzania

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amefanya mahojiano na Wasafi TV na hii ni sehemu ya nukuu zake kuhusu filamu ya Royal Tour ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Aprili 18, 2022 Nchini Marekani:

Sababu za Wamarekani kupewa tenda
"Ile filamu uzinduzi wake ni Tarehe Aprili 18 na utafanyika mara mbili New York na Los Angels, sasa mnauliza kwa nini walirekodi wageni na si Watanzania? Unachokifanya lazima uwe na malengo.

"Sisi malengo yetu kwenye filamu hii ni kuifikia dunia na kuiambia fursa zetu za utalii na uwekezaji na biashara, sasa rafiki yangu Ukimchukua Msigwa aende akarekodi hiyo filamu si ataishia kutazama Zungu na nyie Wasafi mtanisifia tu lakini vipi kwenye kuwafikia walengwa?"

Lengo ni wasanii milioni 5 kwa mwaka
"Waliotengeneza filamu wanaenda kuizundulia Marekani, maana yake kule tayari unaanza kuwafikia watu wengi ambao ni walengwa. Tunataka watalii wafike milioni 5 kwa mwaka ikifika mwaka 2025.

"Idadi ya watalii ilishuka mpaka chini ya laki 6 kutokana na Corona.

“Ripoti ya safari hii inaonesha tumeshafikia watalii milioni 1.7 na tunataka tuendeleze hiyo kasi na tunataka pia watu maarufu duniani ambao hawakai Bombambili au Njombe, wako Los Angeles, Newyork, London huko

Hazikutumika fedha za Watanzania
"Tutapata watalii ili tupate fedha za kujenga shule, vituo vya afya na barabara na mahitaji mengine. Gharama alishazisema Mhe. Rais lakini watu wajue tu kuwa hatukutumia fedha za Watanzania. Kwanza wanaoandaa kipindi wana sera yao ya kutotumia fedha za serikali.

"Watanzania tushabikie hii filamu na tunahitaji kumpongeza sana Mhe. Rais katika hili. Miaka ya nyuma tulitaka kufikisha utalii kwenye majukwaa ya kimataifa tukaletewa bili ya mabilioni tukakimbiana."

Source: Wasafi TV

============================


Mwezi uliopita Rais Samia Suluhu Hassan alinukuliwa akisema hivi: "Tulifanya kuchangisha fedha nadhani tulichangisha kiasi cha bilioni 11 ambazo mpaka tunamaliza shooting (Royal Tour) na kila kitu, tulitumia kama bilioni 7 gharama za kila kitu. Haikutoka fedha serikalini ile yote ilikuwa ni kuchangisha mashirika."
Mashirika ya serikali.
 
Mnajua hata tukisema tunalipenda taifa hili kwa kusifia kila jambo anafanya Rais au viongozi wa kisiasa bila kufikiri nje ya box sitoshangaa ipo siku giza litalikumba Taifa hili na kila mtu aliopo leo huwenda asiwepo na uwenda yale maneno aliwahi sema Mzee Wakaya JK yakawa kweli.

Wajukuu kutafuta makaburi ya mababu zao nakufukua mafuvu na kuyachapa kwa makosa yalifanyika kipindi cha uongozi wao.

Hivi kweli samahani sana hivi kweli matajiri wa Tz wamechangia royal Tour ya Rais wa jamuhuri ya watu wa Tz na high level officer include number one anatoka mbele nakusifia matajiri wazalendo?

