Tujadiliane: Mwaka Mmoja Filamu ya Royal Tour Imetuletea nini?

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu kuzinduliwa kwa filamu ya Royal Tour Aprili 28, mwaka 2022 kwa ajili ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii Tanzania. Akitoa ufafanuzi kwa wanahabari mwaka mmoja baada ya kuzinduliwa kwa filamu hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt Hassan Abbas alitaja mafanikio katika sekta ya utalii yaliyofikiwa tangu kuzinduliwa kwa filamu hiyo.

Swali la msingi tunaloweza kujadili kwa pamoja ni kuwa matokeo ya filamu hiyo yanatoa taswira gani ili kuweza kujua kama mwenendo wake unaridhisha kwa kulinganisha na baadhi ya malengo yaliyokusudiwa.

Royal Tour ilikuja wakati sekta ya utali ilipodorora kutokana na kupungua kwa idadi ya wageni kutokana na janga la maambukizi ya Uviko-19.

Katika kipindi hicho, idadi ya wageni waliotembelea Tanzania ilipungua kufikia 620,000 kwa mwaka 2020 kutoka 1,500,000 waliokuwa wakitem-belea mwaka 2019 na kasi ya ukuaji wa sekta ya utalii kwa mwaka 2020 ilipungua hadi asimilia 5.3 kutoka aslimia 10.7 iliyokuwapo mwaka 2019.

Royal Tour ililenga kuchochea ongezeko la watalii hadi kufikia milioni tano kwa mwaka ifikapo mwaka 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya Dk Abbas, idadi ya watalii kutoka nie imeongezeka kutoka 620,867 iliyokuwa mwaka 2020 hadi kufikia 1,454, 920 Desemba, 2022.


Kwa mwenendo huu naweza kusema imeonyesha matokeo yanayoridhisha, ingawa inahitajika juhudi zaidi na muda ili kufikia malengo ya kimkakati ya watalii milioni 5. Royal Tour pia ilikusudiwa kuchochea uwekezaii kutoka nje ya nchi, hususan kwa kuzingatia hali ya uchumi kwa uiumla kidunia na Tanzania katika wakati wa Uviko-19 na baada ya hapo ilidorora, kwa mujibu wa ufafanuzi wa Dk Abbas.

Mpaka kufikia Machi 2023, jumla ya idadi ya miradi mipya 26 ya uwekezaji kutoka nje ilisajiliwa nchini na Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC), ikilinganishwa na miradi 16 iliyosajiliwa Machi 2020 Uwekezai; kutoka nie ni nvenzo muhimu inayoweza kuchangia ukuaji wa biashara, ajira na akiba ya fedha za kigeni, hivyo tunaweza kuse ma kuwa, Royal Tour imeonye sha kuwa azma ya kupiga ndege wawili kwa jiwe moja inawezekana

Baada ya mwaka mmoja mwenendo wake ni mzuri katika uwekezaii wa mira-di ya sekta ya utalii kwa kuongezeka uwekezaji wa makampuni ya kigeni kutoka nje ya nchi.

Sambamba na hilo, tunaweza kusema Royal Tour pia imechangia pazuri katika azma ya Serikali ya Rais Samia kuitangaza Tanzania kimataifa, kama taarifa zinavyoonyesha takribani zaidi ya watu bilioni 1.2 duniani wanakadiriwa kuwa wametazama filamu hiyo.

Vilevile, ukiacha faida zinazopati-kana katika utalii, kufuatiliwa na watu wengi duniani, inaweza pia kusaidia kufungua fursa nyingine mbalimbali za kibiashara, kwa mfano usafiri wa anga, au kupata masoko ya bidhaa za kilimo na mengine.

Hata hivyo, bado safari ya kushere-hekea matunda ya kiutalii itahitaji kuwekeza zaidi ili kuendana na ushin-dani wa kikanda na kidunia. Kufikia hatua kubwa katika malengo ya kimkakati katika sekta ya utalii itahitaji muda kuwekeza zaidi katika miradi mingine ya kukuza utalii, sera nzuri na kuondoa vikwazo vya kiuwekezaji.

Chanzo: Gazeti Mwananchi
 
Back
Top Bottom