Mungu natubu kwa Taifa langu yani kweli ndugu zangu wa maadili ya umma mnakubaliana eti matajiri wamemchangia Rais royal tour ehe alafu kesho waliochangia mabilion mnapower kuwaambia walipe kodi au kuwazuwia wasipandishe bei wanavyo taka? Au ndio tunarudi kule tulitoka unanijuwa mm nani? Nenda kamuulize Rais wako wasaidizi wake... End

Sorry we lost the way. Hata kama hili taifa ni masikin kiasi gani hiki kitendo cha matajiri kuchangia royal tour italigharimu Taifa kwa muda usio julikana ila pia hata alio waita naku organise uwenda akawa nawakati huko mgumu mbeleni. Maana kitendo hiki japo kinasura nzuri ila kinavunja sheria ya maadili ya umma. Yes Rais ni Taasisi nasio jina au mtu. Mtu amewekwa kikatiba kusimamia taasisi. Huwezi mpelekea zawadi au mchangia Rais ila unaweza peleka zawadi kwa mtu nje ya taasisi. Well muda utasema.

Ofisi ya Rais kwa mujibu wakatiba na tume ya maadili ni ofisi hapaswi pokea asante au hongera kwa aina hii ya uchangishaji. Hakuna pesa yatajiri inatoka bila kuwa na RTN never ever we must pay and who will pay nisisi masikini. Labda uniambie pasingekuwa na miongozo ya viomgozi na watumishi wa umma. Kama mtakumbuka kuna kiongoz aliwahi pewa jiwe na mnakumbuka jinsi lile jiwe lilisumbua tume ya maadili leo amekuja kiongozi amechangisha nakuchangiwa na matajiri na ameitangaza Tz.

Kesho unakwenda na Agency notice unataka mapato jibu lake litakuwaje?

Hivi nani ametuloga mbona kama hatuwoni chochote na kila mtu anapiga makofi while taasisi ya Rais imejiingiza kwenye mgogoro wa kikatiba yani matajiri wanaichangia royal tour while vitu vinapanda at speed ya chita nani analaumiwa?

Haya nimemaliza
 
Mkuu
Tambua
Unaemsema hakuandaliwa kukalia kiti kile,Labda waandalizi HUKO mbeleni watakuwa makini kwenye uteuzi wa namba mbili!!Hadi 2025 tutashuhudia Mengi Sana coz anashindwa kujiamini anahisi kuna Godfather's wamemuweka Pale kwa hiyo anawaogopa hao waliomweka!!
Nadhani umenielewa
 
Uangalizi mzuri sana wa hoja akili na mtazamo, ikulu imepinduliwa na kufedheheshwa sana, hata kama lengo lake ni kuona aibu ya kuambiwa fisadi kwa kutumia pesa za umma vibaya hicho kichaka ameivua nguo nchi, serikali na Urais wenyewe ni aibu sana. Asante kwa hoja na angalizo lenye maslahi kwa taifa letu
 
Mkuu
Tambua
Unaemsema hakuandaliwa kukalia kiti kile,Labda waandalizi HUKO mbeleni watakuwa makini kwenye uteuzi wa namba mbili!!Hadi 2025 tutashuhudia Mengi Sana coz anashindwa kujiamini anahisi kuna Godfather's wamemuweka Pale kwa hiyo anawaogopa hao waliomweka!!
Nadhani umenielewa
Acheni wivu. Matajiri wazalendo wakichangia jambo la maendeleo ubaya ni upi? Mbona hata sisi maskini tunachangia kwa Tozo zetu?
 
Kuna haja ya kumlazimisha raisi awataje waliochangia royo tua, ili tuwaweke kwenye intensive investigation kama wanalipa kodi
Hata wakilipa kodi wewe itakusaidia nini? Pesa ngapi zinapotea mikononi mwa hao wakusanya kodi?

Acheni wivu
 
Bila shaka kutakuwa na msamaha wa kodi wa muda mrefu, kwa hao matajiri waliojitolea kuchangia hii project ya mama yetu kipenzi.

Miaka 50-100 itapendeza, maana sasa hakuna namna.
 
Alipohojiwa na Tido Muhando wa Azam aliulizwa mbona waliochangia hawatajwi kwa majina akasema uzinduzi wa Dar es Salaam atawataja, mimi sikubahatika kuangalia uzinduzi wa royal tour vp wadhamini walitajwa kwa majina?
 
Back
Top Bottom